Huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia CCM

Mkuu;
Pamoja ni kweli kabisa ccm-regime si kwamba wanatakiwa kuondoka lakini kinachotakiwa ni kusambaratisha viongozi waliowahi kuongoza wasibadili vyama. Angalia Kenya mafisadi wa KANU leo ndo wanaongoza bado na ufisadi wa kasi zaidi unaendelea kwa mgongo wa PNU, sijui ODM.

Napingana na mawazo yako, mie nafikiri utakuwa na mawazo ya kidikteta kusema wanaojiunga ccm ni wehu, waache binadamu waamuwe watakayo hiyo ndo demokrasia. Si binadamu wote wanapenda maisha mazuri wengine wanafurahi zaidi wakiwa masikini, kuna wengine wanafurahi zaidi wakiwa kwenye vurumai kama somalia, kuna wengine wanafurahi wakiwa ktk amani, kuna wengine wanafurahi zaidi wakiwa malaya na kunawengine wanafurahi wakiwa watulivu nk.

Ninasochotaka kusema ni kuwa kujaribu ku-impose mawazo yako unayodhani ni mazuri kwa mtu unayedhani mawazo yake ni potofu ndo chazo cha udikteta, madkiteta huanza hivyo kwa kujaribu kui-impose mawazo yao mazuri juu yawengine. Na pia lazima utambue mawazo yako mazuri ndo mawazo mabaya kwa mwenzako.

Nitakupa mfano
Kuna jamii ulaya inaitwa Gypsy nafikiri utakuwa unaitambua, wao kufanya kazi ni mawazo potofu, kwao mawazo sahihi ni kuomba omba tu, wapo ulaya na kazi zinapatikana lakini kazi yao ni kuomba. Hapa nataka kusema, mwanadamu na kiongozi safi lazima uheshimu mawazo ya mwenzako.
Mawazo yako mazuri unaweza kuya negotiate na unayemwona anamawazo potofu, na sio kuya impose kwa vitisho, kejeli na matusi.

Well said Mkama!
if somebody is happy with the "scales(ze gambaz)" let him/her enjoy his/her constitutional right and support the "gambaz" also if somebody enjoys being in "ze gwandaz" attire, let him/enjoy his Constitutional right to be in ze gwanza! and maandamano! tuvumiliane tu ndiyo demokrasia hiyo!
 
Kundi la kwanza la wanaoshabikia CCM: ni wale wanaonufaika na mfumo huu wa kifisadi, Mafisadi hawajui shida zozote za nchi hii, umeme na maji majumbani kwao ni masaa 24, wanazo hela za kutosha, watoto wao wanasoma nchi za ulaya ili waje kuchukua uongozi wa nchi wao wakizeeka. Wengi wa watu katika kundi hili ni watendaji waandamizi wa chama na serikali ambao wanaona mfumo huu wa kuongoza serikali ukibadilika basi watapoteza mianya ya kuchota mapesa serikalini. Wana akili timamu na watahakikisha CCM inabakia madarakani kwa ghalama zozote ili wazidi kuneemeka zaidi na zaidi.

Kundi la Pili: Hili ni lile la watanzania maskini kabisa ambao wananufaika tu wakati wa kampeni, kundi hili ndilo linalotuangusha, wanapewa vijipesa kidogo wanachagua chama hiki - hawa si wajinga ila hawajui haki zao na nini wanafanya. wengi wao wako vijijini ambako elfu kumi ni kama million kumi.

Kwa hiyo ndugu zangu adui wa kwanza wa demokrasia ni umasikini, mtu anachagua chama na kukishabikia kwa sababu ya ujira mdogo, na kwa namna mfumo huu ulivyo na kwa njisi tulivyoutupa uzalendo basi sitashangaa CCM ikirudi tena madarakani ingawa wengi wetu HATUPENDI KABISA.
 
Kila mara huwa nawakumbusha watanzania wenzangu kwamba hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kushabikia kile CCM na serikali yake wanafanya. Ukiachilia mabali yaliyotokea Tarime ya kuua wananchi wanaoenda kudai mali yao inayo dhulumiwa na wezi wa kizungu na vibaraka wao ndani ya nchi.

Angalia wanavyo shughulikia suala la umeme. Kikwete mwaka 2006 alitamka kwa mdomo wake kwamba ndani ya miaka 3 chini ya utawala wake mgao wa umeme utakuwa historia, sasa na asimame na athibitishe usemi wake huo!!

Kiinimacho kingine ni upumbavu wanaoufanya juu ya mitambo ya Dowans. Wanapitia mlango wa nyuma kununua mitambo hiyo wakidhani hatujui, wadadisi wa mambo mkitafuta info kidogo mtajua hiyo kampuni ya Symbion imefikiaje uamuzi wa kujitwika Dowans na hapo mtagundua tu kwamba ni jamaa wanazunguka mbuyu.

Niseme tu kwamba kwa CCM na serikali zake walipo tufikisha, si tegemei kwamba kuna mtu ana akili timamu anaweza kujiunga na chama hiki ambacho ni cha kuangamiza wananchi na mali zao.
Mkuu kuna vigezo mbalimbali vya kuamua kushabikia kitu....unapima sifa zake... nzuri na mbaya.....kisha unaamua.... labda ingekuwa vyema ungewauliza wanashabikia kwa sifa ipi....
 
Kwa akili finyu ya mleta hoja angekuwa wa maana kama ange elezea na mambo mazuri ambayo CCM imefanya! Lakini kwa ushabiki mahaba wa kutumwa na Chama chake au kwa umbumbu wake ameonesha kuwa CCM haijafanya lolote! Ni ujuha wa ushabiki mahaba! Miaka ya 50 ya uhuru mafanikio tuna anza kulinganisha wapi? Nchi haikuwa hivi kama ilivyo maisha ya watanzania yamebadilika sana japokuwa maendeleo hayawezi kuwa timilifu kwa wakati mmoja! Acheni ushabiki mahaba sifieni na mambo ambayo CCM imefanya!
 
Hivi hawa watu cjui wametokea wapi,hivi hamuwaonei watz wenu huruma kwa umasikin uliokithiri?kwanin tunapenda kushabikia tu bila kuangalia mustakabali wa taifa na hali ya wananchi,achen unafiki na ujinga,elimikeni!au kwa sababu wengine mko kwenye neema mnawabeza ambao hawana?uzuzu na ulimbuken huo!ccm lazima mtatoka tu taka msitake

Tatizo la sisi watz tunaona karibu sana! kuna baadhi yetu hapa watoto wa jirani wanalala njaa wakati yeye anamwaga chakula, ndugu na hata wakati mwingine mzazi wake akimtembelea anamuona mzigo! lakini akiwa humu JF atajisifu kwa kuonea huruma watanzania masikini! tofauti kati yako na serikali ipo wapi? ni kweli tuache unafiki!!
 
Wametukwaza kwa miaka 50 tangu uhuru, hawawezi kutufaa hata kwa mwaka mmoja, tena serikari ya Kikwete ndio zigo la Watanzania, since day one inaingia madarakani kazi yao ni moja tu KUBOMOA UCHUMI WA NCHI!

Kwa wenye akili timamu zenye utimamu serikali hii haistahili hata mwaka mmoja zaidi, 2015 mbali. Ni Serikali iliyojaa vilaza sio tu ya wasiosimamia maslahi ya wananchi bali ya wanaobomoa nchi na kutesa wananchi bila kuwajibika, No Accountability! Utampaje mtu ofisi ya UMMA(Public Office) bila kumfanya awajibike kwa utendaji wake?
Hadi leo raia wanauawa na polisi, mabomu, umeme unakatika kama tuko zama za mawe. Acha ufisadi na kujihalalishia matumizi yasiyo ya msingi kwa viongozi huku raia wakiwa hawana huduma za msingi (basic) acha zinazofaa.

Halafu tunakaa hadi leo eti tunasherehekea miaka 50 ya uhuru!!???

Hii ni miaka 50 ya upumbavu wa CCM. CCM ing'atuke kama muungwana Mwl Nyerere alivyong'atuka. 2015 mwisho wa tawala za Kinyapala.
 
SERIKALI inatumia zaidi ya sh milioni 50 kwa mwezi kwa ajili ya kugharimia malazi na chakula kwa ajili ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, anayeishi katika Hoteli ya New Afrika tangu alipoteuliwa, Tanzania Daima Jumatano, limebaini.

Taarifa ya Waziri Nahodha kuishi hotelini, ziliibuliwa bungeni wiki iliyopita wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


Ingawa taarifa ya bungeni hazikuwa za kina, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini Nahodha ambaye amepata kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), amekuwa akiishi hotelini hapo tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo Novemba mwaka jana.


Habari kutoka ndani ya hoteli hiyo yenye hadhi ya Nyota Nne zilisema waziri huyo amepangishiwa vyumba vitatu ndani ya hoteli hiyo.


Inaelezwa kwamba amepanga kwenye moja ya vyumba maalumu kwa vigogo, (Executive); chumba ambacho kina sehemu mbili, ikiwemo ya kulala na ya kumpumzikia.


Kwa mujibu wa habari hizo, chumba hicho kinalipiwa dola 300 kwa siku, sawa na sh 480,000.


Vyanzo vyetu vya habari vilitonya kuwa chumba cha pili kinatumika kwa ajili ya walinzi na wasaidizi wake na cha tatu ni kwa ajili ya wageni muhimu wanaomtembelea hotoleni hapo hasa familia yake ambayo iko Zanzibar.


Habari hizo zinasema vyumba hivyo vinagharimu dola 220 kila kimoja kwa siku.


“Kwa maana hiyo, serikali kwa siku inalipa dola 740, sawa na sh 1,124,800 kwa ajili malazi tu ya Waziri Nahodha.


“Kwa hiyo ukifanya hesabu kwa mwezi serikali inalipa sh milioni 33.7 kwa ajili ya malazi tu ya Waziri mmoja na hadi sasa ana miezi saba hotelini,” kilisema chanzo chetu cha habari.


Kwa mujibu wa habari hizo, gharama hizo ni mbali ya chakula na huduma zingine hotelini ambazo kwa mwezi ni zaidi ya sh milioni 20, hivyo kufikia kiasi cha sh milioni 50 kwa mwezi.


Sababu kubwa ambayo inadaiwa na serikali kumfanya waziri huyo aishi hotelini ni uhaba wa nyumba za mawaziri.


Inadaiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliyepita, Laurence Masha, alikuwa akiishi nyumbani kwake katika kipindi chote alichoshika nafasi hiyo na wala siyo kwenye nyumba ya serikali.


“Kwa hiyo Nahodha alipoteuliwa kushika wadhifa huo, serikali ikajikuta haina nyumba kwa ajili ya Waziri wa Mambo ya Ndani na hicho ndicho chanzo cha Waziri Nahodha kulala hotelini,” kilisema chanzo chetu cha habari.


Mbali ya Nahodha, kuna mawaziri wengine wanne wanaoishi hotelini kutokana na uhaba wa nyumba za serikali.


Uchunguzi zaidi unasema kuwa sababu kubwa ya Waziri Nahodha na wenzake kukosa nyumba, ni serikali kuwaacha baadhi ya mawaziri waliotemwa kuendelea kuishi kwenye nyumba za serikali.


“Kuna waziri alifariki; mjane wake bado anaishi kwenye nyumba za serikali, wapo mawaziri waliotemwa, wameomba wabaki kwa muda kwenye nyumba za serikali, ili wajipange. Hawa wote wameziba nafasi za mawaziri wa sasa,” alisema mmoja wa maofisa wa Wizara ya Ujenzi.


Habari zaidi kutoka ndani ya Wizara ya Ujenzi zimedokeza kuwa Nahodha ilishapata nyumba ya kuishi, lakini alikataa kwa madai kuwa haina ulinzi na samani za ndani.


Mtoa habari huyo alisema mvutano uliopo sasa ni kuwa kiongozi huyo anataka apewe stahiki hizo kama Waziri Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wakati Wizara ya Ujenzi ikipinga jambo hilo kwamba anapaswa kugharimiwa sawa na mawaziri wengine.


Chanzo hicho kimedokeza kuwa kilimtaarifa Waziri Shamsi kuwa kama anataka samani za nyumba awasiliane na Wizara ya Mambo ya Ndani anayoiongoza ili kuangalia uwezekano wa kupata vitu anavyovitaka.


Chanzo kingine cha Tanzania Daima Jumatano, kimedokeza kuwa Shamsi, anaweza kupewa huduma hizo kama angeendelea kuwapo Zanzibar na si bara ambako hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri.


Kilibainisha kuwa SMZ, haina utaratibu wa kuwapangia nyumba na kuwapa huduma mbalimbali ikiwemo ulinzi na wahudumu wa ndani viongozi wake wanaoishi nje ya Zanzibar.


Kiliongeza kuwa Shamsi, anapata huduma za hadhi ya Waziri Kiongozi kila anapokuwapo visiwani humo lakini anapotoka nje ya mipaka hiyo kwa maana ya kuwa Tanzania Bara, anagharimiwa sawa na mawaziri wengine.


Alipoulizwa na gazeti hili sababu za Waziri Nahodha kuendelea kuishi hotelini na gharama ambazo serikali inazipata, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ol- Medeye, alisema wizara yake haihusiki na utoaji wa makazi ya viongozi na watendaji wa serikali, bali inahusika kwa Watanzania wote.


“Suala hili sio la wizara yetu, hatuhusiki kabisa na makazi ya mawaziri wala viongozi wengine wa serikali, tunahusika na makazi ya Watanzania wote,” alisema Naibu Waziri huyo.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alipoulizwa kuhusiana na suala la makazi la Waziri Nahodha na wengine, alisema hajui chochote kwani yuko mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti.


“Mimi sijui chochote, muulizeni Katibu Mkuu ambaye yuko jijini Dar es Salaam, atawapa ufafanuzi,” alisema kwa kifupi Dk. Mwakyembe.


Sakata la Waziri Nahodha kuishi hotelini, liliibuliwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF).


Mbubge huyo alitoa taarifa zilizomshtua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na wabunge wengine kuwa Waziri Nahodha, anaishi hotelini.


Kabla ya kutoa kauli hiyo, mbunge huyo alihoji dhamira ya serikali katika kupunguza matumizi.


Alisema serikali inakusudia kusitisha ununuzi na matumizi ya mashangingi, kuacha kuagiza fenicha kutoka nje na kupunguza posho kama moja ya njia ya kupunguza gharama za matumizi kwa serikali.


Alisema pamoja na dhamira hiyo ya kubana matumizi, serikali imewaacha baadhi ya mawaziri wake waishi hotelini na hivyo kuongeza gharama za matumizi.


“Kuna mawaziri wanaishi hotelini tangu walipoteuliwa hadi sasa, serikali haioni kama hali hiyo ni kikwazo kwa mafanikio ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano tulioupitisha hivi karibuni bungenin?” alihoji mbunge huyo.


Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Pinda kwanza alionekana kushangazwa na taarifa hiyo na baadaye alimtaka ataje majina ya mawaziri anaowajua wanaishi hotelini hadi sasa tangu walipoteuliwa.


“Naomba Mheshimiwa Mbunge nitajie majina ya mawaziri unaowajua kwamba wanaishi hotelini,” alisema Pinda.


Mbunge huyo ambaye alikuwa akisubiri majibu ya Waziri Mkuu kwa hamu, akataja jina la Waziri Nahodha kwamba ni mmoja wa mawaziri wanaoishi hotelini.


Huku akiwa haamini na kumwangalia Waziri Nahodha, Pinda alijibu kwa kifupi tu: “Basi nimesikia.”
......................
 
Kwa akili finyu ya mleta hoja angekuwa wa maana kama ange elezea na mambo mazuri ambayo CCM imefanya! Lakini kwa ushabiki mahaba wa kutumwa na Chama chake au kwa umbumbu wake ameonesha kuwa CCM haijafanya lolote! Ni ujuha wa ushabiki mahaba! Miaka ya 50 ya uhuru mafanikio tuna anza kulinganisha wapi? Nchi haikuwa hivi kama ilivyo maisha ya watanzania yamebadilika sana japokuwa maendeleo hayawezi kuwa timilifu kwa wakati mmoja! Acheni ushabiki mahaba sifieni na mambo ambayo CCM imefanya!
Mimi si mwanachama wa chama chochote... lakini kwa jicho langu ninaona kama kazi kubwa ambayo CCM imefanya ni kuwany'ang'any'a walio wengi na kuwapa wachache........kuongeza pengo kati ya matajiri na masikini... lakini si kujisifia kwa mabadiliko ambayo yanakwenda kwa wakati na yasioepukika kama demokrasia ya vyama vingi nk..................... Siku tusishangae watapojisifia kuwa CCM ndiyo inayoleta mvua:A S 114:
 
vice versa is also true!
Kila mara huwa nawakumbusha watanzania wenzangu kwamba hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kushabikia kile CCM na serikali yake wanafanya. Ukiachilia mabali yaliyotokea Tarime ya kuua wananchi wanaoenda kudai mali yao inayo dhulumiwa na wezi wa kizungu na vibaraka wao ndani ya nchi.

Angalia wanavyo shughulikia suala la umeme. Kikwete mwaka 2006 alitamka kwa mdomo wake kwamba ndani ya miaka 3 chini ya utawala wake mgao wa umeme utakuwa historia, sasa na asimame na athibitishe usemi wake huo!!

Kiinimacho kingine ni upumbavu wanaoufanya juu ya mitambo ya Dowans. Wanapitia mlango wa nyuma kununua mitambo hiyo wakidhani hatujui, wadadisi wa mambo mkitafuta info kidogo mtajua hiyo kampuni ya Symbion imefikiaje uamuzi wa kujitwika Dowans na hapo mtagundua tu kwamba ni jamaa wanazunguka mbuyu.

Niseme tu kwamba kwa CCM na serikali zake walipo tufikisha, si tegemei kwamba kuna mtu ana akili timamu anaweza kujiunga na chama hiki ambacho ni cha kuangamiza wananchi na mali zao.
 
mkuu kuseam wanojiunga CCm ni wajinga Umeteleza....unataka tuwe na chama kimoja Au? dhumini la vyama ving ni kuwapa wananchi nafasi ya kuchagua chama wanchokipinda.... Unachokipenda wewe yule hakipendi, hatuwezi kuwa na mtazamo sawa wala mapenzi sawa..... unahuru wa kikatiba wa kutoa maoni yako lakini huna uhuru wa kuwa amua unachokitaka wewe kiwe matakwa ya jamii nzima. ukisema wasijiunge CCM basi ibaki CADEMA peke yake, na chadema wakiwa peke yao watukuwa kama CCm ya sasa..... naomba nikufundishe historia kidogo....CCM ni chimbuko la mfumo wa chama kimoja cha siasa kimelidhi kutoka TAnu na ASP, mfumo huu ndio umejenga ubwanyenye ndani CCM, sela za kubebana na kujuana ndipo zilipoanzia..... kama awtu wasipojiunga CCM hakutakuwa na changamoto...... acha uductecta katiba yetu japo inamapungufu mengi ila inatmbua kuwa binadamu wote ni sawa na wanahaki ya kutoa maoni yao pamoja kuchagua chama wanchokitaka.... kauli yako ni unconstitutional inayokufanya uwe dictecta... tuombe mungu asitupe viongozi wenye mtazamo kama wako labda uwe umeterza nu kulewa chuki dhidi CCM.
 
kuna mbunge mmoja wa chama cha magamba jana kasema wanatumia posho wanazopewa kuwakirimu wapiga kura wao
pindi wakifika kwenye majimbo yao ya uchaguzi,itabidi wakifika waniwezeshe na mimi japo kidogo.
 
Wewe ni Juha, Na ndio mijinga inayozungumziwa hapa, Usistitupe hiyo historia ya kijinga jinga ya CCM tunaijua. Tunachotaka ni jamii ya ambayo ina raia ambao ni critical thinkers, watu ambao sio wanakariri tu au wanashawishika tu, bali wanaoweza kupambanua sawia kwa kutumia akili zao na kujua nini kinaifaa Tanzania na nini ni Madudu.

Mimi si mwanachama wa Chadema lakini Chadema ndio chama Chenye msingi ninaoamini, na sishabikii hili kwa sababu nimeshawishika ni kwa sababu nimepima sera za vyama vyote kikiwemo Chako cha magamba na nikajua chama gani kina dhamira sawia kwa Tanzania na raia wake. Hii ni kutokana na sera nzuri, mtazamo na msimamo mzuri wa Chadema kutanguliza maslahi ya wanzania mbele katika yote wanayoyafanya na kusema.

Mfumo tunaotaka ni wa vyama vingi wenye ushindani, Chama kinachoshika madaraka kiwe scrutinized kudeliver kikishindwa kipigwe chini kiingie kingine, sio chama kimoja tu, tena iwe constitutional kam ilivovyokuwa kwa rais kwamba chama kimoja kisishike madaraka zaidi ya miaka 10.

Unafahamu fika ubadhilifu wa serikali ya CCM, Ufisadi, kukingia kifua posho zisizo na msingi wowote (wakati watanzania hawana mahitaji ya msingi kabisa) Ukubwa wa serikali na anasa zake kuanzia kujinunulia mashangingi, kupanda ndege business class (wakati viongozi ulaya nchi tajiri hawafanyi hivyo) Kutaka wasilipe kodi n.k....Mikataba mibovu ya madini na uwekezaji, kuiingizia nchi hasara, kutokuwajibika kwa serikali kutokana na ubutu wa waziri mkuu hadi Raisi wa nchi, leo tunakosa umeme kizembe zembe tu........in short unajua madudu ya Chama Chako cha Magamba halafu unasema (kwa kubana pua) "it iz unconstituional kusema wanaoshabikia CCM ni wajinga" Huo upupu wanaofanya CCM kufisadi Nchi na upuuzi mwingine ni Constitutional sio? ovyo kabisa!


mkuu kuseam wanojiunga CCm ni wajinga Umeteleza....unataka tuwe na chama kimoja Au? dhumini la vyama ving ni kuwapa wananchi nafasi ya kuchagua chama wanchokipinda.... Unachokipenda wewe yule hakipendi, hatuwezi kuwa na mtazamo sawa wala mapenzi sawa..... unahuru wa kikatiba wa kutoa maoni yako lakini huna uhuru wa kuwa amua unachokitaka wewe kiwe matakwa ya jamii nzima. ukisema wasijiunge CCM basi ibaki CADEMA peke yake, na chadema wakiwa peke yao watukuwa kama CCm ya sasa..... naomba nikufundishe historia kidogo....CCM ni chimbuko la mfumo wa chama kimoja cha siasa kimelidhi kutoka TAnu na ASP, mfumo huu ndio umejenga ubwanyenye ndani CCM, sela za kubebana na kujuana ndipo zilipoanzia..... kama awtu wasipojiunga CCM hakutakuwa na changamoto...... acha uductecta katiba yetu japo inamapungufu mengi ila inatmbua kuwa binadamu wote ni sawa na wanahaki ya kutoa maoni yao pamoja kuchagua chama wanchokitaka.... kauli yako ni unconstitutional inayokufanya uwe dictecta... tuombe mungu asitupe viongozi wenye mtazamo kama wako labda uwe umeterza nu kulewa chuki dhidi CCM.
 
Kwa wakati tulionao CCM haifai tena na hasa kwa vijana wanaotaka mabadiliko!!
 
Sio kushabikia ila ww pia ni vuvuzela maana wanatia mapka hasira sana kuona hawana jipya juu ya taifa letu tanzania
 
Katika hali kama hii bado jairo na CCM magamba wenzake wanagawana shilingi bilioni moja eti ili wapitishe bajeti.

madawati.jpg
 
Mimi nitaisifia ccm kwakuwa nina akili na wewe na nguchiro wenzio endeleeni kulalamika na hakuna chochote mtakachopata zaidi ya kupiga kelele kama za wapiga debe mateja wa kinondoni ccm ndiyo chama bora africa kukingoa madakarani ni hadi mwisho wa dunia
 
@ mleta mada, wewe wasema.


"'Love until it hurts, and when it hurts love some more, love until it hurts no more' by Smarter".


Surely reading all your comments concludes you as 'miss. Love-person' loving all and everything. Why not spending sometime to sleep rather than this tedious rubbi.sh?
 
Mtu yeyote anayejiunga au anayeishabikia CCM ama atakuwa punguani au ana mawazo ya kifisadi. Ni punguani kwa sababu hana uwezo wa kutofautisha mema na mabaya hivyo kumpa nafasi ya kuchagua yaliyo mema. Atakuwa na mawazo yakifisadi iwapo anajiunga au anashabikiia CCM kwa lengo la kujipendekeza kwa mafisadi wa chama hicho ili afaidike na ufiisadi unaofanywa na mafisadi hao.

Wengi wa watu wanaojiunga na chama hicho hawatoi sababu zinaingia akilini mwa mtu mwenye akili timamu
 
Back
Top Bottom