FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,881
- 109,191
- Thread starter
- #121
Faida gani tutapata tukitumia hizo herufi za kiarabu?
Post yangu namba 50 ina majibu ya hilo, ngoja nikuwekee tena hapa uisome:
Umenielewa kabisa point yangu na mpaka hapo juu nimeweka mfano wa Wazungu Waalimu wa awali wa Kiswahili wa vyuo vikuu huko nje walivyoona huo umuhimu wakujifunza Kiswahili kwa kujuwa maandiko na matamshi ya Kiarabu, sijuwi hawa ndugu zangu ambao hawalioni hilo na wanalipinga wanapinga nini haswa?
Mimi kuileta hii mada nna maana yangu pana sana, ni juzi juzi tumesikia kuwa Tanzania imetowa maamuzi kuwa lugha ya kufundishia masomo yote iwe Kiswahili. Ni jambo jema sana hilo. Ni wakati muafaka tukatambuwa kuwa inabidi na watu wafundishe kukijuwa Kiswahili fasaha kwa matamshi ya Kiarabu ili wawe na ufasaha na kina cha kuelewa maana ya maneno mengi ya Kiarabu yaliyomo kwenye Kiswahili.
Itakuwa ni rahisi sana kwa mwanafunzi kuwa na ufasaha wa hali ya juu na au Mwalimu atakuwa na kina cha kufundisha ikiwa tu atakielewa Kiswahili kwa herufi za Kiarabu kuliko yule ambae atabaki na kukielewa kwa herufi za Kilatini tu.
Leo hii utashangaa mtu anakuja na jina la kiajabu ajabu la kutunga hata halina kina wala halina uhusiano wowote na ubaridi wala historia eti "jokofu", wakati neno hilohilo kwa Kiswahili fasaha lipo "barada", ambalo lina historia, lina kina na lina uhusiano na ubaridi.
Nnawashauri Waalimu wa Kiswahili, wa kuanzia shule za msingi mpaka juu kabisa huko, waanze kujifundisha herufi za Kiarabu na waone wakisha zijuwa kuandika na kuzisoma herufi hizo watavyoona raha kufundisha Kiswahili kwa ufasaha na kina zaidi.
Fikiri.