Huyu Jamaa Naona Alichokuwa akikiimba kimetimia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu Jamaa Naona Alichokuwa akikiimba kimetimia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kasimba123, Mar 19, 2011.

 1. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Hakika ninaposikiliza nyimbo hizi mbili

  YouTube - Ndio mzee Professor jay ft Juma nature

  Kikao Cha Dharura-Prof J

  na habari hii niliyosoma kwenye gazeti la Nipashe naona yanatimia yaliyosemwa na professor J. hakika nyimbo hizi mbili ni kweli tupu.

  habari yenyewe niliyosoma ni hii hapa
  Mkulo: Kila Mtanzania atakula kwa jasho lake

  19th March 2011
  [​IMG] Asema hali ngumu hakuna wa kulaumiwa
  [​IMG] Aeleza kuwa kodi za mafuta hazitapunguzwa
  [​IMG] Barabara zilizotengewa fedha zatelekezwa

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Serikali imesema haina uwezo wa kumaliza makali ya maisha yanayowakabili Watanzania na kumtaka kila mtu ale kwa jasho lake mwenyewe kama maandiko ya Mungu yanavyosema.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kadhalika, serikali imesema haina mpango wa kupunguza kodi katika mafuta ili kusaidia kushusha bei ya bidhaa hiyo inayozidi kupanda siku hadi siku.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Msimamo huo wa serikali ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kwa waandishi wa habari baada ya waandishi wa habari kumtaka atoe kauli ya serikali kuhusiana na malalamiko ya wananchi kuhusu kasi ya kupanda kwa gharama za maisha nchini.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Maandiko yanasema kila mtu atakula kwa jasho lake na apigae hodi atafunguliwa, hivyo wananchi wasitegemee unafuu wa maisha utaletwa na serikali,” alisema Waziri Mkulo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkulo alisema hakuna mtu yeyote nchini aliyesababisha kupanda kwa gharama za maisha, bali hali hiyo imetokana na matatizo ya ulimwengu mzima.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata nchi tajiri duniani bado kuna watu maskini wa kutupa ambao wanakaa mitaani kwa ajili ya kuomba omba hivyo sio Tanzania pekee ambayo watu wake wanakabiliwa na tatizo la ugumu wa maisha,” alisema Waziri Mkulo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Waziri Mkulo akizungumzia mlalamiko kuwa kuna kasi kubwa ya mfumuko wa bei nchini, alisema kuwa serikali inafanya kila jitihada ili kuhakikisha mfumuko wa bei hauongezeki zaidi ya asilimia 7.5 ifikapo Juni mwaka huu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hivi sasa kiwango cha mfumuko wa bei nchini ni zaidi ya asilimia sita.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Pamoja na kutokueleza hatua ambazo serikali itazichukua kudhibiti mfumuko wa bei, lakini Waziri Mkulo alieleza hatua ya muda mrefu ambayo alisema ni kuwekeza katika sekta ya kilimo na kwamba chakula kikipatikana kwa wingi, hakuna uwezekano wa kuwepo kasi ya mfumuko wa bei.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alijisifu kuwa Tanzania inafanya vizuri katika kudhibiti mfumuko wa bei ikilinganishwa na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Waziri Mkulo alisema kiwango cha mfumuko wa bei katika nchi nyingi za Afrika Mashariki ni zaidi ya asilimia 10.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika hatua nyingine, Waziri Mkulo alisema serikali haina mpango wa kupunguza kodi katika mafuta kwa ajili ya kupunguza makali ya maisha.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]BARABARA ZATELEKEZWA[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huohuo, imeelezwa kuwa serikali imetelekeza miradi mingi ya barabara ambayo ilitengewa fedha kwenye bajeti iliyopitishwa na Bunge mwaka jana bila ya kutoa maelezo yoyote kwa wabunge.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge wa Bariadi (Magharibi), Andrew Chenge, alimuomba Mkulo kumpa sababu kwa nini miradi hiyo inashindwa kutekelezwa licha ya kuwa fedha zake zilikwisha kutengwa.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Mimi naomba ufafanuzi wa Waziri Mkulo ni kwa nini miradi ambayo Bunge lilipitisha fedha zake imeshindwa kutekelezwa kwa wakati,” alisema Chenge katika semina ya wabunge iliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Waziri Mkulo juzi na jana alihudhuria semina hiyo na kuelezea vipaumbele vya serikali katika bajeti ijayo ya mwaka 2011/12.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akijibu swali la Chenge, Waziri Mkulo alisema sababu iliyochangia miradi hiyo kushindwa kutekelezwa kwa wakati ni kutokana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuingia mikataba ya ujenzi wakati hawana fedha.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kutokana na hali hiyo, serikali ilijikuta ikiwa na miradi mingi kuliko ile iliyoombewa fedha na hivyo kushindwa kuitekeleza kwa wakati kama ilivyotarajiwa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Mkulo aliitakaTanroads kuacha kuingia mikataba ya ujenzi wa barabara kwa kutegemea fedha za bajeti ya serikali inayopitishwa kila mwaka kwa kuwa hali hiyo itazidi kuleta mkanganyiko wa kiutendaji ndani ya serikali.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
   
