Huyu mpenzi wangu wa zamani kunidhulumu mtoto bado sijaridhika

Barikiel

JF-Expert Member
Feb 2, 2014
403
401
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu. Niliwahi kuwa na mahusiano na Dada mmoja kumbe alikua na mwanamme mwingine lakini hakuniambia kabla nilivyo ji ingiza ndo akaniambia ana bwana na in Dereva wa mabasi. Akaniambia yule bwana amekaa nae mda mrefu ameshindwa kumjaza mimba. Akaniambia nikibeba mimba tu namkimbizia Frenk. Jina siyo halisi, kweli tukaenda kupima afya tukaendelea na maisha sisi tuko Mwanza Frenk yupo DSM. Kweli baada ya mwezi tu, kitu kikatinga mwanamke kanitoroka kimya kimya kampelekea Frenk mimba. Frenk kalea mimba hadi mtoto, nimejaribu kuwasiliana na huyu Dada lakini imeshindikana nimeongea na Mama mkwe nae ananitukana. Naombeni msaada wa mawazo nifanyeje nimpate mwanangu. Au nisubiri mtoto ajitambue nimfuate mwenyewe? Mtoto yupo darasa la kwanza sasa hivi. Nairudia hii mada Mara ya pili. Jamani matusi sivyo naomba ushauri. Nawakilisha
 
'Mkwe' rekebisha hapo kwanza sababu sio kauli fasaha kumuita mkwe wakati humkuoana bali ni wapenz tu.. Mpe heshima mama wa mkeo kwa kumwita "mkwe"
 
Nenda ufungue kesi una uhakika gani kuwa mimba ilikuwa yako..!?
au subiri akitaka mtoto was pili atakitafuta
 
Mtoto wa pili tayari anae, ila hafanani na huyu jamaa hata nukta 1 nikiweka picha ya mwanagu hapa na mimi hakuna haja ya DNA
 
Nenda kwenye vyombo vya sheria uchukue mwanao. Na km baba usisubirie mtoto afike darasa la 5 ndiyo uende, ajabu naye atakukana. Atakuuliza'' ulikuwa wapi siku zote?''
MCHUZI WA MBWA HUNYEWA WA MOTO
 
Wewe jamaa sijui vipi yaani umeona kabisa shamba sio lako, ukatupa mahindi sasa yameota unadhani utaweza kwenda kuyavuna kwa kigezo eti wewe ndio uliye tupa mbegu za mahindi kwenye shamba ambalo sio lako
 
Sawa shamba sivyo lako, lakini kumbuka nimeandikaje hapo. Alijenga kwanza mahusiano then kafunguka baadae.
 
Hata kama alijenga mahusiano na wewe, na isitoshe ulijua kabiaa kwamba akipata mimba atabambikia mumewe, bado ukaendelea kujifanya unajua kupenda sana, sasa utafanya nini aisee, shamba la jirani hilo huwezi vuna mazao yake
 
Tafuta demu mwingine umjaze mimba , fikiria Mara mbili maana unauweza hata akakuzuru huyo jamaa
 
Mama mkwe ndio mama yake nani umemwita hivyo!?

Ila mwanamke huyo alikueleza kila kitu na ukamsikia.. inabidi uwe mdogo mdogo ujinyamazie kimya.. mipira ilikuwepo ambayo ungeitumia.. au ulifikiri dereva sio binadamu na anaweza kupendwa?

Muombee mema mwanao na omba Mola akupe nafasi uonane nae siku moja na akutambue wewe ni baba mzazi.. omba huku ukiwa na imani kubwa.
 
Mkuu, nilipata mshtuko mkubwa sana hasa hapo ulipo andika jina la Frank...... Duhhhh.....
 
Anaelea mimba ndo baba wa mtoto, ahhh jiliwaze hata mimba haikuwa yako kwan unafikiri mdada walikuwa na frenk tu???

Wacha Maneno oa wako akuAliw mtoto
 
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu. Niliwahi kuwa na mahusiano na Dada mmoja kumbe alikua na mwanamme mwingine lakini hakuniambia kabla nilivyo ji ingiza ndo akaniambia ana bwana na in Dereva wa mabasi. Akaniambia yule bwana amekaa nae mda mrefu ameshindwa kumjaza mimba. Akaniambia nikibeba mimba tu namkimbizia Frenk. Jina siyo halisi, kweli tukaenda kupima afya tukaendelea na maisha sisi tuko Mwanza Frenk yupo DSM. Kweli baada ya mwezi tu, kitu kikatinga mwanamke kanitoroka kimya kimya kampelekea Frenk mimba. Frenk kalea mimba hadi mtoto, nimejaribu kuwasiliana na huyu Dada lakini imeshindikana nimeongea na Mama mkwe nae ananitukana. Naombeni msaada wa mawazo nifanyeje nimpate mwanangu. Au nisubiri mtoto ajitambue nimfuate mwenyewe? Mtoto yupo darasa la kwanza sasa hivi. Nairudia hii mada Mara ya pili. Jamani matusi sivyo naomba ushauri. Nawakilisha
Use common sense huyo demu alikuja kwako ili aokoe ndoa yake. So ulipomkubaria hiyo ndo ikawa faida kwake.
Hivyo basi tulia kabisa tafuta demu mwingine mpe mimba au oa kabisa alafu subiri mtoto awe mtu mzima kabisa atakuja kukutafuta tu. For now usiharibu ndoa ya watu. Kwani ilichokifanya ulijua kabisa nini kitatokea. Kaa mbali nao na endelea na maisha yako.
 
Mpaka frenk afe ndo utapewa huyo mtoto. Ukitanguliya wewe ndo basi tena
 
Mama mkwe ndio mama yake nani umemwita hivyo!?

Ila mwanamke huyo alikueleza kila kitu na ukamsikia.. inabidi uwe mdogo mdogo ujinyamazie kimya.. mipira ilikuwepo ambayo ungeitumia.. au ulifikiri dereva sio binadamu na anaweza kupendwa?

Muombee mema mwanao na omba Mola akupe nafasi uonane nae siku moja na akutambue wewe ni baba mzazi.. omba huku ukiwa na imani kubwa.
Wewe angalau ume nena. Asante mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom