Huyu, HANAGA Mpinzani BONGO NZIMA

Sie watu wa pwani ndo tulomfunda huyu mzee wenu kuvaa kistaarab (sarawili + kikoi), yy alikua mtu wa makaputura na masulupwete..pichani dhahiri ni baada ya kuoneshwa jinsi ya kuketi wakti ukialikwa ustaarabuni. najua wabara mtapinga/

sasa mbona kila kukicha mnamlaumu???
 
wanaomchukia nyerere ni wale wenye element za kifisadi na waliokataa kuwapeleka shule watoto wao au walikataa wenyewe kwenda shule eti watalishwa nguruwe....
aliweza ku-debate na wazungu hadi wakaiacha tanganyika huru..wale wazee wa saigon shule sufuri wameishia kulalamika wakati walipowaona wazungu walikimbia sababu lugha haipandi
 
305901_493865240654303_791731685_n.jpg

kweli mtu wangu!
 
Msingi wa uchumi mbovu huyu ndo aliyeutengeneza.Halafu leo mnamsifia kweli hamnazo.Ila yako mazuri amefanya ila ni machache sana ukifananisha na uharibifu aliofanya

msingi wa uchumi mbovu ni wa kuwatunzia rasilimali kama madini ambazo mnakuja kuzitapanya kwa ulafi...

msingi wa uchumi mbovu ni viwanda kama vya nguo...karibu kila mkoa ...una umri gani? unakumbuka MUTEX,MWATEX,KILITEX,SUNGURATEX? Mmeviuza ? kwa bei ipi?

msingi wa uchumi mbovu ni kujenga mahusiano na wachina wazambia na kujenga reli...niambie nchi ngapi za kiafrika zimejenga reli baada ya uhuru? yeye aliwezaje?

msingi wa uchumi mbovu ni kutaifisha barclays na kuifanya benki ya taifa kwa ajili ya wananchi na ninyi baadaye mkaiuza kwa bei ya kutupa...yeye wakati anataifisha aliwalipa waingereza fidia yao na wakaridhika,mlijua hilo?
 
wanaomchukia nyerere ni wale wenye element za kifisadi na waliokataa kuwapeleka shule watoto wao au walikataa wenyewe kwenda shule eti watalishwa nguruwe....
aliweza ku-debate na wazungu hadi wakaiacha tanganyika huru..wale wazee wa saigon shule sufuri wameishia kulalamika wakati walipowaona wazungu walikimbia sababu lugha haipandi

wazungu watuache?! Hivi unatambua Ukoloni mambo leo? (Neo colonialism)
 
Angekuwa wa maana sana kama hangetufikisha alipotufikisha. Pengine ubwana mdogo ni bora uulize tulifika wapi au waambie hao wenzio wakuonyeshe kitu chochote cha maana ili uwe na kumbukumbu ili usiwe unashabikia bila ya kuwa na kitu cha kuonyesha kilichofanywa na huyo babu yako.
Hivyo unafikiri huo uhuru alipigana peke yake?
 
hakupiganaia uhuru peke yake lakini yeye ali-play a great role,kuhusu uchumi tafuta takwimu za kipindi cha nyerere na sasa,angalia thamani ya fedha enzi za nyerere na sasa,alikusomesha bure hadi chuo bure(if you ever got there)bila dhahabu na almasi,tanzanite,..uzalendo ulikuwa mkubwa kuliko sasa..on top of that hakujilimbikizia mali kama hawa wa sasa ambao utajiri wa watoto wao ni sawa na bajeti ya wizara...sihitaji kuwepo kipindi cha nyerere kujua historia,kama ulikuwa muhujumu uchumi utamchukia nyerere hadi kufa...
 
wazungu watuache?! Hivi unatambua Ukoloni mambo leo? (Neo colonialism)

kipindi cha nyerere hakukuwa na hicho kitu neo-colonoialism!!!nyerere wasn't a western puppet broda,infact he was against all western oppression ndio maana alipigania uhuru wa kweli wa bara zima la afrika,waulize msumbiji,zimbabwe,south africa,namibia,angola,wanamjua huyu mzee
 
Nyerereism bado inawasumbua! Hata wakijitahidi wanashindwa kwani bado wako wengi wanadanganywa na utakatifu wa nyerere hivyo si rahisi kuuacha hata kwa mdomo tu na nyuma ukimpinga kwa vitendo!

Mimi naona wengi wenu bado hamjui mnasema nini, pengine naomba mnitajie basi viongozi bora wa Tanzania ili tuwamwagie sifa na pongezi, na ili tumchafue Nyerere kwa kulinganisha.Vinginevyo ni roho mbaya, udini, ushabiki, kukosa shukurani na kukosa moyo wa uzalendo hasa ndivyo vinavyokusumbueni!
 
