Huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia CCM

Huo ni mtazamo wako; akili timamu za kuishabikia CCM tunazo lakini hatulazimiki kushabikia vitendo vyake ambavyo havipo kwa maslahi ya watanzania. Hatukatai kuna mambo mengi yamefanyika kinyume na matarajio ya wanaccm lakini je matendo hayo yanatulazimisha tuhame? Je iwapo tutahama na kwenda Chadema na hadithi ikijirudia tuhame tena? Ukweli CCM kama chama hakihubiri ubadhirifu wa mali za umma tatizo lilopo ni viongozi wetu ambao wamepewa dhamana ya kuendesha chama ndio wanaoleta matatizo. Tatizo siasa yetu imeingiliwa na watu wasio waadilifu hata huko Chadema wapo viongozi ambao tayari wameshajionesha ni si waadilifu wapo kwa maslahi binafsi; nafahamu fika mpo kwenye vugu vugu la kupenda huyaoni kama utahitaji nitakupa mifano hii.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Hata UNICEF watu wanalipwa sasa bunge ndio imekuwa kanisa watu wasilipwe?wewe acha kelele za kinafiki.
Hivi hawa watu cjui wametokea wapi,hivi hamuwaonei watz wenu huruma kwa umasikin uliokithiri?kwanin tunapenda kushabikia tu bila kuangalia mustakabali wa taifa na hali ya wananchi,achen unafiki na ujinga,elimikeni!au kwa sababu wengine mko kwenye neema mnawabeza ambao hawana?uzuzu na ulimbuken huo!ccm lazima mtatoka tu taka msitake
 
Miezi kadhaa nilisema "huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia CCM" lakini waosha vinywa wakanikalia kooni. Sasa nalirudia tena kwani imejidhihirisha katika suala la kupunguza matumizi kwa kutowalipa wabunge posho za vikao kwani vikao ni sehemu ya kazi zao za kawaida.

Wabunge wa CCM wakiongozwa na spika wamegoma kata kata kuachia posho na mpaka wanamtishia Mh. Zitto Kabwe kuwa watamfukuza bungeni. Hii inadhihirisha kwamba CCM ipo kwa masilahi ya mifukoni mwao na si kwa maslahi ya wananchi na hivyo yeyote anayeishabikia pamoja na vitendo vyao naye hana akili timamu ya katambua mema na mabaya.

Miaka 50 ya uhuru na CCM madarakani lakini bado tuna shule za msingi zilizo ezekwa kwa nyasi, madawati hakuna ili hali tuna miti ya kutosha, umeme hakuna ili hali tuna makaa ya mawe hadi tunawauzia wageni, gesi ipo ya kutosha, geo-thermal ipo lukuki..... je, tuna haja gani kuwa na CCM??

Wenye njaa wanashabikia CCM ndugu yangu ili wapone njaa zao
 
Hata UNICEF watu wanalipwa sasa bunge ndio imekuwa kanisa watu wasilipwe?
wewe acha kelele za kinafiki.

Kwani Unicef ni serikali ya nchi gani na inaongoza walalahoi gani?
Je bajeti yao inawategemea wahisani kama Tanzania? Usishabikie
tu bila kujua msingi wa hoja husika
 
Lazima mama agome posho huna taarifa ya kuwa bara2 ilifungwa il ashushe mjengo?we unafikiri pesa gani zinatumika pale?Wanaowaita mafisadi tu na mapesa yote lakini bado wapo kung'ang'ania ubunge unazani ni padogo hapo?watu wanachuma sio mchezo
 
Nakuunga mkono 100%.Hata kama mtu huyo atasema anafanya hivyo kimaslahi,kama wengi wanavyo sema,lakini mimi bado nasema mtu huyo hana akili timamu.Mtu mwenye akili timamu habadilishwi na mazingira, ana msimamo usio yumba.
 
Wewe mwenye akili timamu umeakataa kiasi gani katika mshahara wako. Ukiwa huna akili timamu utakuwa unaona watu wote hawaakili timamu. Wewe ndo hazimo kabisa. Kataa mshahara wako wote tukuone ujinga wako zaidi.
 
Hata UNICEF watu wanalipwa sasa bunge ndio imekuwa kanisa watu wasilipwe?wewe acha kelele za kinafiki.
Mtoa mada ameshatanabaisha kwamba kama hauna akili ndio unaweza kuishabikia ccm.WEWE ni mmoja wao.Huwezi ukajiongezea malipo wakati wengine hawana hata uwezo wa kupata mlo angalau mmoja.Wabunge wanapewa posho kwa kuhudhuria vikao na mshahara juu.Acheni hzo watu wa magamba hamna utu ndani yenu
 
