Huyu Likwelile aliyeachwa kuunganishwa na Kitilya ni Yupi?!!!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,022
114,394
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), tarehe 1/4/2016 iliwafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon.

Washtakiwa wote walishtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na.333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na.12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na.12 ya Mwaka 2006 ‘Anti-Money Laundering Act’.

Lakini mtu muhimu sana anaitwa Likwelile ameachwa,sababu za kuachwa hazipo wazi..Sijamjua vizuri huyu mtu kwenye hii big deal.Magufuli na system humjui pia huyu jamaa? Basi Bana
 
Ametajwa Mahakamani kuw ameachwa au? Labda wamemuweka kama shahidi no 1! Kesi ndio imeanza! Tusubiri!
 
gazeti la Mwanahalisi lilidokeza kwamba yuko nchini Marekani kubembeleza MCC irejeshwe .
 
Ni katibu mkuu wizara fedha anajuwa mengi.Akiguswa atamwaga mboga.Kumbuka tangu Escrow yupo.
 
Tunasubiri utamuuuu raaaaahaaaa, yeye yumo kivipi, tiririka mtoa post
 
Pesa ya umma haiwezi kutolewa na mtu au kampuni binafsi bila kimshirikisha mtumishi wa umma atakayepitisha malipo
 
Kwani kafanya nini? yaani mleta hoja unataka tu kumwingiza mtu kwenye skendo ya watu wengine? Tuambie kwanza Likwelile anahusika vipi na hiyo saga ya EGMA.
 
Ni kweli kwamba ukiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha unajua mambo yote yanayoendelea kwenye mabenki?

Gavana wa BOT ndio alitakiwa aunganishwe hapo kwani fedha taslimu kiasi hicho haziwezi kutolewa bila BOT kufahamu!! Kumbuka fedha ziikuwa zinatolewa $$$$ taslimu!!!
 
Gavana wa BOT ndio alitakiwa aunganishwe hapo kwani fedha taslimu kiasi hicho haziwezi kutolewa bila BOT kufahamu!! Kumbuka fedha ziikuwa zinatolewa $$$$ taslimu!!!

Ahsante sana Mkuu. Hata mimi nafikiri hivyo. Ni vigumu sana KM wa Hazina kuelewa kiinachoendelea kwenye mabenki. Jipu letu hapa ni Gavana wa Benki kuu. Na hii si mara ya kwanza haya "madudu" kufanyika bila benki kuu kuchukua hatua.
 
Kwa akili ya kawaida EGMA walifanya kazi ya udalali. Kama serikali iliajiri dalali pasipohitajika, watumishi wake washitakiwe na madalali wawe mashahidi.
Ni rahisi kuthibitisha kesi hii dhidi ya watumishi wa serikali kuliko EGMA kama siasa itawekwa pembeni.
 
Back
Top Bottom