Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Kila nimipita Ubungo kurejea nyumbani muda ya jioni mara nyingi namuona kijana huyu akiwa na kidonda kikubwa sana kwenye mguu wake wa kushoto
Muda wote anazunguka kutoka gari moja kwenda jingi akipata fedha kidogo anazozitumia kwaajili ya chakula
Kwasasa mguu wake umefikia hatua nzito zaidi kuliko hapo mwanzo ambapo alikuwa na nafuu sana
Najiuliza kwanini asichukue uamuzi wa kwenda Hospitali?
Niliwahi kumshauri hivyo lakini nikabaini anatumia kidonda chake kujiingizia kipato
Kifupi hajali uhai na afya yake, nilimwambia hata akienda Muhimbili hakuna wa kumfukuza hata kama hana fedha
Licha ya kuendelea kuharibu mguu wake lakini anawaumiza sana mioyo wapita njia