Hushpuppi kabambikiwa kesi kwa sababu ya ushamba pamoja na Mwafrika kuchukiwa akiwa na maisha ya juu

Mkuu tupe maujanja
Jamaa alikuwa atandiki code,yeye alikuwa ananunua scripts za Python toka Hungary na Pakistan huko anawanyoosha wazungu,why usumbuke mkuu?? Nunua scripts uingie mzigoni fasta.Coding itakuchukuwa zaidi ya 5 yrs Kuwa master
 
duh umechelewa kuipata hii habari.
Mkuu hii habari nimechukua CNN Jana unless Niko outdated
Screenshot_2020-07-13-14-59-12-776_com.cnn.mobile.android.phone.jpeg
 
Ulimbukeni tabu sana.

Kuna watu wamepiga zaidi, hawajulikani, wanakula kwa ubua.

All in all, crime does not pay.

Yani kwangu ni bora kuwa na hela ya halali ambayo inakufanya unaishi kwa raha bila magutu.

Ukishaibia watu hela hata maisha yako yanakuwa ya magutu magutu muda wote.
 
Kweli kabisa.
 
I second you mkuu Ila I know alot of cats walio-come into fortune kwa magumashi but still live lavish life

Nilikuwa simfahamu jamaa ila ndio nimemjua baada ya kuangalia page yake ya instagram.Kiufupi mimi namuona jamaa kama hustler na mpambanaji haswa naweza kumfananisha na James St Patric 'Ghost' kwenye series ya power sema kosa la jamaa ni ulimbukeni na hana ujuzi wa kutakatisha fedha.

Angepiga hizo pesa kimya kimya bila showoffs au angewekeza hata kwenye mipango ya baadae huko au awekeze kwenye gang itakayomlinda just incase akikamatwa kama hivi.Mwisho wa siku jamaa amefaidi sana akitoka jela inatakiwa arudi kitaa kwa hasira zaidi maana kutoka umilionea mpaka ubukuonea sio mchezo!
 
Mapacha walikuwa kati ya rapper ambao nawakubali sana ngoma zao, kuanzia ujumbe au style ya kughani.
Pamoja sana...

Hata mimi pia walikuwa na jumbe nzuri.

Style ya kughani ndio nailewaa vibaya mno...

Ngoma Vita ya Benghazi alioimba na Nikki Mbishi humo kaua sana...K wa Mapacha.

"Macho Kama bundi, Kama Askari Wakikrudi"

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Habari wana Jukwaa?

Hii habari ya Bilionea wa Naija bila shaka wengi wetu tunaifahamu baada ya kukamatwa na Dubai Police.

Sasa nasikia huyu Mwamba hakuwa na elimu yoyote ya kutisha katika masuala ya tech hasa cyber tech lakini ameweza kuwatapeli wazungu wenye sayansi yao.

Je, huyu mwamba alitumia mbinu zipi? Tupeane Abc's kwa lengo la kuelimishana.

Lakini pia, kwanini nchi ya Naija na nchi nyingine za West Africa zina matapeli wengi?

Nawasilisha
 
Sema jamaa katuwakilisha vizuri sana,jamaa alikuwa anawatumikisha wazungu kama vijakazi wake,asa hivi mompha anatamba tu
 
yeye alikua n kiongozi wa genge la wahuni () fatilia iyo video uta elewa
 
Kwa level yako sikutegemea uchangie ivi, kuna watu wanaongoza kutapeli kama Hao whites uko? Mana wewe sijui ukisema crime sijui unamaanisha nini mana hata mikataba tu ya nchi zetu na ukoloni vyote ivo ni crime, Ngombe wanazaliwa kila siku

Mkuu, nakuomba chondechonde usiniweke level yoyote, kwa sababu ukiniweka level fulani unaninyima uhuru wangu wa kuwa level yotote.

Mimi nathamini zaidi uhuru wangu wa kujieleza ninavyoona kuliko kuwekwa level fulani na wewe.

Huyu Hushpuppi kafulia.

Kafulia kwa watu wanaohalalisha upigaji, kafulia kwa watu tusiohalalisha upigaji.

Kwanza kabisa, kumtetea kwa " hao whites wanaongoza utapeli" kama unavyosema wewe, ni kukosa uwezo wa kuchambua na kuifanya hii ni ussue ya identity politics. Hawa WaNigeria si some modern day Robin Hood wanaowaibia wazungu tu, hata kama hilo lingekuwa ni right. Hawatapeli whites tu, wanapiga hata kwao, zaidi two wrongs do not make a right.

So, lets get that right.

Zaidi, hata kama ukisema unahalalisha upigaji wewe mvaluvalu hujali dini wala utamaduni wala siasa, unajali kupiga hela tu, sawa.

Lakini, kwa mtu yeyote asiyejua au kuweza kufanya "self preservation" akapiga hela kubwa, akashindwa kujizuia kuwa "under the radar" na "off the grid", akakamatwa, huyo kafulia.

Kwa sababu, kaweza kazi ngumu ya kupiga hela kubwa, halafu kashindwa kazi rahisi ya kuzuia nyege zake za kujionesha machoni pa watu kwamba yeye kapiga hela kubwa.

Hii Kiswahili tunaita "ujanja mwingi, mbele kiza".

Hapo nimemaliza kwa mabaharia valuvalu wasiojali la muazini wala mchota maji msikitini, wao wanajali kupiga pesa tu.

Kwetu sisi tunaojali maadili, tunaoangalia pesa zimepatikanaje, sio kujali pesa tu, tunaojali miiko ya maana ya kijamii, tusiotaka kuiba, tusiotaka kuishi kwa hofu, tunaotaka tuwe na uwezo wa kutamba na mali zetu bila hofu ya kushikwa (hata kama hatufanyi hivyo kwa sababu nyingine za kimaadili na kiusalama), mtu kujiingiza katika maisha ya wizi na utapeli ni kukubali kushindwa maisha. Bila kujali kwamba mtu huyo anakamatwa au hakamatwi.

Mimi naamini kwamba, kama una uwezo wa kutapeli watu dola za kimarekani Milioni 40, kwa akili hiyo hiyo uliyotumia kutapeli nje ya sheria, ukijipanga vizuri, unaweza kutengeneza dola za Kimarekani milioni 400, kisheria, hata kama ni kwa kuwapiga watu kisheria tu.

Kwa hiyo Hushpuppi kafulia kwa sababu kakamatwa, kwa wasiojali maadili wanaojali hela tu.

Kwetu sisi wengine, tunaojali maadili, hata kama asingekamatwa, tungeweza kusema "hizo hela hata matajiri wa Forbes hazihesabiwi, kwa sababu zinajulikana ni hela chafu, hazina heshima".

Vyovyote utakavyoamua kumuangalia Hushpuppi, kishua ama kisela, amefulia.

Suluhu yake sasa hivi ashinde kesi, kitu ambacho Mmarekani hawezi kuruhusu na hata kama ikitokea, reputation yake ishaharibika vibaya sana.
 
I second you mkuu Ila I know alot of cats walio-come into fortune kwa magumashi but still live lavish life
Kuna lavish life, halafu kuna "death wish on Instagram".

Kwa hashuo zile za Hushpuppi hata kama hela ya urithi baba yako Bakhressa, kujianika vile ni kuanika watu waje kuku kidnap kama Mo.

Huyo Mo hajioneshi vile na watu wamemkidnap.

Hawa jamaa wamefanya ulimbukeni kiasi kwamba hata kama hela zao zilikuwa legitimate, kujianika vile ni kujiongezea risk ya vitu kama kuwa kidnapped.

Granted, huko kwao wanaweza kuwa wanajulikana na wana channel zote za wahuni, lakini kimataifa huwezi kushika channel zote.

Kibaya zaidi, maisha ya mazishi, ukishawatapeli watu wengi, wengine wanakufuatilia, wanaweza hata kukuchukulia contract kwa hitman aje akuue.Ushawaibia watu mamilioni ya dola?

Kwa hiyo, ashukuru ameshikwa na mkono wa sheria.

Kuna Wanigeria wawili waliwatapeli ma drug dealers wa Mexico. Wale ma Don wakashtuka wamepigwa. Wakaitumia tamaa ya Wanigeria kuwanasa. Wakamwambia njooni Mexico City tupige deal kubwa zaidi, wakawatajia kidau kikubwa.

Wanigeria wakakubali.

Walichowawafanyia siwezi kusahau.

Unajua unavyochoma nyama mshikaki? Kuna ile spike halafu unaweka nyama unachoma? Wa Mexico walimuweka hivyo hivyo katika spike wakawa wanamchoma nyama polepole.

Story na picha zipo hapa kwenye forum kama JF ya WaNigeria.

https://www.nairaland.com/4862935/nigerian-yahoo-boys-roasted-death
 
Hata mwizi, akiiba akakimbizwa akiona anazidiwa huwa wanakimbilia kituo cha polisi, wakati mwingine vyombo vya Dola huwa msaada mkubwa kwenye baadhi ya situations
 
Huyu jamaa jinsi alivyokuwa Nyoko alimchukua yule mchoma nyama maarufu wa dunia 'Kama ushawahi kuona zaltan Ibrahimovic, cr7 na mastaa wengine wa dunia wakichomewa nyama" jamaa alimtafuta na kufanyiwa manjonjo na jamaa kifupi jamaa aliishi maisha ya Pesa chafu hatari
hahahah huyo si hata benpol alimchomea nyama, hebu toa ujinga wako

Sent from my MI NOTE Pro using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom