Huyu Fundi Wangu Ananipiga?

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,420
Wakuu nipo kwenye shughuli ya ujenzi wa kibanda changu. Tatizo nalopata ni bei za ufundi (leba chaji) anazonitajia huyu fundi ninayemtumia. Simuelewi kwa sababu naona kama anakurupuka kutaja chaji zake.

Mfano vifaa vitaweza kuwa za laki 3, utakuta yeye anataka leba chaji ya laki 6-7, yaani chaji yake inakuwa mara mbili ya hivyo vifaa vya kazi. Sasa nashindwa kuelewa hii ni sahihi au huyu mtalaam wangu ananipiga kiaina.
 
Wakuu nipo kwenye shughuli ya ujenz wa kibanda changu. Tatizo nalopata ni bei za ufundi (leba chaji) anazonitajia huyu fundi ninayemtumia. Simuelewi kwa sababu naona kama anakurupuka kutaja chaji zake.

Mfano matilio zitaweza kuwa za laki 3 utakuta yeye anataka leba chaji ya laki 6-7, yaani chaji yake inakuwa marambili ya hizo matairio za kazi. Sasa nashindwa kueleweshwa hii ni sahihi au huyu mtalaam wangu ananipiga kiaina.

Anakupiga wapi? Tulia tu atamaliza uendelee na shughuri zake.
 
Kikawaida labour charge huwa ni 30% mpaka 40% ya material cost,hivyo unapobagain naye bei unalala humo humo kwenye hiyo formula hiyo hapo juu
 
pole sana
ili uweze ku deal na mafundi
1. pata mshauri ambae ni mzoefu wa ujenzi, awe architect, engineer au fundi alie na experience, kila cost za labour na materials awe ana hakiki, sio unatajiwa bei mafichoni.
2. hata materials japo unaweza kua unanunua wewe, uwe mwangalifu unaweza kua unajenga nyumba ya mwingine pia
3. kwenye mikataba mingi ya ujenzi mara nyingi labour hua 25% to 40% ya cost ya materials, but its not always the case. kwa mfano unataka kuweka kuweka sink la kunawia mkono.. ukinunua brand ya kawaida ni 250,000 na ukinunua brand quality kama roca, grohe etc labda ni mil 3. ss huwezi tumia assumption ya 25-40%
4. kwa sbb bei za mafundi haziko that specific, kila unapokua na kazi ita mafundi wasiopungua wa 3 na wajue kua umewaita wa 3, ili wakupe competitive prices uweze kufanya comparison ya bei na evaluation ya kawaida ya mtu.
5. usihisi hua kuna fundi wako au ambae anakufaa, wako mafundi wengi sana na wazuri
6. ongeza muda kwenye kazi yako, kama huna muda tafuta mtu akusimamie mwenye muda.
7. hongera kwa ujenzi. kila la kheri.
 
8. hua hakuna fundi ambae anajua kila kitu, yani yy ni wa umeme, matofali, plumbing, tiles, fundi jiko... usitumie fundi mmoja kufanya kazi zote.. ukifanya ivo anakua dalali. mwambie akuletee fundi unaemhitaji ili uongee nae, au la msource from different recomendations. so tegemea kua na mafundi wengi.
binafsi naona dalili za wewe kukaa ofisini na kumpigia simu fundi wako huyo mmoja na kumuuliza bei ya vifaa ngapi na vp na labour yako ngapi. be more involved.
 
Kikawaida labour charge huwa ni 30% mpaka 40% ya material cost,hivyo unapobagain naye bei unalala humo humo kwenye hiyo formula hiyo hapo juu
Inategemea mkuu....mfano nataka kuweka choo cha 500,000 na shower 250,000 nitampa 225,000??!!! Hapo anapewa maximum 50,000 tu,kuna vitu vya kupatana % hazifai.
 
Back
Top Bottom