Huwezi kimbia kifo, alitoroka hukumu ya kifo akafa kwa kipigo bar

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
gregg.jpg

Georgia, Marekani, hili ndilo tulio la kwanza kwa mtu aliyehukumiwa kifo kutoroka gerezani. Alitoroka siku moja kabla ya hukumu yake ya kifo. Bahati mbaya mtu huyo, alifariki kesho yake kwenye ugomvi uliotokea BAR

Troy Leon Gregg alizaliwa April 22, mwaka 1948 na kufariki July 29 mwaka 1980. Gregg alikamatwa kwa tuhuma za kuua na kupora watu wawili (Fred Edward Simmons na Bob Durwood mnamo November 21 mwaka 1973). Mwanzoni alikana kuhusika lakini uongo wake haukuzaa matunda

Hadi alipokiri kutekeleza tukio hilo. Alijitetea kwa kusema hukumu ya kifo ni nzito sana kwake na ni kinyume cha sheria lakini Wazee wa baraza wakapinga mashauri yake yalitupwa chini. July 28, 1980 Gregg na wafungwa wengine 3 , walifanikiwa kutoroka kwa kuvunja milango ya selo,

Guku wakiwa wamevalia nguo za askari magereza. Askari hawakujua kama hawa mabwana wametoroka hadi pale Gregg alipowapigia simu watu wa gazeti na kuwasimulia yeye mwenyewe kuwa ameshatoroka.

73557158_131102901979.jpg

Siku hiyo hiyo Gregg alianzisha fujo bar na kumfanya achezee kipigo mpaka mauti kumfika. Maiti yake ilikutwa ziwani, wenzake watatu walikamatwa siku tatu baadaye.
 
Back
Top Bottom