Huyu abiria lazima katumwa kuvuruga biashara ya kampuni hii

Abiria kama wewe ndio mliojaa kwenye haya mabasi yanayowachinja kama kuku.... basi linaburuzwa mmenyamaza tu mnataka kufika haraka, na akitokea mmoja au wawili wenye akili kama huyo unaemlaumu mnamuona mnoko kumbe ni mtu anaejitambua na kujali uhai wake

Sio kujidai mna haraka sana na mkipata ajali ndio wa kwanza kusema dereva alikuwa anakimbia sana...tukipata abiria kama hao at least mmoja tu ajali zitapungua ukiwa na haraka panda ndege mabasi ni usafiri wa taratibu.
 
Gari inayotoka Dar saa 12 asubuhi ikafika Mwanza saa 2 usiku haiwezi kuwa imeenda mwendo wa kawaida kaka. Hiyo yako iliyofika saa 6 usiku ndio ilienda mwendo wa kawaida.
 
Ila kama mngepata ajali watu wangekufa na wengine kujeruhiwa na kwa bahati nzuri ukanusurika ndio ungekuwa wa kwanza kusema kuwa basi lilikuwa mwendo kasi na matrafic hawafanyi kazi yao yaani povu lote linakutoka kwa sababu ya hela ya gest
 
Gari inayotoka Dar saa 12 asubuhi ikafika Mwanza saa 2 usiku haiwezi kuwa imeenda mwendo wa kawaida kaka. Hiyo yako iliyofika saa 6 usiku ndio ilienda mwendo wa kawaida.

Nimekuelewa mkuu. itabidi safari za usiku zihalalishwe walikosea kupiga marufuku
 
Duh! sawa ndugu, naona siku hizi Dar to arusha itakuwa mwendo wa saa sita au saa nane usiku., na vipi ile sheria ya kutotembea usiku kwa mabasi siku hizi imefutwa?

Weye ndo ulitakiwa umripoti kuwa anaendesha basi lenye abiria ndani saa 5 usiku. Ulitakiwa umwombe huyo mwenye namba za SUMATRA mpige simu huko ili mkamatwe tena dereva aswekwe ndani mlalie Shinyanga.
Siku utakapojikuta umelazwa chali na ma dripu ndo utajua kuwa Mwendo kasi ni hatari kuliko danger. Hili ungeliandikaje??
 
Weye ndo ulitakiwa umripoti kuwa anaendesha basi lenye abiria ndani saa 5 usiku. Ulitakiwa umwombe huyo mwenye namba za SUMATRA mpige simu huko ili mkamatwe tena dereva aswekwe ndani mlalie Shinyanga.
Siku utakapojikuta umelazwa chali na ma dripu ndo utajua kuwa Mwendo kasi ni hatari kuliko danger. Hili ungeliandikaje??

Mbona mnahamisha hoja? ishu ni pale watu wanapodai eti kusafiri usiku ni salama wakati ni hatari zaidi
 
OStory hii ina mahoha (comedy) zake kidogo. Dereva anapo amua kutembea speed 50/60 anamkomoa nani?! Au yeye alikuwa ametangulia kwa basi jingine na kwa remote akawa anaongoza hili lililokamatwa?!

Narudi kwenye mada.
Mkuu poleni sana kwa yaliyowasibu. Yamkini abiria huyo alipiga simu hiyo kwa nia njema sana. Tumezoea kupiga mayowe na malalamiko lukuki baada ya watu kufanywa vilema, kufa n.k Elimu ya uraia ya huyo abiria iwe sehemu sasa ya kuendelea kuwaamsha watanzania wengine wenye kuamini kufika salama na hatimaye kufika vibudu.

Tanzania ya sasa tunataka mabasi yanayofikisha, ndugu na jamaa zetu salama, na kuwatunuku vyeti madereva wote ambao hawaku sababisha ajali kwa mwaka mzima. Tunawahi wapi wakati nchi hii imeshawahiwa na wajanja?! Ningewaona wa maana sana kama mngekuwa mnawahi kwenda kuhamasisha watanzania wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la mpiga kura. Tafakari...
 
Si bure unalaana wewe, hv hujui mwendo kasi unaua? et mabasi ya mwanza mengine yalifika saa 2 hujui hayo mabasi yaliendeshwa kwa spidi kubwa sana? kwa taarifa yako kutoka Ukitoka Saa 12 ASBH DAR TO MOR UNAFIKA SAA 4, MORO TO DOM Utafika Saa Nane, DOM TO SING Utafika Saa Kumi SING TO IGUNG Saa Kumi Na Mbilh INGUNG TO NZEG Saa Mbili Hadi Tatu Usiku NA NZEG TO MWANZ Utafika Saa Sita Usk.LAKINI SIYO CHINI YA SAA SITA.

SASA WEWE UNASEMA MAGARI MENGINE YALIINGIA MWANZA SAA MBILI USK WAKATI MUDA HUO YALITAKIWA YAWE YAMEINGIA NZEGA!! UMEONA JINSI MWENDO ULIVYOKUWA MKALI? Omba Radhi Kwa Upuuzi Wako Na Umuombe Radhi Aliyepiga Sm Sumatra Tena Umshukuru Kwa Kuwaokoa Kenge Wee.
 
Kweli wasafiri mna matatizo ya kuchangia hizi ajali, unashabikia mwendo kasi eti umechelewa kufika Mwanza saa 2 wakati ilikuwa ukitaka kwenda Mwanza unapita kenya na inawachukua siku mbili kufika leo umesahau!
 
Tatizo habari wengine wanashangalia mwendo kasi
Tena naomba abiria wote tuige mfano kama wa hy jamaa aliyetoa taarifa SUMATRA
 
Ulitaka uwahi kufika ee, usalama kwanza mkuu, asikuambie mtu, ila hapo dereva alishindwa kutumia busara, aliamua kukomoa, kwann asingerud na kutembea na 80kph? Madereva wetu ujinga wao ndo huo wakielekezwa wanakasirika, na abiria wengi hawana akili, huyo mwenzenu alisimamia usalama wenu
 
Back
Top Bottom