Huyo msuluhishi anaetafutwa wa mpaka wa tz na malawi akishauri mpaka uwe ufukweni je?

SUMLEY

Member
Mar 11, 2011
90
121
Nimeisikiliza hotuba ya rais wetu Mh.Jakaya M Kikwete, amejitahidi kutuelezea vizuri tatizo lililopo na lilipotokea. Ktk maelezo yake amesema tume ya pamoja ya TZ na Malawi ilishindwa kuafikiana kutokana na TZ kusisitiza mpaka uwe katikati ya Ziwa wakati wenzetu wa Malawi walisisitiza mpaka uwe ufukweni mwa TZ. Kutokana na kutofikia muafaka, wakaadhimia kutafuta msuluhishi mwingine tofauti atakaesuluhisha swala hilo.

Sasa kwa mtazamo wangu, kama kweli tumeafiki atafutwe msuluhishi, maana yake tuwe tayari kwa usuluhishi atakaoutoa au kwa namna nyingine ushauri wake utazingatiwa. Je akishauri au akisema anaona ni vema mpaka uwe ufukweni (mbaba bay) kama wanavyotaka Malawi tutakua tayari kukubaliana na maamuzi hayo? Kama hatuko tayari kukubaliana na maamuzi tofauti na mpaka kuwa katikati ya ziwa basi haina haja ya kutafuta msuluhishi.
 
Back
Top Bottom