Huwezi kuwa kiongozi imara bila kukubali kukosolewa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,213
2,000
Duniani kote binadamu kukosolewa ni jambo la kawaida ukosoaji unamuimarisha na kumjenga kiongozi haswa kimatendo na kimienendo
Hapa duniani hakuna mkamilifu
Lakini serikali yetu pamoja na mkuu wetu wa taifa hapendi kukosolewa kabisa
Ukimkosoa utarajie kutumbuliwa ama kubadilishiwa kazi ama kuondolewa kabisa
Hii mienendo itaigharimu taifa
Mfano mdogo ni suala la utafiti wa bi malecela kuhusu uwepo wa,zika waziri angekanusha lakini angeagiza timu ya utafiti kujua ukweli kama ni kweli ama la lakini badala yake wamemfukuza kazi
Haya ni mambo ya ajabu kabisa hadi kufikia 2020 tutakua tumejaza counter book ya mambo ya kushangaza yanayoendelea Tanzania
Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na Japan yamesonga mbele kwa sababu ya kuwepo kwa ukosoaji na kiongozi anayafanyia kazi
Hiyo tz ya viwanda itakuepo vipi wakati kunakuwepo na maamuzi ya mtu mmoja
Nawasilisha
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,955
2,000
Kweli kabisa Mkuu..

Huyu mtu hashauriki na kila mtu alie pembeni yake anaonekana kwake ni mpiga deal.

Unasema wewe ni kiongozi wa wanyonge wakati wanyonge ndio wanaoongoza kwa vilio vya Mateso.

So sad.
 

kulwa MG

JF-Expert Member
Aug 29, 2016
1,290
2,000
angekuwa na uwezo wa kimungu,sijui angewatendaje wanadamu..huyu malaika lucifer hawapendi mashetani wenzake wala malaika wasaidizi..anajipenda mwenyewe na kupenda kutukuzwa hovyo pasipo sababu za utukuzwa..jehanam inamungojea!!
 

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,070
2,000
Bado nakumbuka Clip moja ilikuwa inasema'' Hawa Ma-DC, Ma-RC pamoja na wakurungenzi kuhusu hii ishu ya wamachinga wawaache na kama kuna yeyote miongoni mwa hawa viongozi niliyowataja hawakotayari kwa hili waachie ngazi" Si kwamba ukiwa na mawazo mbadala uende ofisini mkajadili NO uachie ngazi huko huko ulipo...Mfano No.1 huu...
 

Aaaaaaa

Member
Dec 9, 2016
39
95
Hakuna mtu asiye penda kukosolewa ila tatizo huyo mkosoa anakosoa kwa nia ipi mathalan unapomkosoa kwa nia ya kujenga na ukikosoa uwe na njia mbadala ambayo wewe unaiona kutokana na upeo na taaluma yako kuwa ndio bola kuliko hiyo unayo ikosoa huo ndio ukosoaji wa watu welevu dunia nzima lakini sisi kama watanzania tunacho fanya sio kukosoa ila ni kulalamika na unapo muuliza huyo anae kosoa kuwa njia mbadala ni ipi hana jibu nafikili tunaitaji kubadili jinsi ya kufikiri kwanza
 

Da Lu

JF-Expert Member
Jul 18, 2016
929
1,000
Mambo yanaoyoendelea nchini kwa sasa yashanichosha jamaniii... Bora zrud zama za machifu tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom