Uchaguzi 2020 Huwezi kuwatishia wananchi ambao hawana cha kupoteza

Feb 18, 2019
50
532
Baba yangu ni mkulima wa alizeti toka miaka ya 1980 kipindi ambacho hakukuwa na barabara za lami kabisa. Toka miaka hiyo kipindi hamna lami mpaka sasa pana lami maisha yake hayana tofauti sana katika kuuza mazao yake.

Hakuna mwaka hajawahi kukosa kuuza mazao yake kisa ubovu wa barabara. Wala hamna mwaka mazal yake yamepanda bei eti kisa kuna barabara ya lami.

Kifupi haya mambo ya mindombinu yanawapa ahueni wafanyabiashara tuu. Sisi wakulima wala hayana mantiki sana sababu hayana effects kwetu.

Sasa anapokuja mgombea anatuambia eti tumchague ili atuletee lami hatumuelewi kabisa. Mambo ya lami na mandege akayaongelee mjini huko lakini sio huku vijijini ambako tumevuna mazao yetu tumeweka stoo, hatuna njaa.

Ninachomkubali Lissu anajua kufanya situation analysis kabla hajazungumza kwenye kampeni zake. Yani akianza kuelezea Uhuru,Haki &Maendeleo basi anaelezea kwa kureletisha na maisha yenu halisi ya eneo lenu mnaloishi.

Sasa wewe unaomba kura Geita ndanindani kwa kuwaahidi kununua ndege zaidi kweli? Ndege zitawasaidia nini wao? Thats not their immediate nor long term need.

Wagombea muwe mnaielewa hadhira mnayozungumza nayo kabla hamjaanza kuongea, mnatia huruma sana.
 
Mkuu, hao huwa tunawaita vichwa maji. Wanajiondoa ufahamu kuhusiana na adha na shida halisi za wananchi na kuishia kujificha ktk kutoa takwimu zisizo hata aminika.

Mathalani, badala ya kuongelea ubora wa huduma za afya na elimu itolewayo kwa ngazi ya msingi, wao wanatuambia idadi ya vituo vya afya na idadi ya ongezeko la wanafunzi. Nani asiyetambua fedha kiduchu za bajeti zitolewazo ambazo haziendani na mahitaji halisi na ubora wa huduma zenewe.

Wakati umefika wa akili kubwa kutawala nchi hii. Hawa watu waliozoea kuishi kwa mazoea ni lazima wapumzishwe kupitia uchaguzi wa mwaka huu.
 
Mkuu, hao huwa tunawaita vichwa maji. Wanajiondoa ufahamu kuhusiana na adha na shida halisi za wananchi na kuishia kujificha ktk kutoa takwimu zisizo hata aminika...
Wamejenga vituo vya afya vilivyojaa vumbi na buibui, havitumiki coz hawajaajiri coz wanajenga SGR, Ndege, bwawa, ujinga mtupu.

Tuna shida lukuki katika primary level, afya, elimu, ajira hakuna, mishahara haipandi.

Leo anawafanya watu wajinga anatangaza ajira 10,000 za walimu wakati wa kampeni..
Mambo ya kizamani!
Eti anampigia simu Mfugale&co wajenge barabara! Ovyo kabisa.
CCM wamechemka sana!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Tunataka mtu atakaeonea uchungu kodi zetu
Exactly na sie anayebagua kwa kupeleka maendeleo wakati kila mwananchi analipa kodi.
"Mkichagua upinzani siwajengei barabara"
"Nendeni mkamuulize mbunge wenu, si mlichagua mpinzani nyie?"
"Sipangiwi, na ukijifanya unanishauri uwii ndo sifanyi kabisaa"
Ni chache kama kuna zingine mwaweza mwaweza ongezea kauli zakibaguzi, zilizojaa jeuri na kibaguzi
 
Thanks to globalization. Hata waliokuwa vijijini wengi wana smartphones wanafuatilia kila kitu. Hata haya tunayoyanena hapa wanayasoma na kuyaelewa.
Akili kubwa daima hudumu.
Magu na genge lake, wamekuwa wanasimama majukwaani miaka mi5, famous slogan,
#tunamshukuru mheshimiwa raisi Dr JPM kutupatia billions,

Bashite was a bad influence.
Wamekwapua pesa halali za watu wa kawaida, hard earned cash, wakiwaita wapiga dili, wamewanyang'anya, wamewabambikia kesi, haya ndiyo matokeo!

Wamefilisi watu. Ili wajifananishe na Nyerere, mambo ambayo hata Nyerere aliyajutia baadaye!

Hata akirudi madarakani ametambua kumbe na hata wananchi nao walikuwa wanamtizama tuu na kusema, ihiiiiiiiiiii!

Vitambulisho vya machinga siyo lazima, ni kwaajili wamachinga wasisumbuliwe na nani??
Hoja ingekuwa kwa ajili ya machinga wawekewe miundo mbinu bora yakufanyia kazi, au hiyo hela iwe kwa ajili ya kulipia wafanya usafi katika mazingira yao ya biashara!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Bwana yule yuko hoi hapa Dodoma. Anachokiona kwa sasa hakukitarajia.
Amekonda, amepauka, amechoka na kuchakaa.
Amekosa raha kwani watanzania hawayataki mandege yake, mafly over na hata madaraja yake ya Busisi- Kigongo.
Wanachohitaji ni unafuu wa maisha ya kila siku ambapo ni mgombea wa CHADEMA pekee ndiye kawaahidi kutekeleza matakwa yao.

Udhalimu wa Meko ndio unamgharimu sasa.
Busisi Kigongo unajenga daraja la nini wakati unatengeneza vivuko vipya??

Rome was not built in a day, kwa sababu hashauriki haya yote anataka afanye yeye, ajenge LEGACY BINAFSI, huku akiwaumiza watu wengi wa kawaida, atakuja kushukuriwa na vitukuu huko akiwa kiranja wa malaika, lakini generations ya sasa, itamlaumu kwa huu ugumu wa maisha!

Everyday is Saturday......................... :cool:
 
Bwana yule yuko hoi hapa Dodoma. Anachokiona kwa sasa hakukitarajia.
Amekonda, amepauka, amechoka na kuchakaa.
Amekosa raha kwani watanzania hawayataki mandege yake, mafly over na hata madaraja yake ya Busisi- Kigongo.
Wanachohitaji ni unafuu wa maisha ya kila siku ambapo ni mgombea wa CHADEMA pekee ndiye kawaahidi kutekeleza matakwa yao.

Udhalimu wa Meko ndio unamgharimu sasa.

Mjinga sana yule baba. Yeye ana agenda yake na watanzania wana agenda tofauti kbs. Kwa miaka mi5 kodi zetu zimetumika kuridhisha ego ya mtu mmoja tu kweli bila huruma. Anahotaja yeye ndiyo kinapaswa kufanyika hata kama hakijibu matakwa ya watanzania kwani Tz ni yake peke yake? Hii ni NONSENSE and it must stop.
 
Tatizo jiwe haambiliki Alafu anaendesha nchi ki Familia Sana nani alikua anajua mwenye funguo za hazina ni mtoto wa dadake?
Nani alikua anajua amejibinafsishia hekta 25000?
Nani alikua anajua mayanga construction ambayo inapewa tenda za ukandaras nchi nzma bila zabuni ni ya mume mwenza wa Pombe
Tumechoka kutawaliwa kidikteta na Familia moja
We can't breathe
Ukiona kiongozi anabana Sana media ujue anamaovu mengi hataki yajulikani

Mungu wangu raisi wa wanyonge kapora hekta 25,000 za wanyonge wake ziko wapi hizi mkuu? Anataka kuzifanyia nini mitamaa ya kijinga hii jamani? Hiyo pesa yote aliyokusanya na mihekta yote hiyo ya nini?
 
Zipo kule karagwe kekta 25000 zinalindwa na JWTZ
Wewe hujiulizi kwa nini mkuu wa majeshi,, wakuu wa usalama wa taifa, ni watu wa Familia yake
Mwenye dhamana ya pesa zote za Tanzania ni mtoto wa Dadake
Ile ardhi nasikia ameanza kujenga nyumba nyingi kama zile za Sadam husein wa Iraq
Nyumba ambazo zinafanana halafu chini kwa chini kuwe kuna Barabara ili hata walinzi wasijue kalala wapi
Huyu mtu kwa ukatili aliofanya anahofu Sana
Ukiona kiongozi anabana media ujue kuna mambo maovu mengi hataki watu wajue
 
JPM ananadi sera wakati Lissu analalamika kapigwa risasi 16.sasa kupigwa kwake risasi 16 zinamuhusu nini mwananchi wa kijijini?
 
Zipo kule karagwe kekta 25000 zinalindwa na JWTZ
Wewe hujiulizi kwa nini mkuu wa majeshi,, wakuu wa usalama wa taifa, ni watu wa Familia yake
Mwenye dhamana ya pesa zote za Tanzania ni mtoto wa Dadake
Ile ardhi nasikia ameanza kujenga nyumba nyingi kama zile za Sadam husein wa Iraq
Nyumba ambazo zinafanana halafu chini kwa chini kuwe kuna Barabara ili hata walinzi wasijue kalala wapi
Huyu mtu kwa ukatili aliofanya anahofu Sana
Ukiona kiongozi anabana media ujue kuna mambo maovu mengi hataki watu wajue

Inauma sana hii kitu mkuu. Mimi huwa ninajiuliza kila siku kama kuna tofauti kati ya huyu baba na Mobotu Seseseko. Binafsi sioni tofauti na kama ipo tofauti basi ni unafiki hakuna kitu kingine. Ni unafiki uliopitiliza kujiita rais wa wanyonge halafu ukatumia 56 billion za wanyonge kujenga airport kwa ajili yako peke yako halafu kama haitoshi ukajimilikisha hekta 25,000 ambazo ni size ya Taifa moja huko ulaya.
 
Ni kweli yeye anataka awe Rais wa wanyonge
Maana ya wanyonge ni watu mfukara kupindukia ki hali na Mali
Mnyonge hata ukimkanyaga bahati mbaya hawezi kusema unanikanyaga
Na kweli kwa miaka mitano watanzania wamekua wanyonge Sana
Lakini lissu si mnyonge ni shujaa Sana
Let's wait and see
 
Back
Top Bottom