Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Duniani kote hao makamanda wana misafara kama kero ikizidi unaweza kubadili barabara tu
Acha uongo ,watanzania kitu kidogo chenye ukweli unataka kutuaminisha hapa,wote tumetembea dunia hii na hakuna kitu unachotaka kutuaminisha,personal nimeshawahi kuwa msafara mmoja na president wa Botswana (alikuwa anaendesha pikipiki yake)kwenye foleni na hakuna mwenye wasiwasi na alikuwa anafuata sharia za usalama barabarani kama watumiaji wengine ikiwa ni pamoja na kusimama kwenye stop sign.watanzania tumeshafikishwa mahali pa kuogopa vivuli vyetu!!
 
Hicho ni kiwanda vumilia tu.ametoka kubangua korosho kwa meno.
tapatalk_jpeg_1550950906922.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio kero kwanini usiamke usiku muda huo ukukute umefika unakokwenda.
Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...:mad: au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
askari/mjeshi siku zote anatakiwa awe role mode kwa kufanya vitu ambavyo vinawavutia raia. Kuhusu polisi kuwachukulia hatua wajeshi hiyo haipo na haitakuja itokee na maafisa wa polisi nguvu yao ipo pale pale.

Jeshi na polisi ni organs mbili muhimu sana na zinazoheshimiana kikazi.

Over!!!

5/5
Askari huo ujasiri wa kutii sheria mnaupata wapi huku kila siku mnatenda yasiyofaa kwa maelezo kutoka juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipeni
Majina yake mayatu
Cheo chake
Anakofanyia kazi
Umri wake
Kazi yake ili nikam Google vizuri
 
kuna madaraka na cheo... CHIEF OF STAFF ni madaraka cheo chake huyo jamaa ni LIEUTENANT GENERAL mind you hicho cheo anaweza kupewa hata MAJOR GENERAL so sio lazima kiwe ni chapili kutoka jenerali

turudi kwenye shida yako nakumbuka mwaka 2017 nilikuwa mtumiaji mkubwa wa hiyo barabara mida ya jioni shughuli ilikuwa ni hiyohyo kwa former tpdf chief of staff LIEUTENANT GENERAL JAMES MWAKIBOLWA akastaafu nikajua shughuli itaisha

ila huyu mpya tena kaja LIEUTENANT GENERAL YAKUBU HASSAN MOHAMEDI pia shughuli ni hyohyo so usitegemee kama hii shida itaisha

hata upige kelele vipi shida yako haitaisha labda tu jamaa ahame kule kambini anapokaa ila asipohama na ninahisi kwa protakali za jeshi lazma akae kule...

nakuomba ubadilishe njia au ww uwe unawahi kabla yeye hajaanza kwenda kazini

Sent using Jamii Forums mobile app

Maboresho kidogo.Kwa miakayote huko nyuma ilikuwa mara zote madaraka ya Chief of staff ilikuwa hayatenganishwi ni cheo cha pili chini ya Jenerari. Maana yake kulikuwa na Leteni General mmoja na Generali mmojatu in service at all times. Kwa mara ya kwanza ilitokea wakati Kisamba alipoteuliwa kuwa kiongozi wa peace keeping Darfur kukawa naLt. Gen wawili lakini huyo mmoja alikuwa stationed Darfur. Alipomaliza muda wake mara moja akahamishiwa ubalozi nje ya nchi.

Kwahiyo kwa mara ya kwanza wapo wawiliin service an in country kwa maana mkuu wa National Defence Collage naye ni Lt.Gen. Kimsingi nakubaliana na wewe kuhusu cheo na madaraka maana huyo wa NDC hana msafara. Na hata kwenye profession unaweza kukuta mwenye cheo kidogo ana mamlaka na hivyo maamuzi kuliko mkubwa. Kwenye hali hiyo huwa wanatumia first officer na second officer.
 
asante sana mkuu...kuna kitu nimeongeza kupitia maelezo haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom