Huyu mgonjwa wa mguu makutano ya Ubungo anajimaliza mwenyewe

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
IMG_20181206_205708.jpg
Hicho kitu cheupe kwenye mguu sio kwamba kitu kimefungwa bali ni usaa uliotanda kuzunguka eneo hilo

Kila nimipita Ubungo kurejea nyumbani muda ya jioni mara nyingi namuona kijana huyu akiwa na kidonda kikubwa sana kwenye mguu wake wa kushoto

Muda wote anazunguka kutoka gari moja kwenda jingi akipata fedha kidogo anazozitumia kwaajili ya chakula

Kwasasa mguu wake umefikia hatua nzito zaidi kuliko hapo mwanzo ambapo alikuwa na nafuu sana

IMG_20181206_205656.jpg

Najiuliza kwanini asichukue uamuzi wa kwenda Hospitali?

Niliwahi kumshauri hivyo lakini nikabaini anatumia kidonda chake kujiingizia kipato

Kifupi hajali uhai na afya yake, nilimwambia hata akienda Muhimbili hakuna wa kumfukuza hata kama hana fedha

Licha ya kuendelea kuharibu mguu wake lakini anawaumiza sana mioyo wapita njia
 
Achana naye huyo. Hana kidonda wala usaha. Huwa kuna materials fulani wanazungushia mguuni au mkononi na mguu au huo mkono huonekana kama una kidonda kikubwa au usaha mwingi.
Hu ungekua usaha hata yeye asingepata nguvu ya kwenda kuzurula barabarani. Usaha usikie hivihivi tu.
 
Hawa jamaa waone tu hivi, kuna mzee yupo pale makutano ya Morogoro road na "Muhimbili road", nilivyokuwa namuona nilidhani ni mgonjwa haswa. Siku moja nikapishana nae mtaa wa jangwani yupo safi anatembea vizuri hana shida yoyote, nikadhani amepona.

Baada ya siku kadhaa nikamuona tena katika hali mbaya, nikajua kumbe hizi fix tu. Wengi ni waongo...
 
Duh aisee lakini ukimcheki mchana unaona kuna jeraha pale
 
Hawa jamaa waone tu hivi, kuna mzee yupo pale makutano ya Morogoro road na "Muhimbili road", nilivyokuwa namuona nilidhani ni mgonjwa haswa. Siku moja nikapishana nae mtaa wa jangwani yupo safi anatembea vizuri hana shida yoyote, nikadhani amepona.

Baada ya siku kadhaa nikamuona tena katika hali mbaya, nikajua kumbe hizi fix tu. Wengi ni waongo...
Ha ha ha ha haaa ungemchana live
 
Haha wabongo wanajua sana kujiongeza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom