Huyu atakuwa Genius hapo baadaye au?

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Kuna utani kuwa waafrika wengi tukiwa tumelala usingizi, huwa tunaweka mikono yetu maeneo ya viungo vya uzazi wakati wenzetu wazungu huwa mikono inawekwa kichwani.

Hii tabia ya kuweka mikono kwenye maungo ya uzazi imetafsiriwa na wengi kuwa muda mwingi sisi watu weusi/waafrika huwa tunafikiria ngono zaidi kuliko mambo ya kimsingi ya kimaendeleo.

Sasa mimi nina mwanangu ana miezi minne, kila muda anaponyonya huwa anaweka mkono wake kichwani na hata anapolala mara nyingi mikono yake iko kichwani. Anakuwa kama vile anafikiria kitu fulani hivi ingawa bado ni mdogo sana ki-umri.

Hivi hii si ndio ishara kuwa atakuwa genius? Nasema hivi kwa sababu na babu yake alikuwa ni thinking machine!

Nawasilisha wanajamvi!
 
Mtego wa Noti,wewe ukilala mikono huwa una weka wapi?,ata hivyo sio kweli waafrika wakilala mikono huwa wanaweka kwenye sehemu za uzazi,unaweza kutuambia hiyo research uliifanyia wapi??au unataka kuleta story za vijiweni.......!
 
Mtego wa Noti,wewe ukilala mikono huwa una weka wapi?,ata hivyo sio kweli waafrika wakilala mikono huwa wanaweka kwenye sehemu za uzazi,unaweza kutuambia hiyo research uliifanyia wapi??au unataka kuleta story za vijiweni.......!
hahahahahahaha.........swali lako zuri sana, mi mikono yangu maranyingine huwa kchwani na mara ingine maeneo ya vizazi....huo utafiti ushafanyika na wahenga!!!!!
 
hongera kwa kuwa na mtoto genius.............akiwa bongo lala uje utupe taarifa tuthibitishe hiyo research yako
 
huo ni mtazamo wakidhanifu! achana nao unachopaswa katika maisha ni kufikiri mambo ya ulimwengu huu kiyakinifu! sawa sawa
 
Back
Top Bottom