Huyu JK vipi???

Mlalahoi

JF-Expert Member
Aug 31, 2006
2,182
883
JK awaonya viongozi walafi

03 Dec 2007
By Maura Mwingira, Kibaha

Rais Jakaya Kikwete, amewatahadharisha viongozi wanaojigawia miradi ya wananchi maskini kuwa wasipoacha tabia hiyo atawataja hadharani.

``Naomba tuelewane kabisa Mkigawana miradi ya maendeleo ambayo imelengwa kuinua maisha ya wananchi maskini na kuwapatia kipato, mtakiona cha mtemakuni nitawasema hadharani mbele ya wananchi,`` alisisitiza.

Alitoa tahadhari hiyo jana baada ya kuelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Christine Ishengoma kuhusu mradi wa ugawaji wa miche ya miembe inayozaa kwa muda mfupi kwa wakulima maskini katika wilaya za mkoa humo.
Habari zaidi endelea hapa

"Vitisho vya kitoto" vya aina hii ungeweza kuvitarajia kutoka kwa kiranja wa darasa kule shule ya msingi,kwamba "atakayeendelea kupiga kelele nitamwandika,au kumtaja kwa mwalimu..." lakini sio kwa kiongozi wa nchi tuliyempa wadhifa wa urais.Kwahiyo akishatutajia hadharani kifuatie nini?Tuawazomee?Tuwapige mawe?Au TAKUKURU ndio waamke usingizini kuwachunguza?Hivi huyu mtu hana mtu anayemsaidia kuandaa hotuba zake?Anyway,pengine atakapoamua kutaja hao wanaogawana miradi atatutajia pia na wala rushwa alodai anawafahamu lakini anawapa muda wa kujirekebisha.Kaaazi kwelikweli
 
Jamani mbona mnakuwa wagumu kumzoea rais wenu?? mpaka sasa ametoa kauli kali nyingi tuu

1. nawajua wauza madawa ya kulevya, nina majina yao nawapa muda na nitawakomesha

2. Nitahakikisha kuwaletea maisha bora kwa kila mtanzania.

3.Viongozi wenye mali kuliko uwezo wao watakiona cha mtema kuni

4. nawajua wala rushwa wote wa nchi huku akikiri utajiri wa wawatanzania upo mikononi mwa watu wachache sana.

ohh and the list of this "matamko makali" will go on and on ila sasa utekelezaji wake ndio tatizo.
Nahisi ana syndrome ya kutamka wakati hamaanishi. Na vyombo vyetu vya habari navyo vina syndrome ya kuwa kama magnifying glass. Mf rais akisema kuwa nasikitishwa na baadhi ya wala rushwa , kesho magazeti yataandika RAIS AKASIRIKA SAAAAANA NA TABIA YA RUSHWA.

jamani mzoeeni kwake ni rahisi kusema when he doesnt mean it.

sasa leo watakaofuja hela za maendeleo wataona cha mtema kuni. LOL heri nicheke ie coz walao pia wanajua hilo ni kama tamko tu utekelezaji wake ni mgumu kwa kuwa mtmkaji amezoea kukemea bila action.
Please Mr. president start living up to yor words.
 
Somebody please.. hang me!!

MNKJJ

Mbona una haraka huyu Rais hata hajamaliza ngwe yake ya kwanza...usitafute wa kukunyonga leo...subiri hadi 2014 pengine utakuwa na sababu nyingine nzuri nzito zaidi, hii bado ni ndogo sana. I mean hata bado hajasajili kampuni yake na mkewe akiwa Ikulu..

why don't u hang ur self?

Watanzania tunatakiwa kufanya sala/dua kwa bidii zaidi...huyu Rais wetu wa sasa anafanya vituko ambavyo havionyeshi dalili njema kabisaaa huko tuendako. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba Watanzania walio wengi hawajui cha kufanya...bila baraka za ziada kutoka kwa Muumba ulimwengu huu na ikiwa ni pamoja na nchi yetu nzuri itakuwa kaazziiii kweli kweli.

JKN alisema kutuasa kazi ya urais si lelemama..watanzania tuchague mtu safi na mwenye busara; waTz tukamuoma mzee ameshazeeka hajui asemalo.
 
Kama kawaida yake mkwere,kutoa mikwara tuu hadi miaka mitano itaisha akafanye biashara na yeye. Ah, Tanzania!! ndio yamekufika hayo!
 