 2. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hayo ndo waliyoyataka watanzania na wala wasilalamike. Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana walielezwa kuwa CCM siyo chama cha kuwatoa kwenye umasikini kama siyo kuwaongezea umasikini lakini wengi waliziba masikio na kujidai vipofu wakaendelea kushabikia JK na CCM yake. Hata nusu mwaka haujapita tokea waichague CCM yao, wakubaliane na ukweli waliokuwa wanaambiwa na Dr. Slaa. Najuta kuwa chini ya utawala wa CCM kwenye karne hii ya 21. Hivi watanzania hamkujua kuwa CCM ilivaa ngozi ya kondoo wakati wa uchaguzi kuwadanganya kuwa yenyewe siyo mbwa mwitu? Haya sasa kaeni tayari kugeuzwa vitoweo vya mbwa mwitu mliyedhani kuwa ni kondoo.
   
 3. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Hakika watu waliacha kusikiliza ukweli wakaenda kwenye uongo. ama kweli CCM inawasanii Jamaa alikaa chini kwenye vumbi na mipicha kibao lakini alipozindua aina fulana ya mbolea alitandikiwa mkeka kupanda mti

  Wakati Slaa aliposema kuichagua CCM nikuchagua maafa nakumbuka mjomba kada wa CCM kijijini kwetu alikuwa akiponda kwasababu ya UCCM wake Leo ananipigia simu nimsaidie maisha magumu ilibidi nimpe ukweli tu kuwa aliwapigia kampeni mwenyewe hivyo hata mimi maisha magumu na kipindi kingine atie akili kwa kichwa na sio kufikiria sukari na Ubwabwa wa kuondoa njaa ya siku moja

  Wakati natafakari hilo la simu yake ndipo nikasoma hilo gazeti na nikakumbuka huu wimbo

  Ndugu zangu tulio na upeo hebu tujitahidi kuwaelimisha wenzetu kule vijijini kwani 2015 sio mbali

  Kumbuka mabadiliko yanaanza na wewe
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hizi ni sababu tosha za kuwashikisha adabu hawa. Hawezi sema hayo kama hayana baraka toka ngazi za juu
   
 5. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni ushabiki wa vyama.
  Watu wako tayari kufanya lolote liwalo bila kufikiria matokeo ya baadaye ilimradi kile wanachokishabikia kionekane ndicho kinacho ibuka na ushindi kama ilivyo katika ushabiki wa michezo.
  Matatizo yanayo wapata watanzania wa hali za chini yanasababishwa na wale walio na hali nzuri kiuwezo, na pia kukosekana kwa dhamira ya dhati ya viongozi walioko madarakani kuondoa matatizo yaliyopo.
  Sasa mambo yanaanza kuwa tofauti watu wanaanza kutambua hali njema inawezekana kwa mfumo uliopo kubadilishwa, na si kwa kudanganywa na ahadi pamoja na mafanikio hafifu yaliyopo kama peremende kwa mtoto anayetaka kuambatana na mzazi, na kuahidiwa abaki nyumbani kwa kuahidiwa zawadi hiyo ndogo.
  Viongozi walioko madarakani wapo kulinda masilahi yao na familia zao tu, si jamii ya walala hoi walio wengi hapa Tanzania.
   
 6. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  TUMEKWSHA,...MAIT ZETU HATA KUNGURU HAWATOZTAKA. Kifo che2 tumeksababsha wenyewe. Na hii ndo faida ya kukumbatia nyuki..2ljua madhara yake ila kutokana na fkra mgando tukashndwa kubadlka..tuldanganywa tukchagua chama kngne vta itatokea ila tulshndwa kufkria iweje alieshnda alete vta? Na ni vta gan mbaya zaid ya hii ya maisha magumu yasiyonama2main tunayopgana? Vta ya mama wajawazto wanaofia hosptal na vchanga 2mbon. Hii ni ngumu kulko kumkwepa mwenye m22 wake.
  WATANZANIA TUAMKE, BADO HATUJACHELEWA. SILAHA YETU KUBWA NI "KURA" YETU
   
Loading...