Huyu mkaka mbona simuelewi??? nisaidieni mawazo wanajf

Kama unaona hakufai achana naye...na kama unampenda mwambie aache ubaili akutwae uwe mwandani wa yeye.
 
jamani nishaurini vizuri sitaki nipendeze lakini angalau angeonesha vijidalili hali yangu ya maisha anaijua na anajua sina wa kunihudumia lakini pengine anadharau hata hivyo suala la kunionja asiweke akilini mwake hata angenihudumia kiasi gani natunza heshma yangu

hiyo heshima umeanza kuitunza alipo kutongoza au uliitunza tangiapo? wewe ni bikra?. mia
 
',,,dunia hii dunia ya leo muda mwingne wakosa mwelekeo..nashukuru nimempata mwenye upeo...naimani nataraji maendeleo'SUMA LEE 2011,

Binti ,nionavyo upo kimtindo naye...maana mpaka amemwona mzaz yamkini upendo unao ila tatizo wapenda kijana asiyomudu kwa kadri muda ulivyo......
 
heheheheheiya....hayo mapenzi mapeziiiii?duuu wrong number imekua mchumba,huyo kitombi huyo.....tena mnataka kuleta mambo ya tamthlia ,hz cm hiz mmmmmh,kubali akuwowe,ila hujue huo ndo mchezo wake,akipiga kwang,na hv nna sauti nyororo atazimika tena,tutakua ryvals lol....
 
hahhaha amina ali you have made my weekend hasa sentensi ya mwisho imenipunguzia uchovu najua umahanishi umeamua tu kutania wakaka wa jf mana hiyo sentensi hawaipendi kabisa.nimecheka kweli.By the way huoni kwamba huyo ni stranger kwako yani mtu hakujui anaongea direct na mama yako?my dear matapeli wanatumia sana hiyo mbinu kuwa mwangalifu.
 
niotee namba yako nami nipige hiyo wrong ...............mimi ukinikaribisha kwenu NAJA NA BARUA YA POSA
 
mmmh...huyu dada na stori yake wote manyoyaaa!! Hali ngumu kimaisha huku unaweza kununua bundle la mtandao uingie jamii forum...tupa kuleeeee!!!!!
 
akuhudumie kwani we kiwete?

mimi si kiwete nashkuru ila nilimueleza historia ya maisha yangu na zaidi nahitaji kusoma tangu afariki baba nimekosa msaada wa kifamilia ila ukweli baada ya kumuona nilimpenda kweli lakini sasa ananirudisha nyuma
 
nimeshaelewa moral of the story.

'unatangaza njaa hapa ili upate mdebwedo? Jibu basi PM, mie ntakuendeleza hadi uchoke kusoma mwenyewe, ada tu hainishindi aisee.

mimi si kiwete nashkuru ila nilimueleza historia ya maisha yangu na zaidi nahitaji kusoma tangu afariki baba nimekosa msaada wa kifamilia ila ukweli baada ya kumuona nilimpenda kweli lakini sasa ananirudisha nyuma
 
Khaaaaa.....
Hata vocha hajakuhudumia....?
Unaogopa Kama Ana mapenzi ya dhati?
Daaaaaa....jamani dunia ina viroja....
Kama unaona pesa ndo mapenzi basi muombe pesa, umpime
Mweeeeeeeeee.....
 
Sasa amtwae kwa vocha ama kwa kumuachia atm card yake?
Soma last sentence uelewe concern yake, anapendwa ila hajawahi kutumiwa vocha!
Kama unaona hakufai achana naye...na kama unampenda mwambie aache ubaili akutwae uwe mwandani wa yeye.
 
mimi si kiwete nashkuru ila nilimueleza historia ya maisha yangu na zaidi nahitaji kusoma tangu afariki baba nimekosa msaada wa kifamilia ila ukweli baada ya kumuona nilimpenda kweli lakini sasa ananirudisha nyuma
Wanaume sie tunachelea kuwagharamia maana hamchelewi kugeuka nyie akina Amina..na kutafuta makuu zaidi.
 
duh hii kali yan mtu humfahamu kiundan afu katangaza ndoa mpk kaja na kwenu we unamkubalia tu. . . ama kweli mdada upo desperate na ndoa. je mkishindwana utakuja kumpeleka mwingne. huon aibu?
 
Shosti mbona umejishusha Sanaa bei? Yani karudi tena kukupigia baada Ya kukosea number,ukaongeanae ukampa nafasi mpaka akuzowee mpaka ukampa cm mzazi nae akaongea mkamuelekeza akaja nyumbani,kwa hiyo ww pia ulimuona kwa mara ya kwanza alipokuja nyumbani ? Kwani ww shida yako hela zake au mumemwenye mapenzi ya kweli na mwenye tabia inayokuridhisha?
 
habari zenu wapendwa, kuna kaka mmoja alinipigia sim lakini akawa amekosea namba baada ya kujua kua kakosea akaniomba samahani nami nikaendelea na zangu, kilichonishangaza alinipigia tena na kunambia kuwa kavutiwa na sauti yangu hivyo kanipenda vyovyote nilivyo na lengo lake ni kuoana, sikumpa jibu rasmi ikawa tunaendelea kuwasiliana akaomba aongee na mama nikamkubalia sasa alipoongea nae akajitambulisha kuwa mimi ni mpenzi wake anataka kuja ili wajuwane, basi akafahamishwa mpaka nyumbani akaja akakaribishwa vizuri, sasa baada ya kuondoka akanitumia sms na kusema kuwa kazidi kuchanganyikiwa anaomba nisimtose nimkubalie tu ili aniowe, swali lipo hapa huyu jamaa hajawahi kunihuduia hata sent zaidi ya vocha nimaneno matupu hivi nikweli ana mapenzi yakweli? nisaidieni jamani nisijejuta kwa uamuzi nitakaotoa.

mruhusu aingize,,, senti zitatoka tu....si mmetugeuza ATM ,
alaah we unataka hela au mapenzi......?
 
Naamini atakuwa hakufai kwa sababu mko mna malengo tofauti yeye anatafuta mke wewe unatafuta ATM!
 
Daaaaaaaah! We wa ajabu sana! Yan unadhani ukipewa pesa ndio una pendwa? Mapenzi ya kweli haya pimwi kwa pesa binti! Unaweza kupewa pesa na ukaambulia maumivu!

Ebu msikilize kijana huyo ana onekana ana nia nzuri nawe!
 
Duh! Sijui nisemeje?ngoja nipite tu khaaa maana watu wana haraka kuliko upesi, mtu hujawahi hata kumuona unamkaribisha straight kwenu kama jambazi je??
 
Back
Top Bottom