Habari zaidi endelea hapa

"Vitisho vya kitoto" vya aina hii ungeweza kuvitarajia kutoka kwa kiranja wa darasa kule shule ya msingi,kwamba "atakayeendelea kupiga kelele nitamwandika,au kumtaja kwa mwalimu..." lakini sio kwa kiongozi wa nchi tuliyempa wadhifa wa urais.Kwahiyo akishatutajia hadharani kifuatie nini?Tuawazomee?Tuwapige mawe?Au TAKUKURU ndio waamke usingizini kuwachunguza?Hivi huyu mtu hana mtu anayemsaidia kuandaa hotuba zake?Anyway,pengine atakapoamua kutaja hao wanaogawana miradi atatutajia pia na wala rushwa alodai anawafahamu lakini anawapa muda wa kujirekebisha.Kaaazi kwelikweli

Rais anatishia watu wazima Nyau...
 
Kwa kweli umeniwahi maana tangu niliposikia habarihiyo kwenye kipindi cha kutoka magazetini leo cha RTD nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa na kukumbuka kauli zake za nyuma kuhusu kuwapa muda Wala rushwa na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya (ambao majina yao yako ofisini kwake).

Swali la kujiuliza hivi Mhe. Rais anaridhika na MAfisadi hao? Mbona haja-specify huo muda ili tujue kuwa tutaendelea kuumizwa kwa miezi/miaka mingapi kabla Rais hajachukua hatua? Heri ya Mrema wa awamu ya pili!
 
Habari zaidi endelea hapa

"Vitisho vya kitoto" vya aina hii ungeweza kuvitarajia kutoka kwa kiranja wa darasa kule shule ya msingi,kwamba "atakayeendelea kupiga kelele nitamwandika,au kumtaja kwa mwalimu..." lakini sio kwa kiongozi wa nchi tuliyempa wadhifa wa urais.Kwahiyo akishatutajia hadharani kifuatie nini?Tuawazomee?Tuwapige mawe?Au TAKUKURU ndio waamke usingizini kuwachunguza?Hivi huyu mtu hana mtu anayemsaidia kuandaa hotuba zake?Anyway,pengine atakapoamua kutaja hao wanaogawana miradi atatutajia pia na wala rushwa alodai anawafahamu lakini anawapa muda wa kujirekebisha.Kaaazi kwelikweli

Oh!!! God help us this country has no President.
Very similar kwa mtoto anapocheza na mwenzake kisha huyu mtukutu akamchapa mwenzie halafu huyu innocent anasema nakuja kukusemea kwa mama. Hapa kuna mawili huyu mtukutu anaweza kumpa token fulani ili huyu asije kusemea kwa mama. Pili anaweza akaendeleza ubabe wake ili liwalo liwe.

Jambo la pili limeniingia kama hadithi fupi kwamba ni sawa na familia moja ilivamiwa na vibaka, familia nzima ikapata mkong'oto wa nguvu kibaya zaidi vibaka wale walianzia kwa Baba mzazi. Watoto baada ya kuona Baba kapigwa wakapoteza matumaini ya usalama wakaanza kulia. Mwisho Baba alilia akasema kwa nini mnanichapa mimi nawasemea kwa watoto wangu.
 
Mbona sioni constructive criticism hapa? labda mkuu wa kaya katoa kauli hiyo kulingana na upeo wake (pamoja na timu yake)wa kufikiri. Tumsaidieni jamani ili next time ajue nini kinapaswa kusemwa aki encounter similar situation.
 
Huyu jamaa anatudanganya tu naye yumo ila hapo nnachokiona anawaambia wenzake wajifiche wasitambulike kirahisi. Naye inaelekea yumo. Kwanza atutajie mafisadi wa Benki Kuu.
 
Mbona sioni constructive criticism hapa? labda mkuu wa kaya katoa kauli hiyo kulingana na upeo wake (pamoja na timu yake)wa kufikiri. Tumsaidieni jamani ili next time ajue nini kinapaswa kusemwa aki encounter similar situation.

Cha kumsaidia ni kumuondoa madarakani mnamo 2010. Yaani jamaa ni mpayukaji ile mbaya! Yaani bado anapiga kampeni hadi leo wakati kashinda uchaguzi? Hivi huwa hafikiri anapotoa hotuba? Na naona kuna upungufu mwingi sna kwa wasaidizi wake. Kauli za ajabu za raisi wetu huwa zinanizcha hoi sana.
 
Jamani mbona mnakuwa wagumu kumzoea rais wenu?? mpaka sasa ametoa kauli kali nyingi tuu

1. nawajua wauza madawa ya kulevya, nina majina yao nawapa muda na nitawakomesha

2. Nitahakikisha kuwaletea maisha bora kwa kila mtanzania.

3.Viongozi wenye mali kuliko uwezo wao watakiona cha mtema kuni

4. nawajua wala rushwa wote wa nchi huku akikiri utajiri wa wawatanzania upo mikononi mwa watu wachache sana.

ohh and the list of this "matamko makali" will go on and on ila sasa utekelezaji wake ndio tatizo.
Nahisi ana syndrome ya kutamka wakati hamaanishi. Na vyombo vyetu vya habari navyo vina syndrome ya kuwa kama magnifying glass. Mf rais akisema kuwa nasikitishwa na baadhi ya wala rushwa , kesho magazeti yataandika RAIS AKASIRIKA SAAAAANA NA TABIA YA RUSHWA.

jamani mzoeeni kwake ni rahisi kusema when he doesnt mean it.

sasa leo watakaofuja hela za maendeleo wataona cha mtema kuni. LOL heri nicheke ie coz walao pia wanajua hilo ni kama tamko tu utekelezaji wake ni mgumu kwa kuwa mtmkaji amezoea kukemea bila action.
Please Mr. president start living up to yor words.

Kinyau, ongezea na hizi!

5. "Tanzania tunasaini mikataba mibovu kwa sababu hatuna wataalamu wabobevu wa sekta ya madini". (Swali kwa Rais: Nyerere na STAMICO yake waliwatoa wapi wataalamu?)
6. "Sijui umasikini wa Watanzania unatokana na nini" (Swali kwa Raisi: Uliomba uraisi ili ufanye nini? Sasa uko madarakani kufanya nini? Biashara? Utalii?
 
Yaani anatoa bit kali kisa ni miti ya miembe??????
Kuna genuine issues nyingi sio tuu za kutoa bit but kuwaadabisha baadhi ya watu lakini sio za miembe
 
Mimi ningempa heshima nyingi tu Rais wetu, hata kama angeanzia hapo pa kuwataja viongozi wanaowaibia wananchi miche ya miembe; kwani hii ingekuwa dalili tosha tu kwamba kazi sasa imeanza; na kwamba hao wenye migodi na mafisadi wakae chonjo!
 
Jamani mi nimeamua kwamba nikikasirika na kuchukia nitawehuka! Sasa nimeamua kucheka kwanza, nakusanya data alafu .... itabidi niifanyie kazi. Yaani tulikuwa tunawacheka wamarekani kwamba wamepata Bozo Bush, lakini sisi ... ni hasara tupu! Hebu endeleeni kushusha utirio, naomba Moderator iunganishwe na Kikweteism thread ya Mzee Mwankijiji ili nipate zile gaffes zoooote!
Wakudata: Huyu rais hawezi kufanya training on the job! Wala hakuna cha kumshauri! Awapishe wengine 2010. Chadema MPO?
Good job Jambo forum!:)
 
Kuweni wavumilivu watanzania, Rais wenu hana experience kwenye post yake ya sasa, hajawahi kuwa Rais before kwahiyo on job training haiwezi kukwepeka hapa!
 
Mbona sioni constructive criticism hapa? labda mkuu wa kaya katoa kauli hiyo kulingana na upeo wake (pamoja na timu yake)wa kufikiri. Tumsaidieni jamani ili next time ajue nini kinapaswa kusemwa aki encounter similar situation.

Hii inareflect upeo wetu sisi watanzania.Hatuwezi kuwa na upeo na akili nzuri tukachagua mtu wa namna hii!!Haijawahi tokea watu wenye macho yanayoona wakamchagua kipofu kuwaongoza,bali vipofu wenye uwezo duni wa kujua njia ndo huchagua kipofu mwenzao mwenye uwezo ili kuwaongoza au mtu mwenye macho na anayeona ili kuwaongoza.

Sisi watanzania naamini wengi wetu ni wajinga ila hatutaki kukubali ukweli huu.Sikubaliani na kumpa lawama zote JK.Sisi wapiga kura tubebe sehemu kubwa ya lawama hizi kwa kuwa na uwezo mdogo wa kuainisha pumba na mchele.Kwani tunaonyesha tunachojali ni ushindi nasi uwezo wa mtu katika kuwajibika kwa uadilifu.
Na bado haya ni manyunyu tu bado masika.
 
Tanzania bado tuna kazi ambayo ni ngumu sana hatuna kiongozi. We angalia nchi yenye vijana wadogo pamoja na matatizo lukuki unakuta Rais Kabila anaweza kufanya decission hata kuliko Kikwete aliyechaguliwa na wananchi kwa 80%.

Huu ni utani. ni Shame kwa watanzania, mtu aliyepewa madaraka na wananchi anarudi kuwaambia kuwa fulani amemshinda ni FISADI. Anataka wananchi wamsaidie nini? Wajichukulie sheria mikononi au? Jk anajua kila aina ya ufisadi unaofanyika nchini lakini anaunyamazia. Mimi nafikiria kuna faida anayoipata akiwaambia nawafahamu bila kuchukua hatua hujue wanakwenda kumuona mzee.

Anatishia hili wamuone.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom