huyu Athmani alifanya nn?

nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
4,771
5,315
wakuu,
Heshima kwenu!
Kuna msemo unasema "Mungu si Athmani"

Naomba kujua na kufahamishwa huyu Athmani
alifanya nn hasa? na kwanini awe Athmani na
asiwe Josefu ama Asha? Kisa kilikuwa nn hasa?

Wataalamu wa lugha naomba msaada.
 
Mungu si Athmani maana yake ni kwamba Mungu sio "mwanadamu" kurahisisha neno hilo ndo maana waswahili wakaamua kutaja jina kabisa la mtu ili ieleweke zaidi.
Ni kweli kabisa MUNGU si mwanadamu ni mtakatifu mnoooo
 
Dah! Umewaza nini hadi kuja na swali hili? Mie nafikiri walichagua jina common tu la binadamu hasa waishio mwambao wa pwani ambako ndiko misemo ya kiswahili hutumika sana,yaani ni sawa na kusema Mungu si Binadamu
 
Tanya;

Mkuu asante kwa maelezo yako mazuri, hii ni misemo ya wa wahenga na mara nyingi huwa ina mafundisho fulani kwa jamii husika! ndo maana cjui na sielewi hasa huyu Athmani alifanya nn mpaka wakaamua kusema Mungu sio Athmani!
Nahisi kuna kitu huyo( ) alikifanya!
 
VUTA-NKUVUTE;
Mungu hana tabia za kibinaadamu

Mzee Tupatupa

Mkuu sana Mzee Tupatupa heshma kwako,
 
mzee wa nguna;
Dah! Umewaza nini hadi kuja na swali hili? Mie nafikiri walichagua jina common tu la binadamu hasa waishio mwambao wa pwani ambako ndiko misemo ya kiswahili hutumika sana,yaani ni sawa na kusema Mungu si Binadamu

Mzee wa nguna nakubaliana na mawazo yako,
 
Inamaanisha kuwa mungu si mwanadamu katika lolote hawezi kudanganywa wala kupendelea upande mmoja
 
Wapoti;
Inamaanisha kuwa mungu si mwanadamu katika lolote hawezi kudanganywa wala kupendelea upande mmoja

Mkuu, huyu Athmani alitolewa kama mfano kwa wengine, hasa jamii iliyomfahamu Athmani halisi na tabia zake alizokuwa nazo!
Mkuu asante umenipa mwanga wa kutosha juu ya hili
 
MUNGU si mwanadamu sawa but why athumani ndio litumike? kwann wasirahisishe tu kwamba mungu si mwanadamu

?
 
Back
Top Bottom