Hakuna binadamu asiyekuwa na mapungufu yake, na Mwalimu hakuwa malaika ila pale alipofanya vizuri ni vema asifiwe

Enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna matabaka ya waliokuwa nacho na wasiokuwa nacho kama sasa, kulikuwa hakuna rushwa kama ilivyo sasa,

Alikuwa anaudhubutu wa kukemea maovu na kuadibisha waliokosea.

Nani kakudanganya?
 
Mimi naona wengi wenu bado hamjui mnasema nini, pengine naomba mnitajie basi viongozi bora wa Tanzania ili tuwamwagie sifa na pongezi, na ili tumchafue Nyerere kwa kulinganisha.Vinginevyo ni roho mbaya, udini, ushabiki, kukosa shukurani na kukosa moyo wa uzalendo hasa ndivyo vinavyokusumbueni!

Kijana hii mada haikuanzishwa nasi tulo wadini na roho mbaya bali ilianzishwa na watu kama nyinyi wadini na wasiofahamu au wasiotaka ukweli. Jambo la busara ni kuwa nenda na changamoto yetu kwa kutuletea mazuri ya huyo unayemuona mtakatifu ili tuyajadili na sio kusema kitu fulani kizuri huku ukiulizwa uzuri wake unashindwa kuutowa.
 
hakupiganaia uhuru peke yake lakini yeye ali-play a great role,kuhusu uchumi tafuta takwimu za kipindi cha nyerere na sasa,angalia thamani ya fedha enzi za nyerere na sasa,alikusomesha bure hadi chuo bure(if you ever got there)bila dhahabu na almasi,tanzanite,..uzalendo ulikuwa mkubwa kuliko sasa..on top of that hakujilimbikizia mali kama hawa wa sasa ambao utajiri wa watoto wao ni sawa na bajeti ya wizara...sihitaji kuwepo kipindi cha nyerere kujua historia,kama ulikuwa muhujumu uchumi utamchukia nyerere hadi kufa...

Kama aliplay sasa wawapi hao wengine na kwanini hawatambuliki michango yao na kumfanya huyu mmoja kama Mungu/
Kusoma bure lilikuwa ni swala la wakati na ndio maana ikawa kulikuwa na matabaka fulani na majimbo fulani yaliyofaidika.
Hao wanaomiliki mali maadam ni watanzania hawafungwi kuwa ni watoto wa nani iwapo tu mali zao ni za halali.
Nyerere alishindwa kabisa kisera na kuongoza na hao viongozi tulionao bado ni zao lake ,ni yeye aliewalea.
Nyerere aliifikisha nchi pabaya kiasi cha kuondoka kwa aibu. Alisema hawezi kugeuka jiwe.Uliza kwanini alisema hivyo?
 
Kijana hii mada haikuanzishwa nasi tulo wadini na roho mbaya bali ilianzishwa na watu kama nyinyi wadini na wasiofahamu au wasiotaka ukweli. Jambo la busara ni kuwa nenda na changamoto yetu kwa kutuletea mazuri ya huyo unayemuona mtakatifu ili tuyajadili na sio kusema kitu fulani kizuri huku ukiulizwa uzuri wake unashindwa kuutowa.
naona unawasifu na kuwapenda sana wale na hawa wanafisadi nchi, mpaka mkuu wa kaya anasema orodha yao ninayo lkn anawaogopa, tupeni basi waliofanya vizuri kuliko Nyerere!!!!!!!!!!!!!!!
 
Iwapo waliopita baada ya Nyerere si wazuri, haimfanyi Nyerere kuwa mzuri kuliko wao. Mbona mifano ni mingi tu, tukianzia na hii nafasi uliyoipata ya kumsema kiongozi kama unavyopenda hungeipata wakati wa Nyerere,alikuwa Nyerere alieuwa uhuru wa vyama vya siasa, alikuwa Nyerere aliyowapa umasikini Watanzania kwa kuwaondowa kwenye mashamba yao na kuwapeleka vijijini ambako hadi sasa hakuna hata kimoja kitakachosemwa kuwa ni mfano.
Hawa viongozi wa sasa wa pande zote mbili, tawala na upinzani si alikuwa nao Nyerere? kwanini basi hata hao tunaowaona kuwa ni wakombozi na wapinga ufisadi hawakumuunga mkono Nyerere hata akaangukia puwa?
Kila kiongozi anakuwa na mabaya yake na mazuri yake lakini hili la kusema kuwa mmoja eti alikuwa perfect ndilo nalikataa.
 
Sie watu wa pwani ndo tulomfunda huyu mzee wenu kuvaa kistaarab (sarawili + kikoi), yy alikua mtu wa makaputura na masulupwete..pichani dhahiri ni baada ya kuoneshwa jinsi ya kuketi wakti ukialikwa ustaarabuni. najua wabara mtapinga/

Hivi watu wa pwani ni wastaarabu?wengine ukisema we mtu wa pwani ni kujidharaulisha.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom