Huyu anayepata 10% ya mshahara anaolipwa Amunike kuna siku Watanzania Watamnyonya macho

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
2,396
2,000
Emmanuel Amunike alikuwa mmoja ya wachezaji wazuri wa naijeria miaka ile ya 90 mnyakyusa huyu na wenzake akina amokachi,george finidi,rashid yekin n.k

Sijajua kwa nini alidhani kuwa mbora katika kusakata kabumbu kungemfanya pia kuwa mbora wa kufundisha.jamaa ameshashindwa katika team yetu ya taifa

Kama anadhani ukocha ni ukali akamuulize Mourihno kilichomkuta. Ukocha ni pamoja na kuwa na saikolojia nzuri ya kukaa na wachezaji kama wadogo zako au watoto wako.

Ni hamasa upendo na kujenga mshikamano.kwa amunike anaonekana kuwa na kiburi,jeuri na ujivuni.namsikiliza kila anapoongea haongei kwa nia ya kujenga.huongea kwa nia ya kutishia na kutaka aogopwe.

Mi nadhani hakupaswa kuhangaika hivyo sura yake tu inatosha kuogofya why na maneno? Kumchagua amunike awe kocha ni kuchagua kushindwa.uchaguaji wke wa wachezaji sijajua unazingatia nini.kama ni nidhamu basi nadhani achague tu walokole na waswahilina.

Lakini hata nidhamu hujengwa taratibu kwa busara na si kutishia watu. Taifa stars ni bora wangepewa hata makocha wazawa lakini huyu jamaa anaturudisha nyuma sana.

Anayachukua 10% percent ya mshahara wake kuna siku watanzania watamnyonya macho hadi yatoke kweye soketi yake.hakuna team ya ushindi chini ya amunike.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,334
2,000
Aisee Amunike ni pasua kichwa. Ingekua amri yake, angechagua mabeki tu na viungo wakabaji kwenye timu ya Taifa. Hataki kabisa kusikia habari ya viungo wachezeshaji kwenye timu kama Hassan Dilunga, Ajibu, Sure boy, nk. Nilipogundua ya kuwa huyu kocha ni bomu, ni ile mechi ya marudiano na Lesotho!

Timu ambayo ilimpa ushindi mnono dhidi ya Cape Verde mechi ya marudiano, aliivuruga kabisa na kupanga timu nyingine iliyojaza mabeki tupu wakati siku zote kwa walimu wa mpira, timu inayowapa matokeo huwa inaachwa icheze kama ilivyo.

Ni ukweli ulio wazi, kufuzu kwa afcon mechi yetu ya marudiano na Uganda; Matokeo yataamuliwa na wachezaji walioitwa, Mashabiki watakaotoa hamasa na na namna Uganda watakavyocheza ila si kwa kumtegemea huyu kocha! Huyu hana kipaji cha ukocha ingawa alishapata mafanikio kadha wa kadha alipokua mchezaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom