Huwenda hizi ndizo zama za mwisho kwa CCM kuiongoza Tanzania, nikitafakari kifo cha Rais John Magufuli na hili la Machinga nafsi yangu inaniambia kitu

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
782
1,000
Kwa mambo hayo mawili naiona Tanzania mpya ikija kwa kasi ya ajabu, na tuelewe ya kwamba watu wa chini kama hawa machinga ndio wamekuwa chachu ya kuleta mabadiliko katika nchi za wengine.

Tujaribu kukumbuka kilichotokea tunisia december 17/12/2020 baada ya machinga anayeitwa “Mohamed Bouazizi” ambaye aliamua kujichoma moto akiwa mzima kabisa na vuguvugu la mapinduzi katika nchi za kiarabu.

Kwa wingi wao hawa machinga busara itumike kuwaondoa katika maeneo yao waliyoyazoea na si vurugu tunazozishuhudia kwa sasa.
 

kopites

JF-Expert Member
Jan 28, 2015
6,208
2,000
Mwacheni Mwendazake apumzike, alidhihakiwa sana,saiv mnamkumbuka tena,hao wamachinga wapambane na hali zao.
 

kopites

JF-Expert Member
Jan 28, 2015
6,208
2,000
Hakuna mwenye akili anaemkumbuka
Serikali inamkumbuka kiongozi wake,sembuse wewe okoroo hakuna anaekujua.Kigogo wa Twitter alikua anawalisha chuki dhidi ya magufuli wajinga wajinga km nyie,na saiv kawahama tena 😂
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,119
2,000
Jisemee nafsi yako usiwasemee wengine boss, Rais Magufuli atakumbukwa sana kwa upendo wake wa dhati kwa watanzania wote

Hao nao wanamsemea nani?Kumbuka at least 90% hapo ni chinga.
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,059
2,000
Fanya Kazi ramli hazitakusaidia,hao Machinga wako ni wachache sana hapa Tzn tena wako miji mikubwa tuu,huko mikoani na Vijijini waliko wapiga kura Wana wachota tuu huko ..

Ujue nyie watu wa mjini huwa mnajifariji Sana,kila kitu kupinga,kwa akili zenu za kijinga ukipinga tozo afu serikali ikakusanya ikajenga hospital na vituo vya afya Vijijini unadhani utawaambia watu wa kijijini ujinga wako? Ndio sawa na hayo ya machinga yako mjini tuu ambako hata kura hampigagi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom