Huyu kocha ataivusha kweli Simba Queens huko Kenya?

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Jun 12, 2021
1,061
2,475
Kanda ya Unaf washatoa mshindi anayeenda champions league ya wanawake africa , wana simba tuna matarajio makubwa simba ashinde zone ya cecafa huko nairobi next month na kukata ticket ila jana wameonyesha kiwango duni, matter of fact wameonyesha kiwango duni tangu siku ile wanacheza na twiga stars wakikabidhiwa kombe lao.

Ni kama vile kina dada wameridhika na ubingwa wamepandisha mabega wanacheza kama ma slay queens, nawaonya kwamba kwenye kundi lao wako na wale kinadada wa Uganda watakula kipondo cha mbwa koko kwa mwendo wanaoenda nao.

Cha kushangaza simba dakikaa za mwisho wakampeleka musa mgosi u-20 ya wanaume na kumleta kocha mpya ambaye jana anajitetea kwamba ndo anaanza kutengeneza team, hata kama waliowapiga 4-0 ni under 17 ywa wavulana ila recently hao ma slay quens wanazengua, MNATUKERA unamtoaje Mgosi aliyekuwa amezoeana na team kwa muda mrefu huyu akifeli nairobisi ataanza kusingizia hakuwa na muda wa kujiandaa na kuanza kuomba apewe muda kujenga team?

koach 1.PNG

koach 2.PNG
 
Amecheza na vijana ulitegemea nini?
umesikia kauli ya kocha?nilkuwepo uwanjani kabadili mfumo kabisaaaa siyo style ya mgosi,muda unatosha kupafomu mfumo wake? maana kuna mbungi next month la cecafa,anacheza counter attack wachezaji iliwashinda kabisa
 
Watakaa sawa tu, ndio maana ya training kaka.
Kua mpole
umesikia kauli ya kocha?nilkuwepo uwanjani kabadili mfumo kabisaaaa siyo style ya mgosi,muda unatosha kupafomu mfumo wake? maana kuna mbungi next month la cecafa,anacheza counter attack wachezaji iliwashinda kabisa
 
Kama ni kweli Simba wamembadilisha kocha wa Simba Queen Mgosi wakati timu ina mashindano makubwa ndani ya mwezi mmoja ujao basi hilo wamefanya kosa la kiufundi. Na timu ikifanya vibaya walaumiwe viongozi waliofikia maamuzi hayo ya ovyo kabisa.

Lakini huyo Mgosi ana tuhuma huko youtube kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Simba queen toka Kenya. Tafadhali Mgosi na hata viongozi wa Simba wanapaswa kuzijibu haraka vinginevyo wazazi watakuja kugomea watoto wao wa kike kucheza mpira wa miguu. Kama tuhuma anazotoa huyo mchezaji ni za uongo basi ashitakiwe haraka kwa kuiharibu "brand" kubwa ya Simba. Na iwapo tuhuma ni za kweli basi huyo mchezaji aombwe radhi na alipwe fidia pia atangazwe kuwa shujaa wa kuvunja ukimya kwani inawezekana wenzake wanaumia kimya kimya huko kambini.

Na link yenyewe ni hapa . Isikilizeni mwishoni kabisa ndio tuhuma dhidi ya udhalilishaji wa kocha na mambo ya kichawi juu ya Simba queen kutumia waganga wa kienyeji.
 
Pumbavu sana huyo kocha wa simba

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Pumbavu sana huyo kocha wa simba
Ndugu tusimuhukumu kocha kwa sasa kwa sababu mpaka sasa tumesikia habari ya upande mmoja. Tusubiri upande wa kocha naye apewe nafasi ajibu hizi tuhuma kwani ni nzito sana na zinaathiri soka la wanawake kiasi naona itakuwa vigumu kwa baadhi ya wazazi kuwaruhusu mabinti zao kucheza huu mchezo ukizingatia kuwa sasa hivi huu mchezo umeanza kuchezwa ngazi ya chini kabisa katika shule za msingi.

Pia kuna kila sababu ya uongozi wa Simba nao kujibu tuhuma zao juu la suala la uchawi. Na kama ni uongo huyo mchezaji ashtakiwe kwani anaharibu "brand" ya Simba ukizingatia kuwa "Youtube" inaangaliwa na kusikilizwa na mamilioni ya watu duniani. Kitendo cha Simba kuacha hizi tuhuma zipite kimya kimya maana yake huyo mchezaji wa Kenya anasema ukweli.
 
Kubadili kocha muda mfupi kabla ya kwenda mashindano yaliyofanyika Kenya imechangia timu kutolewa katika hatua hii.

Vile vile,tathimini ifanyike ya uwezo wa mbinu ya kumkabili adui na kumiliki,kutengeneza nafasi,kupasiana kama timu ilikuwa sawa.Maana timu ya "Commecial Bank of Ethiopia" wapo vizuri,nahisi ndio maana waliweza kumkabili "Vihiga Queen"(Timu mwenyeji).
Mbona timu yetu ikifika mbele ilikuwa inakosa umakini na utulivu.
 
Back
Top Bottom