Huyu mwanamke wa Kitswana kutoka Afrika Kusini anaupendo wa kweli au ni tapeli wa mtandaoni?

Kwa hiyo wewe mchecheto wote huo ni kwa sababu anatoka Afrika Kusini! Sasa huyo ana tofauti gani na Mmakonde wa huko Nachingwea! Kweli nchi hii kuna mazuzu! Hiyo Diploma yako kule sana sana atakutafutia kazi ya kuchunga farasi au punda!
Tena diploma ya ualim duuh
 
Mkuu unataka kuniambia Wabongo wote walioko nje au south Waliooa na kuhamishia makazi huko Nje nao wamefunuliwa hayo marinda???Au umeamua kunitusi tu?
Hahahah mm nikipata nafas hiyo siiachi usisikilize maneno ya walio shindwa mkuu hana rafik yake
 
Ushauri wangu usiende kwa madiba, labda kama utakuwa na dili nyingine tofauti na hayo mahusiano kama anataka ndoa na wewe aje yeye pia usijaribu kutuma pesa wala nini mwambie afanye analo weza aje yeye kama ni gharama n.k utazilipa akiwa huku. Basi jichanganye utalia na kusaga meno kwanza una wajua maaskari wa south wewe....?
 
Ushauri wangu usiende kwa madiba, labda kama utakuwa na dili nyingine tofauti na hayo mahusiano kama anataka ndoa na wewe aje yeye pia usijaribu kutuma pesa wala nini mwambie afanye analo weza aje yeye kama ni gharama n.k utazilipa akiwa huku. Basi jichanganye utalia na kusaga meno kwanza una wajua maaskari wa south wewe....?
Poa kaka mawazo mazuri
 
Jiulize maswali hata...
1. Kwa nini uende?
2. Kuna umuhimu wa kwenda?
3. Umejiandaa vipi endapo utaamua kwenda au kutokwenda (kisaikolojia)
 
Salamu zenu Wakubwa,

Mimi ni kijana Mwenzenu wa Kitanzania mwenye miaka 29, Sina mtoto wala mke,Nina diploma ya Ualimu na Kwasasa nafanya kazi Katika Moja ya Shule Binafsi hapa Dar.

Kilichonifanya nije kwenu Wandugu kuomba Ushauri Ni takriban Mwezi mmoja sasa Katika pitapita huko kwenye Mitandao nikakutana na Binti Mmoja Mrembo anayeishi Katika jiji la Pretoria, South Africa Kabila lake ni Mtswana, Basi tukaanza urafiki na hatimaye tukawa wapenzi wa( Mtandaoni).

Tumekuwa tukichat na kuwasiliana kwa Video call kila siku lakini hatujawahi Kukutana face to face lakini Sasa Binti anasema amenielewa anataka nimuoe kabisa tufunge ndoa na tuishi pamoja hivyo ameniomba niende Kuishi huko kwao Afrika Kusini na amesema yupo tayari nitakapohamia kule anipiganie nipate kazi na atanisupport mpaka pale nitakapoweza kusimama kimaisha.Kwa ujumla amesema yuko tayari kuback up katika harakati zangu zote pindi nitakapowasili huko bondeni.

Wakubwa Nipo njia panda sielewi anayosema ni kweli au ni janja ya Kuiingiza kingi wanipige...Msaada wenu wa mawazo tafadhali.
Nenda ukaliwe 0679
 
Mimi nachokushaur hapo usikurupuke mkalishr bench kwa huyo bint kama anania kwel ata vumilia coz kuna watu huwa wanaenda huko south kwa kigezo kuwa wamepata wachumba....
Mfano kuna binti alipatana na mkaka mtandaoni kaka huyo anaish south sasa uyo kaka akatoka south akamfuata TZ wakaspend mkaka akataka waondoke wakaondoka wote from TZ to south kufikia uko alifikia hotelin bint kufika tu akashikiwa bastora akabebeshwa madawa vya kulevya kinguvu akaambiwa apeleke nchi za nje kufika huko wakamkamata akafunga ni mwaka wa6 tangu afungwe story adi mirad Ayo aliipost kama huwa mnamfuatiliaga SO KUENI MAKINI VIJANA punguzeni tamaa watu wengi hutumia wadada warembo na wakaka watanashati kwakigezo cha mahusiano
 
Mimi Nina mbinu nyingi za kiuchunguzi. Nipe mawasiliano yake then subir baada ya masaa 48 tu nitakupa majibu Kama uende au umpotezee.
 
Acha kukutisha mwenzio tamaa sio poa mwache Akajarb bahat yake tena mkuu aisee kama anarafik yake mwambie nipo twenzet kwa madiba tukapambane

Mwambie aende Mahuta Newala au Mahiwa Masasi atawakuta hao Wamakonde, hakuna haja ya kuhangaika na mtu ambaye hana hata nauli ya kutoka Ndugumbi kwenda Matombo Morogoro!
 
Back
Top Bottom