Huyu Mama Spika anamtisha nani na hizo kanuni zake...?

Micho

JF-Expert Member
Apr 12, 2009
1,122
1,246
Wakuu wa kazi naomba mnieleweshe nataka kujua kwanini tokea huyu mama aapishwe speech yake ya kwanza anasisitiza kanuni..jana wakati wakuahirisha bunge amesisitiza tena mkasome kanuni.....ana maana gani?
 
Dalili ya woga!
Hajui kuwa wengi wao mle ni wanasheria so izo kanuni kwao ni kama kumsukuma mlevi ukizingatia washakamua MACAP ya kutosha vyuoni
 
Yeye mwenyewe hasijui vizuri hasa ukizingatia kuwa kazi uspika alipigiwa simu na akina Makamba mara tu baada ya uchaguzi kupita akaambiwa akachukuwe form ya uspika.
 
Wakuu wa kazi naomba mnieleweshe nataka kujua kwanini tokea huyu mama aapishwe speech yake ya kwanza anasisitiza kanuni..jana wakati wakuahirisha bunge amesisitiza tena mkasome kanuni.....ana maana gani?

1.Huyu Mama amezeeka hataki kufikiria .hajui kanuni ni mawazo ya watu waliyokubaliana wakayaandika na hajui toka wameyaandika ni muda mrefu yanahitaji kuwa reviewed
2. Anafahamu kanuni zimeandikwa kuwalinda na kuwafurahisha watawala na yeye hataki kuwaudhi waliomweka asije akawa kafara kama sita. Lakini amini nawaambieni. Vitu vilivyoivuruka Kenya ni katiba na hivyo huyo mama asipobadilika watanzania watambadilisha kwa nguvu
 
huyu mama ataimaliza ccm, ndiye atakayewafanya watz waichukie ccm kupita kiasi na 2015 ccm ikashindwa kwasababu wananchi wameichoka..hii ni kwasababu ya kauli zake, hana hekima wala busara, bali ana kauli za ukali, amri etc. ni bora wamemuweka ili achafue zaidi na upinzani tupate credit.
 
1 - hazijui kanuni kwa kuwa ubongo wake ulishachoka, na alitumia muda wa unaibu spika vibaya - hakujifunza kanuni na hivyo anadhani kila mtu hajui kama yeye.

2 - anafahamu asilimia kubwa kama si 90% ya wabunge wa ccm ni vilaza, makanjanja wa kutupwa ambao hawaelewi chochote kuhusu bunge na wajibu wao kama wabunge. NA

3-anaogopa upinzani kuovershadow bunge maana akili za wapinzania zinachemka tofauti na za makanjanja ya ccm
 
Jamani muacheni mama wa watu. Yeye kama Yohana Mbatizaji anayo kazi pevu ya kumsafishia njia rais mtarajiwa kutoka CCM. Na hivyo anafanya kila awezalo kujaribu kupata kaupenyo kidogo katika kununi zilizopo katakaomwezesha kutimiza wajibu huo wa kumsafisha huyo rais mtarajiwa na wapambe zake. Habari zisizo za kuaminika zinasema kwamba, mmoja wa wapambe hao, aliyebobea katika fani ya sheria na ambaye huko nyuma aliwahi kuwa mshauri mkuu kwa masuala ya sheria kwa serikali ya Banana Republic ndiye aliyepewa jukumu la kumuongoza mama huyo katika utekelezaji wa kazi hiyo ngumu.
 
huyo spika kaingia hapo kwa influence ya lowasa na rostam sasa inavyoonekana bunge litamshinda mapema sana
 
Wakuu wa kazi naomba mnieleweshe nataka kujua kwanini tokea huyu mama aapishwe speech yake ya kwanza anasisitiza kanuni..jana wakati wakuahirisha bunge amesisitiza tena mkasome kanuni.....ana maana gani?
Uoga ila hakuna namna, ni bora tu akubaliane na situation.
 
Hata mimi nilivyoandikishwa darasa la kwanza enzi hizo nilikuwa kila wakati naimba Ba be bi bo bu! Ma me mi mo mu. Ndicho anachosisitiza Anna kwa wabunge wa ccm. Sasa asichoelewa speaker ni kwamba katika lafidhi ya kiingereza hiyo bu ya mwisho hutamkwa ba. Kwa mwendo huu wa kukariri mpinzani tu akitokea kutamka ba be bi bo ba speaker atakimbilia kumpa adhabu. Hapo ndipo itakapokuwa hapatoshi na madhara ya kukariri yataonekana dhahiri.
 
Back
Top Bottom