Hata UNICEF watu wanalipwa sasa bunge ndio imekuwa kanisa watu wasilipwe?wewe acha kelele za kinafiki.
...Serikali inatumia pesa nyingi katika kulipa posho...na tumewahi kuambiwa na wageni,kwanza tuna bunge kubwa linaloongezwa ukubwa karibu kila awamu,pili mishahara na posho za hao wabunge ni aibu...Kama mtu unamlipa posho katika kila kikao anachokaa...na mshahara wa mwisho wa mwezi ni wa nini? Yaani ni sawa na wewe bosi wako awe anakulipa sh 50,000/= kila siku ukifika tu ofisini na kuhudhuria shughuli na mwisho wa mwezi akulipe 1,500,000/= nini hiki?kuhudhuria vikao vya bunge ni moja ya shughuli za mbunge,hapaswi kulipwa kwa kuhudhuria vikao tena anahudhuria muda wa kazi hauwezi hata kusema ni overtime...Acha uvivu wa kufikiri unafananisha UNICEF na bunge,kwa hiyo una support wabunge kulipwa fedha nyingi hivyo mshahara tu 2,300,000/= marupu rupu kibao....Acha uji***a
 
Wewe mwenye akili timamu umeakataa kiasi gani katika mshahara wako. Ukiwa huna akili timamu utakuwa unaona watu wote hawaakili timamu. Wewe ndo hazimo kabisa. Kataa mshahara wako wote tukuone ujinga wako zaidi.

Mkuu vipi?? Nani kasema wabunge hawapati mshahara?? Hii ni posho juu ya mshahara, sasa ni ya nini wakati mshahara wanapata na kazi ipi inalipiwa posho?? Changanya akili yapo japo imkwisha oza kiasi!!
 
Mwenye akili timamu anashabikia chama gani??

Swali gumu! Lakini jibu rahisi ni kurudi tu kwenye topic....mwenye akili timamu hawezi kushabikia CCM. Ukikosa jibu unajiuliza swali hilo hilo tena halafu jibu linapatikana kwenye topic tena. Mwisho unatengeneza loop kama ile ya 'if not go to'. Ukifika hapo LAZIMA una kuwa na akili timamu kama sisi wengine.
 
Huo ni mtazamo wako; akili timamu za kuishabikia CCM tunazo lakini hatulazimiki kushabikia vitendo vyake ambavyo havipo kwa maslahi ya watanzania. Hatukatai kuna mambo mengi yamefanyika kinyume na matarajio ya wanaccm lakini je matendo hayo yanatulazimisha tuhame? Je iwapo tutahama na kwenda Chadema na hadithi ikijirudia tuhame tena? Ukweli CCM kama chama hakihubiri ubadhirifu wa mali za umma tatizo lilopo ni viongozi wetu ambao wamepewa dhamana ya kuendesha chama ndio wanaoleta matatizo. Tatizo siasa yetu imeingiliwa na watu wasio waadilifu hata huko Chadema wapo viongozi ambao tayari wameshajionesha ni si waadilifu wapo kwa maslahi binafsi; nafahamu fika mpo kwenye vugu vugu la kupenda huyaoni kama utahitaji nitakupa mifano hii.

Chama
Gongo la Mboto DSM
Tatizo halipo kwa viongozi!! Lipo kwenu wanachama!! Wao wanafanya hivyo kwa sababu mmewahakikishia uhakika wa kula wao na familia zao wakati ninyi mnauchapa usingizi wa pono. Katika hili ninakubaliana na viongozi wenu ni LAZIMA wawale kabla hamjazinduka usingizini. Mmewapa mamlaka ya kuwaendeshea Chama badala ya ninyi kukiendesha halafu mnatuambia tatizo ni lao (viongozi)! HAPANA. Mnaimbiwa nyimbo za amani na utulivu, pamoja na kuambiwa wale wanaojitahidi kuwaamsha kuwa ni watu wanaotaka kuuvunja amani na utulivu uliojengwa kwa miaka karibu ya 50 kutokana na usingizi mzito mnaolala.
Nikutie moyo tu kuwa karibu usingizi wenu unakaribia kuwatoka, sababu wengi wetu tumeamka tayari na tunajitahidi kuwasuksuka ili nanyi muamke ili twende pamoja kuwakataa hao unasema wameingia kwenye siasa zenu nzuri.
 
Wana magamba akina Malaria Sugu hii nchi yetu sote sio wengine 1st class then sisi ndo ndo namba kutupwa
 
Umeongelea wanaoshabikia CCM hawana akili timamu, Je sisi ambao tunakiongoza unatuweka kundi gani ndugu?
 
acha lawama wewe.Kodi yenyewe unalipa kidunchu alafu unataka maendeleo.Mtoto uzae wewe wakusomeshee wenzio hata haya huna.We wakuja nini?????

Huo ndio upungungufu wa akili anaozungumzia mwenzio, kwa hiyo unataka tukiwapeleka watoto wetu shule tuwanunulie na madawati?
 
Huo ndio upungungufu wa akili anaozungumzia mwenzio, kwa hiyo unataka tukiwapeleka watoto wetu shule tuwanunulie na madawati?
your IQ is very low Usiulize CCM na serekali yake itakufanyia nini bali wewe utaifanyia nini hapo usikute hata kaz hutaki umekalia kutotoa na kulaumu serekali.khaa! Kwisha habari yako.
 
Umeongelea wanaoshabikia CCM hawana akili timamu, Je sisi ambao tunakiongoza unatuweka kundi gani ndugu?

Wanaokiongoza ni lazima walikishabikia kwanza then wakaamua kukiongoza kabisa kwa hiyo jibu la swali lako liko wazi mkuu. Wito wangu tu..... tubadilike
 
Back
Top Bottom