Huyu mgonjwa wa mguu makutano ya Ubungo anajimaliza mwenyewe

Msaidie. Mchukue mpeleke hospitali, sasa kuja kumuanika humu JF itasaidia nini?
Watanzania tukoje?

Jama ile tu kuleta hii post jf ni kamsaidia vya kutosha..Mimi mwezi wa tisa nilimpa huyo jamaa Tshs.5000 baada ya kuuona kwa mbali mguu wake huo nikamsogelea nakumpa..


Hivyo kama una uwezo wa kumsaidia msidie ila usihoji jamaa kuleta hii post jf.
 
Hicho kitu cheupe kwenye mguu sio kwamba kitu kimefungwa bali ni usaa uliotanda kuzunguka eneo hilo

Kila nimipita Ubungo kurejea nyumbani muda ya jioni mara nyingi namuona kijana huyu akiwa na kidonda kikubwa sana kwenye mguu wake wa kushoto

Muda wote anazunguka kutoka gari moja kwenda jingi akipata fedha kidogo anazozitumia kwaajili ya chakula

Kwasasa mguu wake umefikia hatua nzito zaidi kuliko hapo mwanzo ambapo alikuwa na nafuu sana

View attachment 958722

Najiuliza kwanini asichukue uamuzi wa kwenda Hospitali?

Niliwahi kumshauri hivyo lakini nikabaini anatumia kidonda chake kujiingizia kipato

Kifupi hajali uhai na afya yake, nilimwambia hata akienda Muhimbili hakuna wa kumfukuza hata kama hana fedha

Licha ya kuendelea kuharibu mguu wake lakini anawaumiza sana mioyo wapita njia
Japokuwa picha imetokea giza nahisi kama nishawahi kukutana nae ila ni mbagara Zankem Kuna mlemavu pale siku hiyo naludi kazini akaniomba msaada wa nauli kwenda vikindu nikampatia cha ajabu siku ya pili nika mkuta pale pale stend ana muomba mtu mwengine ili bidi nimsogelee niongee nae kwa dakika chake nilicho Kuja kugundua ile ajali aliyo Pata iliondoka na akili zake nusu na watu wengi huwakuta hali hii mungu amsaidie.
 
Swal la kujiuliza hiko kikamptula kilipita vipi kwenye uo mguu?
Unataka ela alafu unadanganya watu juu juu, pumbavu sana ao


Labda kina zip huko kwenye mshono chini kuelekea HQ
 
Watanzania tukoje?

Jama ile tu kuleta hii post jf ni kamsaidia vya kutosha..Mimi mwezi wa tisa nilimpa huyo jamaa Tshs.5000 baada ya kuuona kwa mbali mguu wake huo nikamsogelea nakumpa..


Hivyo kama una uwezo wa kumsaidia msidie ila usihoji jamaa kuleta hii post jf.


Na ukimsaidia usije kujitangaza kuwa umempa kitu fulani, sadaka sharti iwe siri yako wewe na yeye
 
Hicho ni kitega uchumi chake, kikipona ni sawa na kisima cha maji kukauka, atakufa kiu, hawezi kukubali kutibiwa huyo, muda mwingine matatizo ni mtaji kwa wavivu
 
Mjini hapa, wengine si vilema hujifanya vilema, hata huyo yawezekana kajiweja vitu fulani ili uone kuna tatizo. Kuna mjamaa fulani anatega bondeni Mbezi beach kwenye kichochoro cha eneo la jeshi kuekekea Kawe. Yule hana kidonda bali hujirundika mabandeji na kutia rangi kwa juu.
Kuna mama mmoja yuko Mbezi juu karibu na kanisa la KKKT ana nyumba na wapangaji ndani kwa kazi ya kuomba huko mjini
 
pia yuko mmoja kati ya taa za kuongozea magari vingunguti na tazara ukimuona utajua stroke imempiga ila ni mzima kabisa.
 
Kaka umedanganyika na ukaamini. Huo mguu hauna kidonda sisi tushawahi kumkamata huyo jamaa na kumfungua hiyo bandeji alikuwa analia kama anachinjwa. Kumaliza kumfungua rapurapu la nyama likadondoka puuh. Akaishia kusema washkaji kausheni basi maisha magumu. Na aliyetushtua kuwa anajifunga nyama ni dada mmoja mfanyakazi wa clouds. Hatukuamini kama wewe usivyoamini.
Duuu,,usinambie. Mi nilimuona nikahsi kutetemeka. Ila mguu wake umevimba?? Na hilo linyama kalibandika eneo la weupe tu? Hebu nieleweshe mdau
 
Una uhakika ni kidonda? Kuna mwingine alikuwa na ''donda'' kubwa la kuogovya sehemu za tumbo. Akifunua kuomba msaada utataka kumpa kwa haraka ili aondoe kero. Ikaja kugundulika ni kipande cha ngozi ya ng'ombe mbichi huwa anajibandika kwa kuigeuza!
Haiozagi?? Au anabadilisha
 
Achana naye huyo. Hana kidonda wala usaha. Huwa kuna materials fulani wanazungushia mguuni au mkononi na mguu au huo mkono huonekana kama una kidonda kikubwa au usaha mwingi.
Hu ungekua usaha hata yeye asingepata nguvu ya kwenda kuzurula barabarani. Usaha usikie hivihivi tu.
Hapo ndio umeongea, usàa wa kumwagika halafu mtu anazunguka mtaani!!! angukuwa na homa sana.
 
atkufa kunateja hapa kitaa nguu alikuwa anautumia kama hivyo siku anahangaika kufa watu wanamtizama tu kama masaa sita mateja wenzie kumpeleka tu akanyooka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom