Huyu DAS Monduli ana tatizo la kimsingi kielimu

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,803
13,034
Gazeti la leo Mwananchi pg 3, limemnukuu Katibu Tawala Wilaya ya Monduli, Ndg Robert Siyantemi "akishauri" utafiti wa kisayansi ufanyike kuona uwezekano wa kutumia damu za wanyama kuwaongezea binadamu wenye mapungufu!

Hapo nimechoka!!

Maswali kadhaa yananijia kichwani, je kasoma biolojia ya msingi, form 1 hadi 4?
Au alisoma tu masomo ya biashara?
Hili aliliongelea mbele ya wadau wa afya mkoani Arusha, je hana washauri?

Kidogo mtu mwenye madaraka kuongea mambo asiyo yajua, ni kuji expose ujinga hadharani.

DAS Monduli, pole!
 
Gazeti la leo Mwananchi pg 3, limemnukuu Katibu Tawala Wilaya ya Monduli, Ndg Robert Siyantemi "akishauri" utafiti wa kisayansi ufanyike kuona uwezekano wa kutumia damu za wanyama kuwaongezea binadamu wenye mafungufu!

Tunaposhauri wagombea wapimwe akili huwa mnatuona hatuna akili, nasikia eti naye alichukua fomu ya urais kwa chama pendwa, je kwa bahati mbaya angeteuliwa na kushinda ingekuwaje.
 
Mie nimesikia sikuamini! Sio kwamba ni malaria ilipanda kichwani kweli? Kwani hata std 7 nafikiri atapingana na hilo. Hata kama alisoma biashara , Biology inafundishwa hadi form 2 kwa Enzi yake hajui magroup ya damu kwani? Shame on him!
 
"The one who has knowledge uses words with restraints, and whoever has understanding is even-tempered. Even fools are thought wise if they keep silent, and discerning if they hold their tongues". Proverbs 17:27:28
 
Mimi sioni kosa lake maana kasema utafiti ufanyike. Mbona tafiti zinafanyika tu kugundua mambo muhimu? Mbona insulin ya nguruwe inatumika kutibu watu wenye kisukari? Kama tafiti ikifanyika na kukaoneka kuna mnyama anaendana na mwanadamu kwa damu sio mbaya. Ni miongoni mwa tafiti tu. Lakini wataalamu wanasema mnyama ambaye damu yake inakaribiana na mwanadamu ni nguruwe!!!!!!! Hapo sasa ndo pagumu. Kikubwa tafiti zifanyike ili kuendeleza ugunduzi. DAS hana makosa. Katoa maoni ili tafiti zifanyike. Asubuhi njema wote.
 
Hii serekali yote kuanzia juu hadi chini ina watu wenye uelewa wa ajabu Mno!!! Kama mtu aliesoma uchumi kwa ngazi ya PhD hajui VAT inalipwa na nani, na kama mtu Mwenye PhD hajui Sadam Hussein alikuwa raisi wa nchi gani au wananchi wakipata janga la tetemeko sehemu nyingine huwa wanapewa msaada unategemea huyo ambaye hata elimu yake haijulikani ajue chochote kweli!!! Itakuwa tunamuona.
 
Mkuu watu wanafikiri kuwa na Phd ni kufahamu kila kitu, la hasha.
PhD ni streamlining of knowledge on to a very particular field.
Mtu anasomea na kutafiti kitukidogo na kwa undani Zaidi.
Na si kila kitu.
 
Gazeti la leo Mwananchi pg 3, limemnukuu Katibu Tawala Wilaya ya Monduli, Ndg Robert Siyantemi "akishauri" utafiti wa kisayansi ufanyike kuona uwezekano wa kutumia damu za wanyama kuwaongezea binadamu wenye mafungufu!

Hapo nimechoka!!

Maswali kadhaa yananijia kichwani, je kasoma biolojia ya msingi, form 1 hadi 4?
Au alisoma tu masomo ya biashara?
Hili aliliongelea mbele ya wadau wa afya mkoani Arusha, je hana washauri?

Kidogo mtu mwenye madaraka kuongea mambo asiyo yajua, ni kuji expose ujinga hadharani.

DAS Monduli, pole!

ndiyo maana ameshauri utafiti wa kisayanzi ufanyike!!!

Kwa taarifa tu ni kwamba kuna habari kuwa utafiti unaendelea ili figo za wanyama ziweze kutumika kwa binadamu

angalia utafiti huu Researchers investigate use of pig kidneys for human transplant
 
Mkuu watu wanafikiri kuwa na Phd ni kufahamu kila kitu, la hasha.
PhD ni streamlining of knowledge on to a very particular field.
Mtu anasomea na kutafiti kitukidogo na kwa undani Zaidi.
Na si kila kitu.

Je hao wenye hizo PhD wanaamini hili unaloamini ww?
 
Monduli ni wilaya pekee mpaka leo watu wanalala kwenye nyumba za mavi ya Ng'ombe, wanakunywa maji na Ng'ombe

Huenda hiki ndio kimemushawishi Das
 
ndiyo maana ameshauri utafiti wa kisayanzi ufanyike!!!

Kwa taarifa tu ni kwamba kuna habari kuwa utafiti unaendelea ili figo za wanyama ziweze kutumika kwa binadamu

angalia utafiti huu Researchers investigate use of pig kidneys for human transplant
Kulingana na uelewa, hatua ya kisayansi na maendeleo yetu, technologia tuliyonayo, research outlay and funding, one might as well be asking for the moon!!
Na hapo nauliza busara iliyotumika ukilinganisha na mazingara tuliyonayo.
Hilo lingesemwa kwenye Scientific Symposium ningeelewa!
 
Je hao wenye hizo PhD wanaamini hili unaloamini ww?
Mkuu hilo ni kosa, kuna katabia kuona na kuhisi kwamba mtu aliye na PhD anajua kila kitu.
Ukweli mnauona wenyewe, mtu anakuwa anajua sana kwenye ILE FANI TU ,ALIYOIFANYIA UTAFITI, na si vinginevyo.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom