Huwezi kuwa na Akili timamu Ukawatetea hawa watu wawili. Si sawa hata kidogo

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,355
11,500
Mdude Chadema. Ni kijana ambaye ana ujasiri ambao kama ungetumika vizuri na akapata elimu nzuri akaelimika, akapata mshauri mzuri na akawa tayari kushauriwa angekuwa mtu mzuri sana mwenye uthubutu.

Alikosa malezi mazuri ukubwani au utotoni. Si kosa kukosoa, ila si aina ya ukosoaji wa matusi na dhihaka anaofanya Mdude. Chukulia tu anayekosolewa ni baba yako. Kwa aina ile ya ukosoaji, ni wazi kuwa alijipalia makaa kichwani mwake.

Sikubaliani na watu kutekwa au kuteswa. Naamini katika kufuata sheria hivyo wahusika wanaokosea wahukumiwe kwa mujibu wa sheria, si vinginevyo. Lakini pia wakosoaji ni lazima wajue katika kukosoa hupaswi kutweza utu watu, kumtusi, kumkashifu au kumwaibisha. Kosoa kwa nidhamu.

Wacheni Mdude Nyagali Chadema afikishwe katika vyombo vya sheria, sheria ikaamue hatma yake.

Bwana mdogo mwingine kwa ulimbukeni naye alirudia kosa ambalo linafanana na ambalo aliwahi kuonywa. Niseme tu wazi Idrisa mimi binafsi hajawahi kunichekesha na pengine hili ni tatizo langu si lake, maana kuna wengine anawachekesha.

Kitendo cha kuweka picha ya Mh. Rais pembeni ya video yake akicheka haikuwa sahihi. Kwa mtu mwenye akili timamu alipaswa atabiri matokeo yake maana huyu si mgeni nchi hii. Lakini alishindwa tabiri nini kingetokea na kuamua kuachana na hilo.

Kama Mh. Rais angekuwa baba yangu, mimi binafsi ninge-deal na Idris. Niseme tu kwa uwazi. Hii mitandao isitumike vibaya kuwa bully wengine sababu hawawezi fanya kama sisi.

That was cyber bullying. Mh. Rais angeweza naye kujibishana na Idris? No. Je, angekuwa mzazi wako wewe ungefanyaje?

Kwanini tusikosoe hoja na sera? Tusikosoe mawazo na matendo? Tunapokosoa personality kwa kudhalilisha tunakosea.

Hawa vijana wamejitakia hayo. Ndio maana hakuna anayehangaika nao sana sababu wamefanya mambo ya kipumbavu. Sisi watu wa Bara huwa hatuna utani wa kupitiliza, na wengi wanafahamu hilo wenye uelewa. Mambo mengine nyie wa pwani fanyianeni wenyewe kwa wenyewe. Achaneni na wabara.

Mtu wa pwani mwanaume anaweza shikwa makalio akacheka na kuambiwa mse**e wewe, au fala. Usifanye kosa hilo kwa Mjita, Msukuma, Mkurya, Mnyakyusa, Mhehe n.k hali yako itakuwa mbaya sana kiafya.

Tujifunze kukosoa kwa adabu, kwa kuheshimiana. Ukweli ni kwamba hata kama hupendi, Dr Magufuli ndiye Rais wa Tanzania. Hiyo will not change mpaka when changes happen.
 
Tatizo kubwa linaloambatana na vijana wanaharakati/wanasiasa kukosa nidhamu ni kukosekana kwa mifumo sahihi ya malezi ndani ya vyama vyao. Na hii ni kwa vyama vyote ikiwamo pia CCM ambayo hata katibu wake mkuu alikiri hilo kwenye msiba wa marehemu Mengi alipokuwa akimwombea msamaha Makonda.

Vijana hulelewa kwa misingi ya misimamo zaidi kuliko nidhamu kuelekea itikadi na sera za vyama vyao. Hiyo ndiyo sababu kwa mfano utaona wabunge wa Chadema wakiandika kauli ambazo hata mtoto mdogo anayejitambua hawezi kutamka mbele za watu. Lakini wao huona ni ushujaa kuziandika kwenye majukwaa kama twitter!

Ukirejea post za Halima Mdee twitter kuhusu hiyo picha ya TBT ya mh. Magu iliyomweka matatani Idris utaelewa ninachoongelea. Kuna siku kiongozi mmoja wa Chadema (wa kike) alimtaja ndugu mkuu wa mkoa (unaelewa namaanisha nani) kama mke mwenza wa Halima na akam-tag. Halima naye akaafiki kwa kujibu "namshangaa (huyu mke mwenza), si angenipigia tu simu!" Hapo walikuwa wakirejea kauli ya Makonda kuwa angewakamata uzururaji!

Sasa hao ni viongozi vijana tena wanawake na hawaoni aibu kabisa kujadili mambo hayo ya aibu mbele ya umma! Na hapo chini yake utakuta comments za viongozi wenzao!

Hilo la malezi unaweza kuliona pia kwa huyu bwana Mdude. Mimi ninamfahamu vema kwani tunatoka mtaa mmoja (Ichenjezya, Vwawa). Nimemfahamu enzi hizo akiwa mgeni katika siasa, mwaka 2008. Wakati huo alikuwa akifanya kazi ambayo siitaji hapa kama kejeli kwani ninaiheshimu bali naitaja ili vijana wa kimapokeo wasihadaike na maisha ya mtandaoni wakasahau asili zao. Alikuwa mhudumu/mfanya usafi wa choo cha stendi ya mabasi Vwawa.

Wakati huo kama ilivyo hilka yake ya utulivu, alikuwa mtulivu na mwenye busara. Hakuwa mtu wa kuropoka ovyo. Kuna wakati Dr. Slaa alibabaishwa na afya yake na ni yeye (Mdude) aliyetoa tiba ya asali. Lakini baada ya akina Slaa kutoswa na unadhimu kufa Chadema, kila mtu akawa kambale na anaongea anapojiskia anachojiskia.

Kwa kifupi mitandaoni sasa hivi ni ngumu kutofautisha baina ya kiongozi na mwanachama. Kazi kwenu wenyevyama.
 
Komeo Lachuma,

Mkuu tunakupongeza kwa bandiko hili refu lenye wingi wa busara. Je ww huwa huoni hao viongozi wakitumia madaraka yao vibaya kwa kunyanyasa wengine wenye mitazamo tofauti na wao? Huwa huoni wakinajisi chaguzi za nchi hii? Au kwakuwa una maslahi na madaraka yao, hivyo unaona ni sawa tu wafanyacho?
 
Sina maslahi. Ndo maana nikasema wakosolewe kwa busara. Siungi mkono kila jambo wafanyalo but tukosoe kwa busara.

Mkuu tunakupongeza kwa bandiko hili refu lenye wingi wa busara. Je ww huwa huoni hao viongozi wakitumia madaraka yao vibaya kwa kunyanyasa wengine wenye mitazamo tofauti na wao? Huwa huoni wakinajisi chaguzi za nchi hii? Au kwakuwa una maslahi na madaraka yao, hivyo unaona ni sawa tu wafanyacho?
 
Kwa kweli umenena vzr. Viongizi si malaika wanakosea mengi kama vile wazazi wetu waliotulea walivyokuwa wanakosea, je tulikuwa tunashughulika nao vipi?

Hata biblia kuna sehemu imesema watu wa namna hiyo kuwa

"Nimekabidhi shetani awafundishe" au leo msemo usemao "asiye funzwa na ***** hufunzwa na ulimwengu"

Chukulia kijana anamtukana mzazi wako japo mzazi ana makosa anamtukana matusi na dhihaka ungefanyaje? Sisi wa Bara nadili na wewe perpendicular at 90 degree ili kulinda heshima.

Lkn malezi dunia i.eharibika sana ukiona sisi wazazi labda tunashabikia mwanao kushinda shindano la kukaa uchi jua ipo shida japo atarudi na zawadi .

Kuna mambo nitakapokuwa rais wenu miaka ijayo hamtayasikia kwa mujibu wa tamaduni za kiafrika nitawaweka jela nami baada ya urais wangu mtanipeleka the heague nikafie huko kwangu ni ujasiri
 
Tanzanature,
Mkuu umesema vyama vyote kuna vijana hawana nidhamu, ila mifano yako zaidi ya miwili ni wanacdm tu, au ni mambo ya damu nzito kuliko maji? Mkuu hao viongozi unaoumia sana wakitukanwa, ndio wanaopanga na kusimamia chaguzi za nchi hii kunajisiwa na wote hilo tunalifahamu, lakini hili kwako sio tatizo, bali tatizo kwako ni pale wanapotukanwa tu! Sitaki kusema huu ni unafiki, ila ngoja nitafute kamusi nipate neno jingine zuri nje ya unafiki.
 
Back
Top Bottom