Huyu mama amenikoroga sana akili yangu jana

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,019
3,987
Jana nilikutana na mama flani karibia kuwa mtu wa makamo ana watoto wake ila bahati mbaya watoto wake sijawahi kumuona baba yao ila mmoja tu nina uhakika baba yake namfahamu maana ni rafiki yangu.

Jana nilimpa story ya rafiki yangu mmoja ambaye ni kijana wa miaka isiyozidi 29 kuwa aliniambia bro sijawahi kumuona baba yangu kwa macho.

Yule mama alinijibu kwa mkato tu akaniambia nenda kamwambie huyo dogo vile anafanya kazi afanye kazi kwa bidii sana na kutumia akili nyingi kama ni mfanyabiashara afanye kwa nguvu zake zote muda si mrefu baba yake atajitokeza tu kutoka shimoni huko aliko.

Hadi sasa nimechanganyikiwa kwa majibu ya huyu mama sijui la kufanya
 
Mkuu samahani. Naomba uniambie uhusiano uliopo kati ya Diamond, Esma, Queen Darleen na Ricardo momo. Je wameshare mama, baba au ni ndugu ndugu tu?
.........ila nmeskia mama chibu amesema baba ake Ricardo ....ndo baba ake plutnumz
 
.........ila nmeskia mama chibu amesema baba ake Ricardo ....ndo baba ake plutnumz
Sasa Mkuu mama yake Ricardo ni nani? Mama yake (Baba yake) Esma ni nani? Queen darleen vipi baba yake/mama yake? Ndo kiti kinanifikirisha kidogo.
 
Jana nilikutana na mama flani karibia kuwa mtu wa makamo ana watoto wake ila bahati mbaya watoto wake sijawahi kumuona baba yao ila mmoja tu nina uhakika baba yake namfahamu maana ni rafiki yangu...
Nah! mama aseme baba ni Nani hali ya kuwa Bado dogo ni maskini,asisubiri mpka apate pesa,coz akizipata watajitokeza wababa wengi mwishowe watamchanganya
 
Hivi vitu kwenye maisha huwa vipo sana, binafsi tangu niwe na akili timamu nimemuona Baba yangu mara mbili pekee.

Maisha lazima yaendelee.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom