Huwezi Kufunika Jua na Ungo.

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Duniani kuna mambo mengi, kuna hila nyingi na fitina nyingi. Kuna watu wanapoona mwezao amefanikiwa au anaelekea kufanikiwa kwenye jambo huanzisha fitna, hila, majungu na hujuma ili mradi tu akwame basi , na hii tabia ni maarufu sana Afrika, Tanzania specifically.

Hata hivyo nilichobaini ni kuwa:

Ambaye Mungu kampa , kampa tu hata kama mimi na wewe hatutaki. Kuna watu wamejaaliwa akili na ubunifu mkubwa, anapobuni kitu "A" hata ukimuhujumu anaweza kubuni kitu "B" na ukimfitini anabuni "C" na kote anatoka tu!. Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kumbe

"Huwezi kuziba jua na Ungo".
Ni bora ukiona mwenzako kapambana kafanikiwa na wewe pambana sio kumuhujumu ili mkwame wote. Mwisho wa ubaya huwaga ni aibu, tuache fitna na kuwahujumu wengine tupambane kutafuta maisha kwa ubunifu, uchapakazi na kumuomba Mwenyezimungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom