Huyu member anayejiita UMUGHAKA anatakiwa apewe tuzo ya utunzi wa hadithi

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
10,485
34,788
Jamii forums ina watunzi wengi wa visa vya kubuni na vingine vya kiuhalisia katika maisha yao, Ila huyu mwamba UMUGHAKA ametia fora, sidhan kama kuna member anamzidi Kwa simulizi zake zenye kutisha na kusisimua pia.

Thread zake zimekuwa zikifatiliwa Kwa ukarbu Sana na member wengi kuliko kawaida, mtiririko wake ni wenye kuvutia kiasi kwamba akianza kusimulia unatamani aendelee mpaka mwisho.

Huyu jamaa ana kipaji cha uandishi haijalishi visa vyake ni vya kweli au vya kutunga.

Sijui vituo vikubwa vya televisions eg ITV, TBC, WASAFI TV, STAR TV, CLODS TV , Chanel Ten etc wanakwama wapi kupata script tamu kama hizi Kwa ajili ya tamithiliya.

Simulizi Kali kabisa Kwa sasa Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe
Japo katoa nyingine pia, Uzi unakimbia Kwa speed ya 6G.

Salute Sana kwako UMUGHAKA
 
UMUGHAKA kuna kipindi alikuwa naanifanya naweka bundle ili nifahamu siku atakayomla mwise.

Btw ni mtunzi mzuri pia ana akili especially kwenye matumizi ya methali huwa napenda sana matumizi ya methali kwenye mazungumzo tu ya kawaida.

Mfn kwenye ile story ya kichawi kuna sehemu anasema alichelewa kurudi home akakosa msosi ila hakujali kwa sababu anafahamu kuwa MZURURAJI HULA MIGUU YAKE.
 
Sijasona uzi wake hata mmoja ,ila kwa trend ninayoiona kwenye views , comments na uzi mda wote upo juu huyu mwamba anahitaji pongezi amefanikiwa kuiteka Jf.Natamani siku nipate muda wa kusoma vizuri nyuzi zake zote nishudie yaliyomo.
 
Jamii forums ina watunzi wengi wa visa vya kubuni na vingine vya kiuhalisia katika maisha Yao , Ila huyu mwamba UMUGHAKA ametia fora , sidhan kama kuna member anamzidi Kwa simulizi zake zenye kutisha na kusisimua pia , thread zake zimekuwa zikifatiliwa Kwa ukarbu Sana na member wengi kuliko kawaida , mtiririko wake ni wenye kuvutia , Kias kwamba akianza kusimulia unataman aendelee mpak mwisho...

Huyu jamaa ana kipaji cha uandishi hata kama visa vyake ni vya kweli au vya kutunga ....
Sjui vtuo vikubwa vya televisions eg ITV, TBC, WASAFI TV , STAR TV, CLODS TV , Chanel Ten etc wanakwama wapi kupata script tamu kama hz Kwa ajili ya tamithiliya....
Simulizi Kali kabisa Kwa sasa Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe
Japo katoa nyingine pia , Uzi unakimbia Kwa speed ya 6G

Salute Sana kwako UMUGHAKA
UMUGHAKA apewe PhD yake ya heshima. Huyu ni shaban Robert wa kizazi chetu.
Namshauri UMUGHAKA haraka ajisajili BASATA, ili kazi zake ziweze kutunzwa kisheria midudupori isije ikaziiba na ikafaidi jasho la kijana wetu wa Kikurya
 
Sijasona uzi wake hata mmoja ,ila kwa trend ninayoiona kwenye views , comments na uzi mda wote upo juu huyu mwamba anahitaji pongezi amefanikiwa kuiteka Jf.Natamani siku nipate muda wa kusoma vizuri nyuzi zake zote nishudie yaliyomo.
Mimi nilikuwa nadharau Uzi wake nikiuona always upo juu, nikawa najua ndo Yale Yale ya simulizi za hovyo , aisee juzi nikajichanganya kuufungua mbona nimeshuka nao wote 😁😁😁
 
Ngoja leo niamke naye... Sijawahi kumsoma na ndo namsikia kwa mara ya kwanza muda huu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom