Kinachofanywa na serikali ni kukomoa watumishi hasa waliokuwa wanufaika wa bodi ya mikopo bila kujali kuwa ni watumishi hawa hawa inaowategemea kuleta ufanisi kazini, sikujua kuna umuhimu gani ulikuwepo wa serikali kuongeza makato toka 8%-15% na makato hayo kuanza mara moja bila kujali kuwa watumishi hao walikuwa na mikopo toka taasisi nyingine na serikali haijaongeza mishahara.
Leo hii mtumishi anaepokea 180000/= hawezi kufanya kazi ufanisi kwa sababu ya hali ngumu inayomkabili yeye na familia yake, ikumbukwe gharama za maisha zimepanda, ikiwemo bei ya vyakula lakini tujiulize kama sio kuwakomoa watumishi mbona suala hili halikusubiri uhakiki uishe kama walivyosema kwenye nyongeza ya mishahara.
Viongozi wetu wakumbuke kuendesha nchi bila kukomoana, chuki na visasi kwa kundi lingine hata kama hawakuwachagua.