huyu hana mpinzani,Mungu amlaze mahali pema peponi.AMeen | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

huyu hana mpinzani,Mungu amlaze mahali pema peponi.AMeen

Discussion in 'Jamii Photos' started by Zasasule, Sep 9, 2010.

 1. Zasasule

  Zasasule JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  JKN1.png

  JKN4.png
   
 2. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  KAMA SI HUYO ZANZIBAR INGEUKUWA KAMA ULAYA:playball:
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Ndio katuachia mdudu huyu CCM na mifumo yooote mibaya ya utawala:confused2:
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani alale jehanamu na achomwe Sanaa na moto maaana hay mauzauza ya ccm eye ndo ameleta
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  All in all, he was just a human being, sio vizuri kumwombea mabaya marehemu.
   
 6. Zasasule

  Zasasule JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  watu hata emaan ya huruma kwa binadam mwenzao
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kuna aliyokosea, tena mengi. Lakini inatupasa kukiri kwamba siku zote alikuwa mzalendo mkubwa. Hakutawaliwa na ubinafsi na kutaka kujilimbikizia mali.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mmmh uchumi alifeli kwa kweli na kutuwekea utawala wa kiimla na hili DUDE BAYA kabisa linaloitwa CCM, na kutuulia nchi yetu pendwa TANGANYIKA na kutuletea nchi ya kusadikika inayoitwa Tanzania.
   
 9. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hi legacy will last longer! Hakuwa Fisadi, hakuwa na tamaa, aliipenda nchi yake sio hawa wa leo wanapenda mali ya nchi hii lakini hawaipendi nchi yetu hata kidogo, fedha wanatunzia nje ya nchi, hapa wanaiba na kuhamisha! He was a man of people!!!!!!!!!!!!!!! Alisema wazi kuwa mabaya yake tuyaache ila tuendeleze yale mema alofanya,
   
 10. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mwacheni tu apumzike, yaani nachukia wale wanaofikia kiasi cha kumwita saint
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ulikuwepo wakati wake?
  Hana mpinzani?
  Waliompinga aliwasweka ndani ama kuwapoteza ama walikimbia nchi.

  Unamjuwa Kambona? Unamjuwa Sheikh Takadiri? Unamjuwa aboud Jumbe?

  Uliza walifanywa nini na huyo!
   
 12. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilikkuwepo wakati wake. Namfahamu Oscar Kambona na Mkewe Flora Kambona (aliyepata kuwa mwenyekiti cha chama chao). Namfahamu Aboud Jumbe. Nafahamu walichofanywa na nafahamu walichofanya. Nafahamu pia sababu za waliokimbia kuamua kukimbia.

  Jibu langu kwako,
  "Tatizo ni udogo wa mawazo, Umasikini wa mawazo ni umasikini kweli kweli. Anaweza akaja tapeli akakwambia hii uliyoshika si almasi ni kichupa tu ila ya kwangu ndiyo almasi. Basi we ukasema "Nipe" halafu ukatoka unashangilia kama zuzu......!!!" - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Burito.

  RIP Mwalimu. A visionary Leader, A writer. A Farmer. A Teacher. A patriotic Citizen. Our Child. Father of the Nation.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Lakini hakubeba na vichwa vyetu akaenda navyo kaburini. Kama aliweza kutengeneza formula ya kututawala na CCM, na tumegundua makosa katika formula hiyo, kwanini tusitengeneza formula ya kukataa na kubadili mfumo alioujenga?
  Mara nyingi matatizo hata kama ni ya kwetu tunapenda kumsukumizia mtu mwingine tukidhani ndio namna bora ya kujiondoa kwenye tatizo hilo, and yet tatizo linabaki kutuandama wenyewe.
  Kwa bahati nzuri, Nyerere did his part successiful.Alisimamia aliyoyaamini mpaka dakika ya mwisho bila kutetereka.
  Kama sisi tutafeli, hakuna atakayetusikiliza kama tutaendelea kumsingizia Nyerere.Hiyo itakuwa failure yetu wenyewe. Jamani tuache lawama zisizo na msingi. Tuanze kubadili fikra zetu watanzania na kujifunza kusimamia kwa vitendo yale tunayoyaamini.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hana mpinzani kwa mengi........ mema na mabaya
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Katika watatu tu wa Mwanzo nilowataja umewafahamu wawili tu? Jee huyo watatu?

  Kweli, inabidi umsifu. Kwani inaelekea ni mmoja wa wale waliofaidika na uDikteta wake na hukuwa na hisia za mamilioni aliowatesa, maelfu aliowauwa na maelfu kama si malaki aliowadhulumu.

  Laiti ungekuwa unatazama na upande wa pili wa shillingi.
  Leo, kila mTanzania, kwa njia moja ama nyingine analia kivyake. Anenyimwa haki mahakamani, anaekuwa harassed na polisi anaelilia ufisadi anaekosa haki za msingi wa masomo na afya.

  Jee hujui au hutaki kujuwa kuwa hiyo ndio legacy ya Nyerere.

  Kang'atuka kaiacha nchi inanuka kwa uozo, haina fedha bank, mpaka kaichoma mto benki kuu kabla ya kung'atuka, kachoma moto makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani, kabla ya kung'atuka. Kaacha nchi haina hata diesel ya kuendeshea magari machache yaliokuwepo, seuse ya kuendesha viwanda. Kaacha watu, majority, hawana elimu hawana matibabu, hawana hata kanda mbili za kuvaa kwendea chooni.

  Hiyo ndio legacy? Au yote hayo hukuyaona kama ulikuwepo?
   
 16. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo interest yako ilikuwa nitaje wote uliowataja? Basi nitawataja wote halafu nitaongeza na wengine.

  1. Kambona
  2. Jumbe
  3. Sheikh Takadiri
  4. John Okello
  5. Brigadier Mayunga
  6. X - man
  7. Tuntemeke Sanga
  8. Mwinyi
  9. Malecela
  10. Horace Kolimba
  11. Jakaya Kikwete
  12. Edward Lowassa
  Unahitaji zaidi? Actually, haikuwa interest yangu kutaja watu. Interest yangu ni kujibu hoja na mantiki. Sidhani kama ugomvi wako ni Nyerere kufanya aliyoyafanya kwa watu hao ila Nyerere alivyoperform kiutawala na "kutumia ubabe kuongoza nchi," hii ndiyo ilipaswa kuwa interest yako. Kama nia yako nimtaje Sheikh (sikumtaja ili nikupime, bahati nzuri/mbaya umeingia mtegoni) basi sitajadili chochote na wewe. Japo nafahamu uwezo wako ni mdogo kupambanua mambo lakini nilijipa moyo nikujibu. Kinachonifanya niseme uwezo wako wa kufikiri ni mdogo ni pale nilipotaja wawili kati ya watatu uliowataja badala ya kunibana niseme hao wawili nawafahamu vipi ukaishia kudai sijataja watatu. Hivi suala ni kutaja tu? Hivi unajua hata hao wawili niliowataja ninawalaumu au kuwasifu kwa lipi? Je katika majibu yangu nimewataja hao wawili kuwa wabaya au wazuri? Sasa katika mazingira kama haya unadhani nitavutiwa kujadili na wewe? Ikiwa mambo madogo kama haya huwezi kuyapambanua je tutakapoanza kujadili kuhusu kitabu cha Karl Marx "Communist Manifesto" au cha Newton "Principa Mathematica" tutaelewana kweli? Kumbuka hapa sizungumzii falsafa nazungumza mfumo wa kufikiria.

  Mtu anaweza akakusoma tu akili yako kutokana na unavyoandika. Watu wanaosema "kuuwa" badala ya "kuua" au kusema "dhulma" badala ya "dhuluma" (nazungumzia Kiswahili sanifu) ni watu wa kada moja. Unahitaji kujifunza pia misingi ya maisha kuliko kuingia kichwa kichwa kuubeba urithi wa "katuonea sana. Kazuia dini yetu. Katunyima TV...."

  Watu wa aina yako huwa hawataki kwenda shule halafu wanalaumu kuonewa kimaisha. Hawataki kufanya kazi, wanaishia kucheza bao halafu wanalaumu mtu mwingine kwa umasikini wao. Wanazuia watoto wao kufanya kazi za maendeleo na kwenda sekondari halafu wanadai wanataka nafasi sawa serikalini.

  Summary:
  Sikusudii kuendeleza mjadala na wewe kwa kuwa hutoelewa hoja zangu. Kama ungezielewa na ukazipinga kwa hoja ningekuelewa. Usipozielewa na ukazipinga bila hoja sitakuelewa, sijui hoja yangu umeielewa?

  Sote tuko duniani. Ni lazima utambue sasa u kijana (nimeangalia mfumo wako wa kufikiri na mtiririko wa mawazo kutokana na maandishi yako) unahitaji kufanya kazi na kujifunza busara za dunia. Chuki unazofanya kwa Nyerere na "watoto wa jirani" hazitakusaidia kwa kuwa hautawashinda watoto wa jirani. Kuna muda wewe utakuwa mzee una meno mawili tu mdomoni, mgongo wako hautakuwa na uwezo wa kunyooka na hautaweza kufanya kazi tena kwa sababu nguvu za mwili zitakuwa zimeisha. Wakati huo utakuwa ukisubiri kwenda jehanamu kwa kuwa ulisahau kutenda mema na muda wako ukautumia kumlaumu Nyerere. Hutakuwa na jibu la swali "Ni nani alikuwa imam wako ulipokuwa duniani?" Watoto wa jirani yako waliojikita katika elimu watakuwa wakikudondoshea shilingi mia kama watakuwa na sarafu mifukoni mwao.

  Fanya kazi. Soma. Jifunze maarifa. Jifunze falsafa. Jifunze saikolojia. Jifunze busara. Jifunze kufikiri kisayansi. Mheshimu Mungu. Tambua umri wako na badilika, kucheza na wanasesere waachie watoto.
   
 17. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Endelea kuchukia.
   
 18. S

  Somi JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nilipata kuambiwa mwalimu hakupenda kunyonga kabisa hata ktk utawala wake hakunyonga mtu kabisa na ikumbukwe kipindi cha miaka ya 60, 70 na 80 kulikuwa hakuna harakati za kutetea haki za binadamu nchi za africa watu walinyongwa kama kuku mfano kenya, uganda,malawi na zaire. Hawa kina kambona na wengine walikwaruzana na mwalimu kwa sababu walikuwa na mitazamo isiyofaa ktk kujenga taifa changa la tanzania na walikuwa na mitazamo ya maslahi yao binafsi zaidi .Nafikiri mwalimu alijenga msingi mzuri ktk taifa changa kama hili hata tanu na ccm ya mwalimu ilikuwa na misingi mizuri. Mwalimu alitaka wananchi wote wasipishane kipato hii inapunguza ujambazi,wizi, hongo,rushwa nk na alitaka serikali itoe bure huduma kwa wananchi mfano elimu, afya nk na haya yote ndio nchi za scandinavia na baadhi ya nchi nyingine za ulaya wanatekeleza. Kwa ujumla mawazo mengi ya mwalimu yalikuwa mazuri ila watumishi wake hawakumwelewa. Kama mwalimu angeliongoza sasa wakati nchi ina maliasili ya kutosha south africa na nigeria pekee ndio zingetupita kimaendeleo. Mwalimu aliileta zanzibar ili ilindwe na tanganyika kama sio hivyo zanzibar ingekuwa kama comoro kila siku kupinduana kwa watu wa zanzibar wamshukuru mwalimu, hata karume alipouwawa kama zanzibar haikuwa chini ya tanganyika ingepinduliwa.
   
 19. mapango

  mapango Member

  #19
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hamna kitu hapo, huyo ndio aliyewafanya watanganyika kuwa wadanganyika kwa kuwanyima elimu, na ndio tunaona matunda yake leo..., ni mtu asiyestahili heshima ya kuitwa baba wa taifa bali adui wa taifa.
   
 20. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #20
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Public stunt. Mtu anafanya kazi huku analindwa na polisi.
   
Loading...