Huyu anayeitwa Godlisten Malisa Mungu ambariki sana

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
Abarikiwe sana.
Jamaa kila tatizo anapost mitandaoni ili mwenye shida aweze kusaidiwa.

Post aliyoweka jana hii hapa


Bro shikamoo? Naitwa......

Naishi Goba. Kaka nina shida sana lakini shida yangu sio kukuomba pesa. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24. Naishi na wadogo zangu wawili (mmoja wa kike na mwingine wa kiume). Wazazi wetu walifariki.

Kuwalea hawa wadogo zangu imekuwa jukumu langu pekee na ninapitia changamoto nyingi. Hasa huyu wa kike huwa naumia sana maana kuna wakati nashindwa kumtimizia hata mahitaji yake ya muhimu.

Nina elimu ya kidato cha nne. Nilikuwa nafanya kazi kama utingo wa canter ya mizigo nikajitahid kusave kidogo nikaenda driving school, mpaka nikafanikiwa kukata leseni.

Lakini kupata kazi imekua changamoto kubwa. Nina miezi miwili sina kazi, wadogo zangu wanateseka mpaka sometimes nikiwaangalia nalia siwezi kuwasaidia. Kuna wakati nilitaka kujiua kutokana stress ila nafikiria hawa madogo wananitizama mimi kama baba na mama yao inabidi nijikaze maana nikiondoka nani atawalea?

Ninaomba unisaidie niweze kupata kazi yoyote nitunze hawa wadogo zangu. Najua nitakupa mtihani lakini naomba unitangazie kwenye page yako najua inasomwa na watu wengi sana. Nipo tayari kufanya kazi yoyote kwa uaminifu iwe Udereva wa gari ndogo, ukonda au nyingine itakayopatikana.

Kaka nielewe tuna hali mbaya. Jana tumeshindia uji na mpaka muda huu hatujala chochote. Sina smart phone hii nimeazima kwa mtu ili nikuandikie whatsapp na nikutumie picha ya leseni. Najua unaweza usiwe na kazi ya kunipa ila naomba share ukurasa wako, pengine naweza kusaidika. Samahani kwa kukusumbua kaka.
_________________
Jana nilipokea ujumbe huu kutoka kwa kijana mmoja kupitia WhatsApp. Kwa yeyote anayeweza kumsaidia anicheck inbox nimpatie namba yake. Yupo tayari kufanya kazi yoyote mahali popote ili mradi aweze kujikimu na kusaidia wadogo zake. Mungu akubariki sana.!

104162665_3081604538597884_8883253087067861292_o.jpg
 
Back
Top Bottom