Huyu jamaa angu hana hamu na UDSM kwa hiki alichokipata

Kwema wasomi?
Kuna jamaa angu ni in service wa halmashauri moja hapa Tanzania, mwaka 2019 alinifuata kuniomba ushauri wa program na chuo cha kusoma hapa Tanzania, kwa uelewa wangu kiasi niliokua nao kwa kipindi hicho,nikamahauri ni Bora atafute chuo cha private walau huko kunakua na unafuu na angalau hata jiumiza sana ukizingatia ni mtu mzima kiasi(38+),yeye akaona kama namzibia ridhiki coz ndoto zake zilikua kusoma uchumi udsm,kweli akaomba chuo akapata udsm BA ECONOMICS. Mwaka wa kwanza umeenda vizuri kiasi,mwaka wa pili umekua mbaya sana,kwani kapigwa discontinue,so hapa kanitumia matokeo yake ili nijaribu kumshauri nini cha kufanya.anasema anaona hata aibu kumwambia mkewe kuwa kaliwa kichwa huko chuo.
Matokeo yake nitayaweka hapa ili mtoe mawazo yenu wakuu coz mimi binafsi nimemshauri aachane na mambo za kusoma kwa sasa aangalie maisha yake na familia yake tu.

View attachment 1974214
Udsm hakunaga units za 3, ni 8 au 12

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Mbona sasa mmeyapatia maisha? Shule nini bana kha!

Ndugu yangu! Hapa JF si ndio sehem pekee tunajifariji, nnaweza kuwa Tajiri, Msomi, Boss, Nna kila kitu ili kujifariji tu.

Natamani sana ningekua nimeyapatia...


Kikubwa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai na afya njema.

Elimu haimpi mtu uhakika wa kufanikiwa, lakini inafungua fursa na kukupa uwezo wa kutazama mambo kwa namna tofauti kupata majawabu ya changamoto tunazopambana nazo.

 
Kweli kabisa shule zipo kufilisi tu.
Mfano huyo aliye letwa kama mada hizo hela za ada angezifanyia kazi ingine si ingekuwa swala zuri
kwanza shule zina wenyewe wengine nyota zao ni kuchunga mbuzi na biashara huko tusforce mambo
 
Back
Top Bottom