Huwezi kumlinganisha Lowassa na Lissu. Lowassa alikuwa na mvuto kuliko Lissu

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,120
7,701
Kusema ukweli ukilinganisha kati ya amsha amsha ya Lowassa mwaka 2015 na Lissu mwaka huu 2020 naona Lissu hawezi kufikia hata nusu ya kura milioni 6 alizozipata Lowassa katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Labda Vyama vyote vya Upinzani visimamishe mgombea urais mmoja ndio angalu wanaweza kufikia kura milioni 6 alizopata Lowassa mwaka 2015.

Kwa maaana hiyo ni aibu kumlinganisha au kumpabanisha Lissu na mgombea wa CCM Magufuli, hawalingani kwenye mizani ni sawasawa na kupima gunia la mahindi upande mmoja na gunia la sufi upande mwengine!!

Magufuli anarekodi ya kujivunia ndani ya miaka 5 hilo halina ubishi, anachotafuta uchaguzi huu ni kuongeza asilimia ya ushindi tu.

Tuache ushabiki pembeni huo ndio ukweli
 
Lissu yuko tough kuliko huyo Lowasa .
1. Lissu amejijenga kutokea upinzani . Wakati Lowasa alijengwa na madaraka (vyeo) serikalini.
2. Lissu anazungumza hoja. Wakati Lowasa alikuwa bubu majukwaani
3. Lissu ni democrat wakati Maghufuli ana elements za ki dictator
4. Uchaguzi umeitishwa , Rais hata kama ni malaika lazima apingwe (challenge)
 
Kama huo ndio ukweli, uzi wa nini? Kuanzisha kwako uzi huu kunaonyesha kuna kitu unahofia
Hata wewe unajua ukweli ila hutaki kusema kutokana na ushabiki, mimi pia nawapenda sana wapinzani ila penye ukweli huwa nawaambia ukweli tu bila kuficha
 
Lowasa haitatokea tena labda kwa maiaka 20 ijayo hawa wengine kufikisha kura 1,000,000 itakuwa sawa na ushindi
 
Lowassa alikuwa na Pesa za kampeni Lissu Hana.

Lowassa alifahamika mijini na vijijini kwa watu wote sababu ya cheo chake Cha uwaziri mkuu na uchapa kazi Lissu anajukikana miji michache na hawajui kazi zake aliyowafanyia wanachi anajulikana jina tu

Lowassa alikuwa anakubalika na Viongozi wa dini wengi ,wasanii nk Lissu viongozi wengi wa dini na wasanii hawana mpango naye na yeye Hana mpango nao wakati wao ndio wenye watu wengi
 
Kwanini sasa Lowassa hamkumpa urais sasa kama alikuwa na sifa zilizotukuka namna hyo, kwanini hamkuisha kumsema na kumtukana ?
Lowasa alikuwa na Pesa za kampeni Lisu Hana
Lowasa alifahamika mijini na vijijini kwa watu wote sababu ya cheo chake Cha uwaziri mkuu na uchapa kazi Lisu anajukikana miji michache na hawajui kazi zake aliyowafanyia wanachi anajulikana jina tu

Lowasa alikuwa anakubalika na Viongozi wa dini wengi ,wasanii nk Lisu viongozi wengi wa dini na wasanii hawana mpango naye na yeye Hana mpango nao wakati wao ndio wenye watu wengi
 
Mleta mada labda tu nikujuze, Lowasa alikuwa na mvuto kwako. Wengine kama mimi tulimpigia kura kwa sababu ya CDM na si kingine. Hata leo nikimuona huwa najiuliza sana kwanini nilimpigia kura mtu asiyeweza hata kuongea??? Jibu lake ni CDM ndio ilimbeba. Mwambie agombee leo kama atapata kura hizo.
 
Wapo wanafikiri kushinda uchaguzi ni kufokafoka jukwaani pekee!

Sasa ilikuwaje mkamuacha Dr Slaa bingwa wa jukwaa mkamchukua Lowasa wa maneno matatu?
 
Tofauti kuu Kati ya Lowassa na Lisu ni.kuwa Lowasa alikuwa na uwezo wa kuviungsnisha vyama vyote vikubwa vya upinzani vimchague yeye kuwa mgombea wao na vimpe kura zao zote yeye

Lisu uwezo huo Hana ndio maana kila chama kikubwa Cha upinzani kinaenda kivyake
 
Mwaka 2015 mimi nilimpa kura Lowasa kwa sababu tu yakutaka mabadiliko ya kimfumo nchini, lakini jamaa alijua kutuangusha majukwaani, watu wanakaa masaa matano uwanjani kumsubiri lakini akifika anahutubia kwa dakika 5 tu anaondoka. Lissu hana uzembe huo, mwaka huu kampeni zitanoga sana. #niyeye2020
 
Kwanini sasa lowasa hamkumpa urais sasa kama alikuwa na sifa zilizotukuka namna hyo, kwanini hamkuisha kumsema na kumtukana ?
CCM hatupigii kura mtu Bali chama.Tunatoa kura kwa kila CCM aliyegombea Raisi, mbunge na Diwani.Lowasa alikuwa Chadema nisingempa kura hata angekuwa vizuri vipi chama alichoenda kibaya
 
Kusema ukweli ukilinganisha kati ya amsha amsha ya Lowassa mwaka 2015 na Lissu mwaka huu 2020 naona Lissu hawezi kufikia hata nusu ya kura milioni 6 alizozipata Lowassa katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Labda Vyama vyote vya Upinzani visimamishe mgombea urais mmoja ndio angalu wanaweza kufikia kura milioni 6 alizopata Lowassa mwaka 2015.

Kwa maaana hiyo ni aibu kumlinganisha au kumpabanisha Lissu na mgombea wa CCM Magufuli, hawalingani kwenye mizani ni sawasawa na kupima gunia la mahindi upande mmoja na gunia la sufi upande mwengine!!

Magufuli anarekodi ya kujivunia ndani ya miaka 5 hilo halina ubishi, anachotafuta uchaguzi huu ni kuongeza asilimia ya ushindi tu.

Tuache ushabiki pembeni huo ndio ukweli
Mbona Lisu anaogopeka kuliko Lowasa

Vikao vinakaa Kila siku kubadili jinsi ya kumzuia asigombee kwa Nini?
 
Mwaka 2015 mimi nilimpa kura Lowasa kwa sababu tu yakutaka mabadiliko ya kimfumo nchini, lakini jamaa alijua kutuangusha majukwaani, watu wanakaa masaa matano uwanjani kumsubiri lakini akifika anahutubia kwa dakika 5 tu anaondoka. Lissu hana uzembe huo, mwaka huu kampeni zitanoga sana. #niyeye2020
Huo.umati Lowasa alikuwa aliwaweka kwa pesa zake wakisibiri aonger kidogo wapate Chao waondoke

Sasa hivi kusanya watu Halafu waambie wakae masaa matano wanamsubiri Lisu are uone akija Kama atamkuta mtu mkutananoni atakuta wote wameondoka
 
Back
Top Bottom