Huyu Kamanda marehemu alikuwa mtu wa ajabu sana yaani yeye kama msimamizi wa sheria lkn kazivunja... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu Kamanda marehemu alikuwa mtu wa ajabu sana yaani yeye kama msimamizi wa sheria lkn kazivunja...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mboko, Oct 15, 2012.

 1. M

  Mboko JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hata hivyo, kifo cha Barlow kimetokea siku moja tu baada ya kutoa kauli ya kutatanisha juu ya tukio la polisi kummiminia risasi Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Mwanza, Albert Buchafwe, kwamba aliingia katika mtego wao na kwamba ilikuwa auawe kwa kupigwa risasi.

  Akizungumza na NIPASHE alhamisi iliyopita Barlow alisema kuwa:" Ni kweli kuna tukio kama hilo, lakini yalikuwa ni mashambulizi ya gizani kwa sababu askari walimfananisha ofisa uhamiaji na jamabzi waliyekuwa wamemuwekea mtego, nadhani ana bahati kwanindiyo akwaida yetu hutubembelezani na majambazi."

  Pamoja na kauli hiyo kamanda huyo hakueleza kwa jinsi gani ofisa huyo haliingia katika mtego huo kwani hakuwa katika tukio la uporaji.
  Hahahahaha kuna wimbo wa Twanga pepete waliimba ''iyoyo iyoyoyo mchimba kisima kaingia mwenyewe nambari one mchimba kisimaa kaingia mwenyewe.............yu wapi sasa.Ukiuwa kwa upanga utauliwa kwa upanga na si kwa Jembe
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  imenibidi nicheke tu!!!
   
 3. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mmmm kwani huko mbinguni hamna vikosi vya kuongozwa
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Marehemu amekufa na janaba lake
   
 5. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nadhani maadili bado ni tatizo hapa janvini. Mtu huyu amekwisha tangulia mbele ya haki, hukumu yake ni yeye na Mungu wake sasa tunapokaa hapa na kujadili tena kwa kejeri as if hatutakufa ama tunajua vifo vyetu vitakuwaje hii inanishangaza sana.

  Tunayoyajadili hapa kwa uficho, tukifunuliwa sasa tuyaseme wazi hakuna atakayethubutu kunyanyua mdomo wake. Jamani tuweni na ustaarabu wakati mwingine katika kudiscuss issues zenye sura ya uzuni/misiba.Familia yake,ndugu zake,marafiki zake na jamaa wanaposoma humu hivi wanajisikiaje katika kipindi hiki cha majonzi?. Tuache kuhukumu watu tena wafu!
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Alikuwa anajitabiria kifo chake mwenyewe.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Lohh, hili nalo neno.
   
 8. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Wangekula kiboga kwanza kabla ya kumtupia vitu vizito........wakome kutoa majibu mepesi ktk matatizo makubwa,
   
 9. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mwana JF makini usipoteze muda wako hapa.
   
 10. S

  Sunga Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  na wewe unajua utu kama unajua utu lile la ulimboka na mwangosi we uliishauri nin serikali kama si kiherehere. chamsingi kaa kula chamsibani na uludi kwako utakua umefanya jambo la maana sana kwa kubana bajeti vinginevyo itakukusti.
   
 11. n

  ndokoso Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  kamanda alitakiwa awe kioo cha jamii,na hiyo yote nikutokemea kwa sasa ya msiba ,kemeo lazima liwepo ikiwa na mifano hai kama hii,hujui kuficha uozo kama huu tunaeleka wapi.nyie ndio msiwaeleza watoto wenu ukweli kisa aibu au kifo! Shame on you!
   
 12. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,695
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Acha nidhamu ya uoga, we are discussing seriously.
   
 13. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu,kwa hiyo we ndio mtoa hukumu na haki kwa wanadamu? na ww una uhakika gani kwamba Mungu uliyomtendea kama binadamu kayakubali? acha utoto! mtu kafa ni mtu regardless mapungufu ambayo ww huna yakini nayo,usifurahie kifo kwa mwanadamu yoyote kwani hujui siku, muda wala saa!
   
 14. B

  B.Panther Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi ningeomba kuuliza.Hayo Majinizano alikuwa yanahusu nini?,maana hao wauwaji kuna kitu walikuwa wana mmind kamanda na sio kumuibia,Kamanda alipotoa radio ndo kukawaka.
  TATIZO KUBWA POLISI WETU WAMESAHAU MAJUKUMU YAO.WAO KAWA ASILIMIA KUBWA NDIO MAJAJI,SASA KAMA KUNA INSHU ALIISHILIA KIDEDEA,HICHO NDO KISASI CHAKE...
  Alafu,Polisi jifunzeni MAMBO YA MITANDAO YA KIJAMI,Mtaelimishwa huku na muachane na kuendesha mambo kizamani,Mtakufa mtaisha,Shauri yenu...
   
 15. S

  Sir M.D.Andrew JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wamekuwa waaminifu kwa ccm,wanapiga,kujeruhi na kuua..leo kamanda liberatus kauawa halafu mwenyekiti wa chama chao kaondoka kwenda oman kupanda farasi,hata msiba hana habari nao,ndo wajue wanatetea chama cha wasio na huruma...akufaaye kwa dhiki ni rafiki wa kweli
   
 16. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kuna tatizo kubwa hapa zaidi ya ninavyofikiri.Natambua matumizi ya lugha iliyopo hapa janvini ila bado nabaki na msimamo wangu kuwa si uungwana katika dunia ya ustaarabu ''kutoa lugha ya kejeri kwa wafu'' hii ni ishara ya kukata tamaa.

  Tuwe waungwana, hakuna anayependa kufa na kama ikitokea basi ni mipango ya Mungu.Tunapo kaa hapa na kutumia lugha ya kuuzi eti kisa tu tumejificha nyuma ya key board basi tujue tuna kazi kubwa mbeleni. Wewe unaetaja msiba wa Mwangosi, umeisha changia nini familia yake?ama ni maneno matupu tena kwa mtu ambaye ahusiki na kifo chake.Hizi siasa za visasi zitaaribu familia zetu na kizazi kijacho.

  Nashukuru kwa walionitusi kwani sasa ninaamani na kuamini kuwa ''sikio la kufa halisikii dawa''.Nimetambua pia ni watu wa aina gani wanapatikana hapa jamvini. Usiku mwema Wakubwa na Siungi hoja mkono.
   
 17. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Baada ya kifo hukumu.
   
 18. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  You are not serious yet!Unless hujawahi kufiwa.Je! unajua kifo chako kitakuwaje? Kila mtu huwa na pungufu yake na pengine dhambi zako ulizotenda mpaka sasa ni zaidi ya huyu aliyefariki.Tusiweke itikadi za kisiasa kwenye issue nzito kama hizi tena za kusikia kila mtu na lake!
   
 19. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  he went home to live in the house of god. Amen
   
 20. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Hivi ubwabwa wake ni wapi tujulishane wakuu...
   
Loading...