Huyu Babu Mwanga nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu Babu Mwanga nini?

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, May 17, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 508px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td style="text-align: center; width: 518px;" valign="top">Huyu Babu Mwanga nini?</td> </tr> <tr> <td style="text-align: center; width: 518px;" valign="top"> [​IMG]</td> </tr> <tr> <td style="text-align: center; width: 518px;" valign="top"> Mwanaume huyu ambaye hakufahamika jina lake, alifumaniwa uchi wa mnyama nje ya nyumba ya Waziri mmoja wa Serikali ya Tanzania kwa kile kilichodaiwa kuzidiwa nguvu za kichawi. Picha na Mdau wa soka wa jijini Dar es Salaam, Mama Romana</td></tr></tbody></table>
   
 2. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani hii ni kali kweli kweli...... WATETEA HAKI ZA BINADAMU MKO WAPI?????????
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,321
  Likes Received: 22,167
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani waziri ndio mwanga zaidi maana anawazidi wanga nguvu zao.
   
 4. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyu siyo Babu ni kijana mdogo tu wa umri wa miaka 23 alijulikana kama Mohamed alikuwa fundi nguo maeneo ya mbezi beach nyuma ya Hospital ya Massana kwenye msikiti ndipo alikuwa anafanya kazi...

  huyu jamaa kwa sasa ni marehemu baada ya kukutwa maeneo ya mbezi Afrikana akiwa uchi wa mnyama na wakazi wa Afrikana kumpiga kwa kudhania kuwa ni mchawi aliye anguka toka kwenye ungo.

  Huyu jamaa alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya akili na alikuwa na vyeti toka mwihimbili vikionyesha kuwa ni mgonjwa wa akili.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,524
  Trophy Points: 280
  It is sad! very sad!. Alikutwa nyumba ya tatu toka ninapoishi, ni getini kwa Brig. Gen (Rtd) Adam Mwakanjuki. Nilipomuona asubihi wakati nakwenda job, kwa kumtazama tuu, kwa macho ya kawaida, utamjua wazi yuko insane. nikapiga simu home, garder wangu amletee kaptula yangu yoyote. Kaptula ililetwa, kundi la watu wakazui asisetiriwe eti mpaka polisi wafike, nikaenda zangu job.

  Jioni niliporudi nikapata taarifa eti amepigwa mpaka ajieleze, kadri alivyokuwa hajibu kitu ndivyo alivyozidi kupigwa!, mpaka polisi walipofika na kumchukua. Alifikishwa hospitali ya Mwanyamala, next day alifariki.

  Wanga, uchawi, ulozi, etc ni mbaya, ila pia mtu asiye na akili timamu au aliyechanganyikiwa ukimuona utamjua tuu, haihitaji akili za kidaktari kumjua huyu hayuko sawa, watu wa pale walimpiga kwa kosa gani?.

  Kwa vile nchi yet inaendeleza hukumu ya adhabu ya kifo, wananchi nao wanajichukulia sheria mikononi kwa wao kuwa ndio wapelelezi, waendesha mashitaka na mahakimu hapo kwa hapo, tena very barbaric kwa kuisaidia serikali yao kwenye utekelezaji wa adhabu kama hizi.

  Laiti tungekuwa hatuna adhabu ya kifo, hakuna mob justice ingekuwa inajichukulia sheria mikononi mwao. Najisikia a bit guilt, badala tuu ya kuitisha kijana aletewe kaptula, ningewaita polisi na mimi kuwepo eneo hilo, naamini, ningeweza kuspare maisha yake.

  Nikiwa UD wakati ule niliishi Mabibo Hostel, kuna mwanafunzi wa kike alitibuana na mpenzi wake, akamuitia mwizi, kilichofuatia ni kipigo bila hata kuuliza kulikoni, nilipotaka kutetea japo wamsikilize tuu, ama aliyeibiwa ni nani, hakuna alijitokeza, walitaka kunishukia na mimi kwa madai sijui uchungu wa kuibiwa, niliwaambia najua, but not at a cost of human life, nilishindwa nguvu, jamaa walipiga, wakaua, ukweli ulipokuja kujulikana, it was too late.

  Ndio maana bado nasikitishwa na mwizi wa kuku kufungwa tairi, kumwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto, wakati mwizi wa bilioni 40! za Kagoda anashinda magogoni akinywa chai na mkulu!. Where is justice.
   
 6. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  ??????????????????????????????????? :angry::angry::angry::angry::angry::angry:
   
 7. bht

  bht JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  too sad jamani
   
 8. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #8
  May 17, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yaani we acha tu ndugu yangu, nilipo mwona kwenye tv alivyo kuwa amepigwa nilitokwa na machozi kwani nilikuwa namfahamu alikuwa anani rekebishiaga nguo zangu mara moja moja, na watu waeneo alilokuwa akiishi walikuwa wanajua matatizo yake, siku ya siku alipo kutwa na mkasa huo aliamka alfajiri na kutembea hadi africana alikokutwa na mkasa hou.
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Du kama ndo hivyo kweli inatia huruma!
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Na huyo mwanamama pembeni hapo anapiga picha kwa simu yake kwa mbembwee.
   
 11. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hao wanaopiga picha si wanaonekana kabisa, wakamatwe waeleze ilikuwaje, sheria ichukue mkondo wake...kama walimuua mtu wakati si mwanga,ni mbaya sana, hata kama angekuwa mwanga, si vyema kumwaga damu ya binadamu mwenzetu wajameni....
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Too saaaaaaaaaaaaaaaaaad!
   
 13. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2010
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  .................Sijui kama ni mahali pake, lakini hii habari imeniuma hadi kujiuliza nini hasa kazi za mifuko ya JAMII hapa kwetu? sio kutoa huduma kwa watu kama hawa pamoja na wengine kama vile vikongwe? Au ni kujenga maghorofa tuu??
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hii ndio ile habari iliyo tangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa mwanga alianguka na ungo wakiwa wakielekea kwa mkutano wa wachawi Sherisheri akitokea mwanza?
   
 15. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #15
  May 18, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Haya matukio yapo mengi sana, ili lilitokea mwezi wa tatu mwaka huu, na kuna lingine nimesikia limetokea juzi na huyu wajuzi nae ameuwawa na wana nchi wenye (hasira kali) .
   
 16. M

  MJM JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hapo punje umedondokea chakani na utasongwa na miiba usitoe mazao. Hii ni wizara ya Mama Six inayotakiwa kushughulikia haya lakini sina uhakika kama niliwahi kusikia mipango yake na masuala ya watu wenye matatizo haya, yatima na mambo mengine kama hayo katika jamii
   
 17. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pasco ni sawa lkn kwa ninavyojua mimi,mwizi akiuliwa getini kwako,wewe ndie unayejibu -wacha hilo hata akiuliwa nyumbani kwako amebeba TV yako, wewe ndie unayekwenda kuisaidia police kwa ile tafsiri tuijuayo. Sasa Brig. hakuona jambo hilo na kumuokoa kiumbe wa watu angalau kwa kumuacha apigwe kidogo lakini ampeleke Police?V/V sad lakini raia wasilaumiwe saaaana ,maana siku hizi wezi wamejichanganya kwenye watu wenye matatizo ya kichwa na police wana act kinyume kwa masuala ya hv.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  POLISI na Wapelelezi wangeliwasaka wote waliokuwa kwenye picha na hao waisaidie POLISI kwa kupiga mtu mwenye matatizo ya akili. Ila hata kama hawajakamatwa, basi itangazwe waziwazi kabisa kuwa walioshiriki wote kumpiga, basi WAMESHAKUWA WAUWAJI.
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,468
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Duh
   
 20. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  huyo waziri nae ni mwanga wamezidiana nguvu tu..
   
Loading...