Huwezi kuichafua oil chafu, itakuchafua. RIP Dkt. Magufuli

Siyo siri tena, nimebaini mchezo mchafu unaendelea kwa lengo la kumchafua Hayati Dkt Maguli.

Taratibu wanafiki wanaanza kujionesha mmmoja mmoja, wanahaha kama mtu aliyekula nyama ya binadamu. Mpaka kufikia June wanafiki wote watajulikana...


Ukiona manyoya ujue ameisha chinjwa

Fuga mwingine tu babu

Nadhani kichwa cha habari kinajieleza nilikua sijui kumbe alikua oil chafu tayari du !!! kiasi kwamba uchafu mwingine hawezi kuonekana kirahisi kwa sababu alikua ameshachafuka tayari
 
Siyo siri tena, nimebaini mchezo mchafu unaendelea kwa lengo la kumchafua Hayati Dkt Maguli.

Taratibu wanafiki wanaanza kujionesha mmmoja mmoja, wanahaha kama mtu aliyekula nyama ya binadamu. Mpaka kufikia June wanafiki wote watajulikana...
By Malisa Godlisten

Mmesikia serikali ya wanyonge? Serikali takatifu ya shujaa wa Afrika, tuliyeambiwa amefuta ufisadi? Ngoja nikutajie machache;
Ujenzi wa SGR umesababisha hasara ya 3.5Bil kwa kuajiri wafanyakazi wa kigeni wasiokua na vibali.

Kigwangala alitumia 172M kuandaa Kili challenge lakini pesa hizo hazijulikani zilitumikaje (hazina risiti).

Akaunti ya jeshi la zimamoto ilitumika kupitisha 261M. Yani watu walipiga "mchongo" wakakosa akaunti ya kupitishia, wakatumia akaunti ya zimamoto. Zilipoingia wakazitoa wakasepa. Just imagine watu wana ujasiri wa kupitisha pesa chafu kwenye akaunti ya jeshi? Halafu tunaambiwa mwendazake alinyoosha nchi.

Wasafi walipewa 140M, TBC 201M na Clouds 629M kutangaza tamasha la Urithi Festival. Lakini hakuna mkataba wala risiti yoyote ya kujustify malipo hayo.
18Bil zilizokusanywa ktk wilaya 135 hazikufika serikalini. Yani zilikusanywa lakini wajanja wakalala nazo mbele.

3.9Bil zilitolewa kukarabati ndege ya ATCL iliyopaki tangu mwaka 2015, lakini hela imeliwa na ndege haijakarabatibwa. Yani watu walitafuna milioni 3,900 halafu hawakupaka hata rangi.Hayo ni baadhi tu ya "madudu" ya serikali takatifu ya mwendazake. Sijaongelea HESLB, TANAPA, TANROADS, SGR, Stligler's gorge, Stand ya Magufuli. Huko kuna madudu ya kutisha.

Lakini tuliaminishwa serikali ya mwendazake haikua na doa. Watu waliokosoa waliitwa vibaraka. Serikali takatifu haikutaka kunyooshewa kidole.

Tujifunze kutofautisha mtu msafi na anayeficha uchafu. Mwendazake hakua msafi bali alijua kuficha uchafu. Ndio maana akaminya uhuru wa habari. Hatukusikia skendo kama za Escrow tukadhani serikali yake ni safi, kumbe kuna skendo kubwa zaidi ya Escrow lakini zimefichwa uvunguni.Ndio maana nasema afadhali JK aliruhusu media ziwe huru. Skendo za Richmond, EPA, Escrow aliacha wananchi wajue. Lakini mwendazake alifunika skendo zisifike kwa wananchi.

Ndio maana watu wamemtania CAG atoe pia ripoti aliyopanga kumpa mwendazake, maana angekua hai asingethubutu kusema ATCL imepata hasara ya mabilioni, au SGR imeleta hasara, au mradi wa Stigler's umejaa madudu. Angeficha kwa sababu ndivyo mwendazake alivyopenda.

Tunahitaji viongozi wasafi, sio wanaojua kuficha uchafu.!
 
Siyo siri tena, nimebaini mchezo mchafu unaendelea kwa lengo la kumchafua Hayati Dkt Maguli.

Taratibu wanafiki wanaanza kujionesha mmmoja mmoja, wanahaha kama mtu aliyekula nyama ya binadamu. Mpaka kufikia June wanafiki wote watajulikana...
Kaka Unajua maana ya "Ripoti ya Ukaguzi?" Unataka Ripoti isifie? Nenda kwanza Darasani kisha Urudi uchapishe andiko lako
 
Hata kuondolewa kwa Bashiru Ikulu hii ni mipango ilikuwa imeandaliwa,walianza kwa kumchafua sana lakin sasa hivi huwezi sikia wanamwongelea sababu lengo lao limeshatimia!
Ili umpige mbwa mpe kwanza jina Chafu .Issue ya Bashiru iliniuma sana aisee.Hata kama ni chuki kwa hekina angemhifadhi hata nmiezi minne lakin hata matanga hatujaanua jamaa anatolewa tena kwa kudhalilishwa.

Sasa hivi mama anawasikiliza ukawa huko twitter,wao ndo wanapanga nani awe mkuu wa wilaya nani atolewe .
Soon tunauzwa.
RIP JPM
 
Magufuli will remain the greatest president JMT ever had. Wapiga zomali na mapambio ya kumchafua wanaendelea kusumbuliwa na kivuli chake. To be truthful Samia anapwaya sana bila mtu kumshika mkono... Nina hisia ipo siku atatema nyanga.... Ngoja azinduke ndo atajijua akizingua tunamzingua...,🤔
 
Unaelewa kazi ya CAG wewe?? Kwa nini hii nchi ina watu wajinga hivi!
Kwa faida yako fahamu Kazi ya CAG ni kukagua fedha za umma zimotokaje na zimetumikaje kulingana na sheria za manunuzi. Kama zimetoka kwa utaratibu wa hovyo au zimeibiwa anapaswa kuonyesha hivyo kwenye ripoti na kutoa hati chafu ikibidi. Kama zimetoka kwa utaratibu unaofaa kisheria anatoa hati safi..
Umeeleza vizuri sana labda tu hizi taarifa za ukaguzi zilikuwa haziwekwi wazi au ukaguzi ulikuwa ukifanyika kwa woga hata hivyo wakati mwingine taarifa hizi haziaksi hali ilivyo mfano ofisa akichukua masurufu ya shilingi milioni moja akarejesha nyaraka za matumizi halali ya shilingi laki tisa na elfu tisini hoja ya ukaguzi itasomeka masurufu ya shilingi milioni haijafungwa wakati hali halisi ni shilingi elfu 50 ndizo hazina maelezo
 
Ili umpige mbwa mpe kwanza jina Chafu .Issue ya Bashiru iliniuma sana aisee.Hata kama ni chuki kwa hekina angemhifadhi hata nmiezi minne lakin hata matanga hatujaanua jamaa anatolewa tena kwa kudhalilishwa.

Sasa hivi mama anawasikiliza ukawa huko twitter,wao ndo wanapanga nani awe mkuu wa wilaya nani atolewe .
Soon tunauzwa.
RIP JPM
Eti angemhifadhi
Kumbe mlishaziea kuhifadhiana eeh? Sasa alokuwa anawahifadhi hayupo mmepoteana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ushahidi wa ripoti hii ya CAG Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi,fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda.
 
rais mstaafu nahisi yupo nyuma ya hii skendo ya kuchafua jina la makufuli ila makufuli hakufukua makaburi ya wenzake alificha
whitch hunt doesnt work in this case. ukiwa na mawazo kama hayo utahisi mpaka nyerere anahusika.
Jpm hakuwa malaika. alikuwa mwanadamu wa kawaida. kama wanadamu wengine alikuwa na madhaifu yake. na madhaifu ndio hayo.

msije kujaribu ku white wash mtu. kila mtu avune alichopanda
 
Back
Top Bottom