Huyu Jay Moe wa 'Pesa Madafu' mbona watu wanam-diss sana?

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Toka Jay Moe arejee na ngoma yake ya Pesa ya madafu kumekuwa na upinzani mkubwa sana toka kwa mashabiki wa hiphop.

Wengi wanasema anafanya muziki wa kibishoo ambao sio hiphop orijino.

Ni kweli kafanya trap ila trap pia ni hiphop.

Wengine wanasema kwenye video ame dab.. Which mimi sioni kama ni tatizo kulingana na soko. Hip hop ina element ya kubreki densi.

Sielewi mashabiki wa hiphop nchi hii kwa nini ni watu wa kukalili sana.

Wao wamekalili midundo ya East coast ndio midundo ya hiphop sijui kwa sababu ndio hiphop iliyofanikiwa kupenya zaidi ulimwengu wetu wa tatu ama vipi.

Jay Moe huyu ni wa moto sana mnaomdiss hamjui vizuri muziki wa hiphop.
 
hao ni wadwanzi tu, mi huwa nasikiliza utunzi, na moo kapangilia vyema uandishi wake na hata idea yake ni nzuri. bg up Mo
 
Hebu taja wanaomdisi ili tuone chake yeye kipo kwenye kiwango gani ?
 
Moo anaiwakilisha hip hop vema sema watu wamebaki na mazoea ya mi bishoo bila kuitafsri hip hop kiundan
 
Juma yuko vizuri sana...kwanza binafsi nimefurahi kumsikia tena....Jay Moe ni HipHop. HipHop ya kitambo katika game haiwezi kuwa sawa na ya sasa hivi kuanzia beats mpaka michano. sijaona tatizo kabisa.

Kuna wasanii wakubwa lakini mpaka leo bado wana flow kizamani....lakini sio kwa Mchops.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom