Huwezi na Hutoweza Kuongea / Kuandika Kiswahili fasaha

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,130
107,629
Kiswahili ni lugha ambayo imetokana na Kiarabu na Kibantu na maneno mengine machache yaliongezeka kidogo kidogo kutoka lugha zingine za Afrika, Uropa na Asia.

Kabla ya kuja wakoloni wa ki Uropa maandishi yote ya Kiswahili yalikuwa kwa herufi za Kiarabu na matamshi yalikuwa kwa lafdhi ya Kiarabu.

Nadiriki kusema leo hii, ili uongee na kuandika Kiswahili fasaha inabidi ujuwe Kiarabu. Bila hivyo utaboronga tu.

Na kama huna ustaarabu basi Kiswahili chako hakitakuwa fasaha.

Je, unajuwa maana ya "ustaarabu"?
 
na ww mwenyewe hapo umeandika kiswahili umeboronga. lugha yetu ni nzr lkn sisi wenyewe wenye lugha iyo hatuna muda wa kujifunza, tunaboronga tu,na hata lugha za wageni mfano kingereza tunachokitaka nacho tunaboronga. ni muhmu kuwa karibu na BAKITA ili 2jifunze maneno mengi ya kiswahili.
 
FaizaFoxy, miongoni mwa maprofesa nguli wa Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pengine ni wawili tu ninaowafahamu ambao wanafahamu Kiarabu cha kubabia: M. Mulokozi na Abduli Hamisi Mtajuka... Wengine wote wamesoma tu mahusiano kati ya lugha hizi mbili.

Ziada ni kuwa, zipo lahaja za Kiswahili ambazo hazina maingiliano kabisa na Kiarabu, kama vile Kimakunduchi na Kingwana kinachosemwa Kongo Mashariki.

Uhusiano wa kulazimisha kati ya Kiarabu na Kibantu unapingwa kwa kuwa sio Waarabu wote wanaweza kusikia walau msamiati mdogo wa Kiswahili, na kinyume chake vivyo hivyo.

NB: Kiswahili ni Kibantu hasaa!
 
Last edited by a moderator:

Nisome tena post namba moja halafu nieleze unachokipinga ni nini?

Halafu hayo maneno niliyowawekea nyekundu yanakueleza nini?
 
Kiswahili ni lugha ambayo imetokana na Kiarabu na Kibantu na maneno mengine machache yaliongezeka kidogo kidogo kutoka lugha zingine za Afrika, Uropa na Asia.

Kabla ya kuja wakoloni wa ki Uropa maandishi yote ya Kiswahili yalikuwa kwa herufi za Kiarabu na matamshi yalikuwa kwa lafdhi ya Kiarabu.

Nnadiriki kusema leo hii, ili uongee na kuandika Kiswahili fasaha inabidi ujuwe Kiarabu. Bila hivyo utaboronga tu.

Na kama huna ustaarabu basi Kiswahili chako hakitakuwa fasaha.

Jee, unajuwa maana ya "ustaarabu"?

Yafanyie kazi hayo maneno niliyo yakoleza wino wa rangi ya bluu, kisha ndipo urudi hapa jukwaani. Kwani ustaarabu umekushinda na wewe pia.
 
Ambatanisho la konsonanti ya kiyeyusho (kama 'w' na 'y' kwenye irabu za mwisho ni athari ya Lugha ya Kiarabu kwenye Kiswahili na huonekana sana kwenye usemaji wa Unguja, Mombasa na maeneo mengi ambayo wakaaji wake ni mchanganyiko na bani Arabia.

Mfano: 'mwenziye' badala ya mwenzie,
 
Nisome tena post namba moja halafu nieleze unachokipinga ni nini?

Halafu hayo maneno niliyowawekea nyekundu yanakueleza nini?
Post namba moja hata nikiisoma tena bado wazo langu litabaki kuwa lile lile. Hapo ambapo mimi nimeweka nyekundu naona Kiswahili kinaanza kuwa Kiingereza sasa.
 
Yafanyie kazi hayo maneno niliyo yakoleza wino wa rangi ya bluu, kisha ndipo urudi hapa jukwaani. Kwani ustaarabu umekushinda na wewe pia.

Hiyo inayakinisha "point" yangu kuwa Huwezi na Hutoweza Kuongea / Kuandika Kiswahili fasaha, laiti tungekuwa wote tunayaandika maneno ya Kiswahili kwa Kiarabu wala kusingekuwa na utata, maneno hayo wala yasingeleta ubishi kabisa. Kwa sababu Kiarabu ni lugha yenye alama za matamshi kwenye "irabu" zake na haitegemei "vowels" za herufi pekee.

