Huwezi kuwa mpiganaji ukiwa ndani ya ccm? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huwezi kuwa mpiganaji ukiwa ndani ya ccm?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jile79, Aug 28, 2009.

 1. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Ccm kumkomalia sitta imeendelea kujiumbua zaidi na zaidi.Muda wote najaribu kufikiria kuwa hivi ningekuwa sitta sijui ningefanyaje(nijiuzuru?uspika napenda kwani kuna maslahi makubwa,lakini je maslahi binafsi ni bora kuliko ya taifa?,je kweli mimi ni mzalendo au natafuta tu umaarufu?)Sitta aachie ngazi huwezi kuwa mpiganaji ndani ya ccm.Ndio maana akina slaa,zitto hawaguswi pamoja na kuwa mwiba mkali kwa serikali kwani wako upande salama ccm si salama na hata walipojaribu kuwawajibisha ili kuwatiisha ikiwa ni pamoja na kuwekewa vinasa sauti ndani ya nyumba zao bado wakabaki na msimamo,slaa alikataa walipomtisha kuwa atakamatwa kwa kuwa anamiliki nyaraka za siri hakujali,alijiamini aliwajibu kwa kuwa tu yuko nje ya ccm.Wabunge wa ccm wamecharuka kwa kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakishuhudia wenzao wanavyojichotea keki ya taifa bila hata aibu wameamua kusema na wanayo mengi sana ila hawawezi kuyasema kwa sababu wapo ndani ya ccm.Akina mwakyembe walitishia kueleza kila kitu ambacho kingewagusa wakubwa kuhusu richmond kwani wanasiri nyingi ambazo hawawezi kuzisema kwa kuwa wapo ndani ya ccm.Serelii alieleza kuhusu ujenzi wa barabara ikachukua zaidi ya wiki moja kutoa jibu,jibu likawa serelii hajakosea na wala serikali haikukosea serelii akakaa kimya pamoja na majibu yasiyoridhisha ya mheshimiwa spika na kwa kuwa yupo ndani ya ccm.Wale majemedali wa ccm wa vita kuu dhidi ya ufisadi(mwakyembe,kilango,sitta,sendekA,serelii,kimaro,zambi,na wengine wengi)wanajua fika kuwa ccm ni mahututi ila wameamua kufa nayo hivyohivyo wakipigana,ccm yenyewe imewatisha.Watoke wote kwenye hilo tanuli ambamo kuna moto,wajimalize kabla hawajamalizwa na ccm.Wameambiwa kuwa bila ccm wasingeweza kuwa maarufu nao wamekubali wanaamini ccm ndio mama na baba yao wanogopa kuasi hawataki kuleta upinzani wa kweli ambao Baba wa taifa alishatabili kuwa utatoka ccm na ambao tuna usubiri kwa hamu.Tuta pata upinzani ulio na picha ya kitaifa hasa kuliko chama cha upinzani chochote kilichopo,we fikiria hawa wanaamua kujiengua kwa maslahi ya taifa(mwakyembe,kilango,sitta,sendeka,na wale wengine)hapa utapata chama chenye sura ya kitaifa kuliko vilivyopo sasa ambavyo eidha kuna udini au kuna ukabila au vyote.
  Tuendako siko,maamuzi mazito yanatakiwa ili kujinusuru na hali itakayojitokea.
  ''USAWA HAUPATIKANI KWA MZANI KUWA SAWA ,INATEGEMEA NA MPIMAJI MWENYEWE''
  [​IMG]
   
Loading...