Huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, May 25, 2011.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kila mara huwa nawakumbusha watanzania wenzangu kwamba hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kushabikia kile CCM na serikali yake wanafanya. Ukiachilia mabali yaliyotokea Tarime ya kuua wananchi wanaoenda kudai mali yao inayo dhulumiwa na wezi wa kizungu na vibaraka wao ndani ya nchi.

  Angalia wanavyo shughulikia suala la umeme. Kikwete mwaka 2006 alitamka kwa mdomo wake kwamba ndani ya miaka 3 chini ya utawala wake mgao wa umeme utakuwa historia, sasa na asimame na athibitishe usemi wake huo!!

  Kiinimacho kingine ni upumbavu wanaoufanya juu ya mitambo ya Dowans. Wanapitia mlango wa nyuma kununua mitambo hiyo wakidhani hatujui, wadadisi wa mambo mkitafuta info kidogo mtajua hiyo kampuni ya Symbion imefikiaje uamuzi wa kujitwika Dowans na hapo mtagundua tu kwamba ni jamaa wanazunguka mbuyu.

  Niseme tu kwamba kwa CCM na serikali zake walipo tufikisha, si tegemei kwamba kuna mtu ana akili timamu anaweza kujiunga na chama hiki ambacho ni cha kuangamiza wananchi na mali zao.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Minuso tuu inawasumbua watu ,utashabiliaje serikali katili yeny kukiuka haki za binadamu kama hii
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Hili la Dowans ni kichekesho kitupu
  Kampuni inatoka marekani kuja kununua mitambo mitumba tanzania
  kama walikuw ana mpango wa kuzalisha kumeme kwa nini wasingekuja na mitambo mipya ya kuzalisha umeme badala yake wanakuja kununua mitambo mtumba tanzania
   
 4. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu;
  Pamoja ni kweli kabisa ccm-regime si kwamba wanatakiwa kuondoka lakini kinachotakiwa ni kusambaratisha viongozi waliowahi kuongoza wasibadili vyama. Angalia Kenya mafisadi wa KANU leo ndo wanaongoza bado na ufisadi wa kasi zaidi unaendelea kwa mgongo wa PNU, sijui ODM.

  Napingana na mawazo yako, mie nafikiri utakuwa na mawazo ya kidikteta kusema wanaojiunga ccm ni wehu, waache binadamu waamuwe watakayo hiyo ndo demokrasia. Si binadamu wote wanapenda maisha mazuri wengine wanafurahi zaidi wakiwa masikini, kuna wengine wanafurahi zaidi wakiwa kwenye vurumai kama somalia, kuna wengine wanafurahi wakiwa ktk amani, kuna wengine wanafurahi zaidi wakiwa malaya na kunawengine wanafurahi wakiwa watulivu nk.

  Ninasochotaka kusema ni kuwa kujaribu ku-impose mawazo yako unayodhani ni mazuri kwa mtu unayedhani mawazo yake ni potofu ndo chazo cha udikteta, madkiteta huanza hivyo kwa kujaribu kui-impose mawazo yao mazuri juu yawengine. Na pia lazima utambue mawazo yako mazuri ndo mawazo mabaya kwa mwenzako.

  Nitakupa mfano
  Kuna jamii ulaya inaitwa Gypsy nafikiri utakuwa unaitambua, wao kufanya kazi ni mawazo potofu, kwao mawazo sahihi ni kuomba omba tu, wapo ulaya na kazi zinapatikana lakini kazi yao ni kuomba. Hapa nataka kusema, mwanadamu na kiongozi safi lazima uheshimu mawazo ya mwenzako.
  Mawazo yako mazuri unaweza kuya negotiate na unayemwona anamawazo potofu, na sio kuya impose kwa vitisho, kejeli na matusi.
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Yaani nimeona hii heading Nimecheka kicheko kisicho na nusu.
  Hivi majuzi nilikaa katika kilinge fulani na jamii moja ya wakulima, katika maongezi nilijaribu kujiweka katika support ya Chama Tawala.

  One of the very old men told me and I quote ''yaani kijana na ujana wako wote huo unaiunga cccm mkono? Lazima utakua na matatizo'' End of quote.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Si kweli kwamba kuna watu nafurahia kuwa maskini. Hapo ujue ujinga bado wanao na hapo ni failure ya serikali kuwakwamua huko. Mbona leo wamasai wanasoma shule na kusomesha watoto wao?? Mbona zamani ilionekana kuwa wao ni watu wa kuishi na ng'ombe tu??

  Ndugu, una uhuru wa kutoa maoni lakini kwa watanzania naona CCM inadhani hatuna akili ndo maana inafanya hayo ifanyayo. Hivi fikiria, India wananunua kwetu makaa ya mawe na wanazalisha umeme kwao, sisi ambao tuna makaa ya mawe hapa kwetu umeme hatuna, je, hili nalo tumlaumu nani???

  Mkataba wa TRL-RITES tumlaumu nani??? Je wanaoingia mikataba hiyo mbona hawajafungwa??? Je, unaweza kufanya ujinga huo China ukapona???? Tafakari!!!
   
 7. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,268
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  @ mleta mada, wewe wasema.
   
 8. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Agree by 100% esp kama una elimu
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hii ni kweli kabisa
   
 10. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Kuna jamii zinapenda umasikini ama kuomba omba nenda ulaya nzima kawatafute watu wa jamii ya Gypsy wao wanapenda kuomba omba kazi hawaendi hata kwa rungu. Hata hivyo mie nilikubaliana na sera na mienendo ya ccm-regime inaliangamiza Taifa, ambacho napingana na wewe ni kusema wote wanaojiunga na ccm ni vichaa, hii si kweli na ni asili ya udikteta yani ya kwamba unawataka wakajiunge wewe unakofikiri ni salama, lakini yawezekana wao wanafikiri huko wewe unakofikiri ni salama si salama zaidi.

  Hicho ndo ninachokiongelea, yani linapokuja swala la uamuzi lazima uheshimu mawazo na uchaguzi wa mtu. Fanya ka utafiti chukua watu 3 nenda kanunue shati dukani harafu omba maoni yao, utasishangae kuona unaloona ni shati safi wenzako watasema ndo shati bovu kuliko yote hapo dukani .

  Kuhusu nchi inavyoenda mrama chini ya usimamizi wa ccm, sina hoja nakubaliana na wewe 100% , lakini tusishurutishe watu kufuata tunachona ni sahihi, mawazo yao yaheshimiwe.
   
 11. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Umenena vema Mkuu.
   
 12. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Magezi

  Sikutegemea kauli hii itoke akilini mwako. Akina Magezi wote hufikiria kabla ya kutamka au kuandika. CCM ni chama Tawala hapa Tanzania. Hivi kwa akili yako undhani wote walioko CCM ni wajinga? Ni kweli, CCM imeundwa na inaongozwa na wanadamu, ninarudia wanadamu. Ni kweli ndani ya CCM kuna watu wachache, nirudie tena wachache ambao ni chini ya takribani 0.5% ya wanachama wote ambao kwa njia moja au nyingine wamepoteza sifa za kuwa wana-CCM. Dhana ya kujivua gamba inawalenga hawa.

  Sasa ndugu yangu Magezi, kwa sababu zipi unajumuisha watanzania wote wanaozidi 5,000,000 (wakulima, madaktari, walimu, wanazuoni, wanasiasa, wanafunzi, wavuvi, madereva, wakunga, n.k) na kusema hawana akili timamu kwa kuwa wako CCM? Umesema hayo wewe kama nani na kwa capacity gani? Je, wewe uko sawasawa?
   
 13. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ila hilo nalo neno....
  U-CCM, ni mawazo mufilisi.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Numefikiria sana mpaka nika weka mada hii. Kwanza ni kushangazwa na wananchi (wanaojiunga na CCM) kuto tambua kwamba wanaelekea kwenye kinywa cha mamba ili awatafune lakini wakishauriwa kwamba huyo ni mamba hawasikii,.... hapo nikasema ....hawa huenda hawana akili timamu.

  Pili, haiwezekani mtu mwenye akili timamu akatamka hadharani eti CCM haina mafisadi alafu baada ya siku mbili akawafunga wana-CCM kwa ufisadi. Hapo akili hakuna!!
   
 15. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,964
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Mambo yanayofanywa na CCM na serikali yake sasa hivi yanakifanya chama kionekane KAMA chama cha watu wenye upungufu fulani hivi wa kufikiri.

  Inasikitisha sana.
   
 16. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #16
  May 25, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu Naymi, Magenzi yuko sahihi kabisa, sisiemu wenywe wamekuja na mkakati wa elimu vijijini na mikoani kuna huko? wanaamini watu wao wako vijijini, sasa huko vijijini kuna wanaojijua kweli? kuna wanaoamini siasa ni kila kitu? huko wanakokimbilia sisiemu hasa vijijini ni kwa vile watu wa vijijini hawajapevuka kama mijini na urasimu wa kiuongozi ndiyo unawafanya watu wa vijijini waone chama ni sisiemu tu, unakuta mweneykiti wa kijiji au kitongoji analazimisha mambo kwa vitisho, hicho ndiyo kinachofanya hukovijijini wakichague sisiemu na kwamba wankipenda ila wakionekana wankikimbia watatishiwa au kususwa, na walioko mjini wote wapo kimaslahi zaidi, sasa sijui wewe upo kimaslahi gani maana huwezi kuona sisiemu inafanya vibaya hata kwa hali ya sasa??
   
 17. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mkama kwa issue hii usilinganishe na ulaya, watu wanaopenda kuomba kwa hobby si sawa na wanaoomba kwa sababu hawana options, watanzania hawajaendelea kiasi cha kufanya maisha ya kuomba iwe hobby.
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,401
  Trophy Points: 280
  ni kweli kabisa... u must be stupid if ur supporting that party!
   
 19. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Ukiona mtu anashabikia CCM ya leo jua kuna maslahi fulani anapata au anategemea kupata hata humu JF ukiona mtu ana support kila kinachofanywa na CCM hata cha kipuuzi jua huyo kama hajui anachokifanya akili zake zimetangulia, chukulia mtu anashabikia kitendo cha polisi kutupa jeneza barabarani hata kama ni ushabiki lakini ushabiki wa aina hiyo ni wa wendawazimu.
   
 20. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Vice versa also true. Na Huwezikuwa Ccm ukawa na akili timamu!
   
Loading...