Tusingeweza kabisa kuandika "ntu" badala ya "mtu" au kinyume chake kama wengi watakamkavyo. Ingawa neno "ntu" ndiyo moyo wa Ubantu.
 
Hiyo inayakinisha "point" yangu kuwa Huwezi na Hutoweza Kuongea / Kuandika Kiswahili fasaha, laiti tungekuwa wote tunayaandika maneno ya Kiswahili kwa Kiarabu wala kusingekuwa na utata, maneno hayo wala yasingeleta ubishi kabisa. Kwa sababu Kiarabu ni lugha yenye alama za matamshi kwenye "irabu" zake na haitegemei "vowels" za herufi pekee.

Tusingeweza kabisa kuandika "ntu" badala ya "mtu" au kinyume chake kama wengi watakamkavyo. Inagwa neno "ntu" ndiyo moyo wa Ubantu.
WAsanifishaji wa Kwanza wangezingatia usemaji huu kuwa ndio msingi wa Kiswahili, leo hii tuhuma zingekuwa kuwa Kiswahili ni Kimakonde
 
Post namba moja hata nikiisoma tena bado wazo langu litabaki kuwa lile lile. Hapo ambapo mimi nimeweka nyekundu naona Kiswahili kinaanza kuwa Kiingereza sasa.

Ukinisoma post namba moja hata hii ya Kiswahili kuwa na maneno ya Kingereza utaikuta, au Kingereza si Kiuropa?.

Mpaka sasa sijakuelewa unachokipinga au kukikataa ni nini haswa.
 
Ooh!

Hata mimi sielewi unachokihubiri hapa nini nini, ila najua ni urongo!
 
Kwanza hapa sina nnacho "kihubiri", hapa nnaandika kuwapa watu faida ya kuwa na mawazo mapana zaidi. Si wale ambao wamefikia upeo wao usiozidi urefu wa pua zao, wasioelewa wanachokipinga ni nini, wewe ni mmojawao.

Kama hukielewi umejuwaje kama ni "urongo"?

Na huo "urongo" uko wapi?
 
Kiswahili ni lugha ambayo imetokana na Kiarabu na Kibantu na maneno mengine machache yaliongezeka kidogo kidogo kutoka lugha zingine za Afrika, Uropa na Asia.

Kabla ya kuja wakoloni wa ki Uropa maandishi yote ya Kiswahili yalikuwa kwa herufi za Kiarabu na matamshi yalikuwa kwa lafdhi ya Kiarabu.

Nnadiriki kusema leo hii, ili uongee na kuandika Kiswahili fasaha inabidi ujuwe Kiarabu. Bila hivyo utaboronga tu.

Na kama huna ustaarabu basi Kiswahili chako hakitakuwa fasaha.

Jee, unajuwa maana ya "ustaarabu"?

Swali dogo, Je, Kiswahili ni Kiarabu? Kuna uhusiano gani kati ya Kiswahili na Kiarabu ukiacha maneno ya kuazima?
 
Soma post namba moja.

Tatizo ni kwamba sielewi hoja yako hasa ni ipi! Unaposema ili uweze kuongea Kiswahili fasaha ni lazima ujue kiarabu unamaanisha nini haswa?
Je, unamaanisha kwamba Kiswahili na Kiarabu vina uhusiano zaidi ya kuazimana meneno? Hebu fafanua hapo kama ukiweza kwa maana kuna upotoshaji mkubwa sana kuhusu hii lugha ya Kiswahili jambo linalofanya Waafrika wengi hasa Watz kukichukia ( kwa kutokuelewa kwamba wanachukia lugha yao wenyewe ) kwa sababu wanaamini kwamba Kiswahili ni Kiarabu au Kiswahili kimetokana na Kiarabu wakati SIYO KWELI!
Kiswahili hakina uhusiano wowote ule na Kiarabu isipokuwa maneno ya kuazima ya Kiarabu, jambo ambalo ni la kawaida kwa lugha zote hapa Duniani! Ndio maana ningependa ufafanue zaidi kama ukipenda ili huu mjadala uwe mpana na kufungua macho wengi hapa!
 
Kiswahili kabla ya kuja maandiko ya Kilatini kikiandikwa kwa herufi zipi?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom