Huyu anaomba kazi ya kuua CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu anaomba kazi ya kuua CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Dec 3, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  EMMANUEL Martine anachumbia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anataka kimpe fedha ili akisaidie “kudhibiti vijana waliokinyima kura” katika uchaguzi uliopita.
  Mradi wa kijana huyu anayejiita “mwanachama mwaminifu” wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), unalenga kuvamia vyuo vikuu nchini ambako anadai CHADEMA imejenga ngome.
  Katika andishi lake alilolipa kichwa cha maneno “Waraka wa Siri,” anasema CHADEMA ina mkakati madhubuti kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, hivyo anataka CCM imwezeshe kuudhibiti.
  Anasema vijana wamekuwa mwiba mkali kwa chama na serikali, kwa sababu CHADEMA wamefanikiwa kupenyeza kile alichoita “sumu” vyuoni. Sasa anataka CCM imwezeshe aondoe sumu hiyo.
  Andishi hilo la Martine linaonekana kuwa limewasilishwa kwa viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), idara ya usalama wa taifa, makamu mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UV-CCM), Beno Malisa na mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete.
  Martine anajitambulisha kuwa ni kiongozi wa jukwaa la vijana la taifa, mratibu wa shughuli za vijana wa CHADEMA, makamu mwenyekiti wa vyuo vikuu nchini na mwanzilishi wa alichoita “CHADEMA University Network” – mtandao wa CHADEMA Vyuo Vikuu.
  Anasema serikali imekuwa ikikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vijana kutokana na Umoja wa Vijana (UV-CCM) kushindwa kufanya kazi zake.
  “Umoja wa vijana wa CCM umeshindwa kutimiza wajibu wake,” anaeleza kwa nia ya kushawishi ufadhili.
  Pamoja na kuomba ufadhili CCM, Martine analalamika kwamba baadhi ya vijana wa chama hicho “wameachwa solemba” pamoja na kujitolea kwa hali na mali katika kampeni za kumwingiza madarakani Rais Kikwete.
  Anawataja baadhi ya wanafunzi walioachwa solemba kuwa ni pamoja na Mnanyi kutoka chuo kikuu cha Dodoma, Alex kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Luhajo kutoka Mbeya. Anawataja kwa jina mojamoja.
  Aidha, Martine anamwagia sifa Kingunge Ngombale –Mwiru na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa kwa alichoita jitihada zao katika mkutano wa vijana uliofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.
  Hata hivyo, mwandishi wa waraka analaumu chama kujisahau. Anajitapa kwamba ni yeye aliyesaliti wanafunzi wa vyuo vikuu nchini waliokuwa wanadai haki zao za msingi.
  “Hapo ndipo tulipounda jukwaa la vijana ambalo leo hii limekuwa kama kinga na ngao ya CHADEMA kwa kuweka vijana wasiopungua 35 katika halmashauri na wabunge sita,” anaeleza Martine.
  Anasema baada ya uchaguzi mwelekeo wa chama umekuwa mgumu; hakuna namna yoyote ya kukabiliana na hali hiyo wakati UV-CCM imejiweka kando.
  Kuhusu mipango ya CHADEMA, Martine anasema chama hicho kimeunda kamati tatu ambazo zitafanya kazi ya kuhakikisha vijana wote walioingia vyuo vikuu nchini wanakuwa wafuasi wake.
  Katika kampeni hiyo anataja wanachama na viongozi kadhaa wa chama hicho kuwa wanahusika katika utekelezaji wake.
  Kwa mfano, katika mkoa wa Dar es Salaam anawataja mbunge wa viti maalum, Suzan Lyimo, mbunge wa Kawe, Halima Mdee, mbunge wa Ubungo, John Mnyika, Barton Gwakisa, Innocent Ngowi na Sauda Hemed.
  Katika mkoa wa Dodoma anawataja Mtui, Mchange, Baraka, Hango mwenyekiti aliyemaliza muda wake (hataji majina ya pili), mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na mbunge wa Singida Mashariki Tindu Lissu.
  Mkoani Mwanza, Martine anawataja waliomo katika mpango wa kuingiza wanafunzi wa vyuo vikuu katika CHADEMA kuwa ni mbunge wa Nyamagana, Ezikea Wenje, Hawa Abdallah na Mussa Nyalagwinda.
  Naye, mbunge wa viti maalum wa chama hicho, Lucy Owenya, Anderson Rwela anayemtaja kuwa ni katibu wa ushirika wa CHADEMA na mwanachama wa chama hicho aliyemtaja kwa jina moja la Kimemeta, ndio waliopangwa kufanya kazi mkoani Kilimanjaro.
  Mkoani Mbeya, wanaotajwa ni mwenyekiti wa chama hicho, Shambwe Shitambala, mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na mwenzake wa Mbozi Magharibi, David Silinde.
  Anasema nyuma ya mipango hii ya kukuza uelewa wa jamii, kuna nguvu ya wafanyabiashara na baadhi ya wakuu wa shule.
  Kwa mujibu wa mwandishi wa waraka, viongozi wa serikali za wanachuo wamepokea utaratibu wa CHADEMA kupitia Profesa Mwesiga Baregu na Dk. Kitila Mkumbo.
  Bali MwanaHALISI lilipowasiliana na Profesa Baregu na Dk. Mkumbo, walikana madai hayo wakisema, “hayana ukweli na yametolewa na mtu mwenye njaa.”
  “Namfahamu mwandishi wa waraka huo ambao nami nimeupata. Ni kijana mmoja ambaye hana kazi na ameandika hayo ili kuweza kujikimu kimaisha,” amesema Profesa Baregu.
  Martine anaandika kuwa kwa sasa, hakuna vijana ambao tayari wameandaliwa kugombea nafasi za uongozi katika vyuo vikuu nchini.
  Hata hivyo, mwandishi anasema, “ …jambo la kutia moyo wengine nimewaweka mimi madarakani kwa msaada wa Ridhiwani.”
  Martine anasema utekelezaji wa anachoomba ni mgumu na wa “hatari.” Bali anatoa pongezi kwa baadhi ya viongozi wa UV-CCM akiwemo Ridhiwani, Aggrey Marealle na makamu mwenyekiti taifa, Beno Malissa kwa msaada wao kwake.
  Wengine wanaomwagiwa sifa, ni Kingunge Ngombale–Mwiru anayesema amekuwa wa msaada mkubwa kwake hata kumfanya arudishe matumaini ya “…kumsaidia Rais Jakaya kikwete…”
  Mwandishi anadai lengo lake la sasa ni kukisaidia chama chake ambamo amekulia.
  Kuhusu mtandao wa shule, mwandishi huyo anadai kuwa CHADEMA kinatengeneza mtandao wa shule zote nchini. Hataji kazi ya mtandao anaodai kuwa CHADEMA wataunda.
  Bali anasema, kazi hiyo itaanzia mkoa wa Kilimanjaro na kuenezwa katika mikoa ya Mwanza na Kagera.
  Anatoa ushauri kwamba ni vema CCM kikawa makini kutokana na vijana hao kuwa ndio mtaji unaogeuka kuwa mwiba kwa CHADEMA katika siku zijazo.
  “Kwa kuwa mpango wote tunao na kwa kuwa kila siku mipango ya chama huenda na utekelezaji, nawaombeni sana kuanza kufanya kazi katika vyuo vyote na shule ili kuwe na ripoti ya wapi tumetoka na wapi tunakwenda,” anaeleza.
  “Shukurani za dhati ziende kwa makada wa Moshi na Hai waliojitahidi sana kutimiza wajibu wao, ila ugumu na makovu bado yako palepale,” anasema.
  Martine anasema, “Sasa ni wakati wa kuamka…ni kama mfumo wa kijasusi…hii iwe wakati vyuo vinafunguliwa na katika mahafali. Nalazimika kufanya hivyo ili CHADEMA wasije nitoa roho.”


  Source Mwanahalisi wiki jana


  My Comment hivi kuna watu bado wana ndoto za mchana siyo? Wanadhani Chadema ni sawa na CCM? Wanadhani Chadema chama sawa na CUF au NCCR au TLP?

  Hiki ndio chama pekee CCM wamejaribu kukitikisa bila mafanikio. Wampe dogo pesa akatumbue. Vya wajinga uliwa na wajanja!
   
 2. WA MAMNDENII

  WA MAMNDENII JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Thread kama imenichanganya sijaielewa kiviile
   
 3. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Thread haieleweki kwa kwa sababu mbili,
  moja ,kuna uwezekano hii habari imechakachuliwa yaani mtoa thread amesoma habari na kuamua kuijadili kwenye thread yake AU pili hii habari imetoka Mwanahalisi bila kufanyiwa uhariri
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mwanahalisi nao wamezidi!
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hujaelewa nini?
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mie nimetoa comments zangu kama nilivyoisoma toka Mwanahalisi. Habari hii haijachakachuliwa. Nenda mtandao wa Mwanahalisi usome mwenyewe. Nyie ni wavivu wa kusoma online.
   
 7. B

  Bull JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kawaida yenu chama cha mtandao, mnataka mounewe huruma !!!
   
 8. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  What Do U mean????
   
 9. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jitu linaloamini kinachoandikwa na MwanaHalisi anahitaji msaada wa maombi!
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wamezidi kupita mpaka, yaani we acha tu
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sawa na nyie chama cha kuchakachua matokeo, hamkosi kuiba na kulialia kuhusu udini wakati nyie ni wadini namba moja
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  We endelea kusoma Uhuru, habari leo, na daily news au soma magazeti ya RA maana hayo ndio saizi yenu. Hayanunuliki na Mwanahalisi hulikuti kwenye vibanda vya magazeti.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nenda mahakamani!
   
 14. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  The guy is dreaming, eti kuisambaratisha CDM? ataanzia wapi? all varsities wanasupport CDM, their policies
  are clear, constructive & implementable, huu uchizi huu
   
 15. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,279
  Trophy Points: 280
   
Loading...