Huwa unatumia Mswaki wako kwa muda gani kabla ya kubadilisha/kununua Mswaki mpya?

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
46,881
122,124
Wataalamu tofauti wa Afya hasa madaktari wa meno, wamebainisha kwamba mswaki lazima ubadilishwe kila baada ya miezi mitatu.

Hata hivyo, wengi wetu hatuzingatii hii kanuni ya kiafya ipasavyo kwa kuweka mdomo katika hali ya usafi, ila kuna baadhi wanaozingatia hii kanuni.

Kwa mimi binafsi hii kanuni huwa naivuta kabisa ambapo huwa natumia mswaki zaidi ya miezi mitatu

Ebu tuwe wakweli, wewe huwa unabadilisha mswaki kila baada ya muda gani kwa kujali afya ya kinywa chako?
 
ilikuwa hivyo zamani napiga hadi mwaka mzima
ila kwa sasa nabadili kulingana na ushauri wa daktari eidha miezi 2 au mi3 baada kugundua chanzo cha mavizi kuuma mpk nahamisha upande nilozoea kutafunia ni mswaki kutumia kwa muda mrefu kiasi brash kukakamaa inapelekea kuzihalibu nyama za vizi mwisho huvimba nashindwa kutafuna nahamia upnde mwingne kitafuna ambao hujazoea naishia kujing'ata tu
na sio kubadili mswaki kila miezi 3
inapaswa pia kila baada miezi umuone daktari wa meno akusafishe meno yako
vivo hivyo jitahidi kila wiki utumie magadi au ukikosa agharabu sabuni ya unga
ili kukifanya kinywa meno pamoja na fizi kuwa bora zaidi
 
Sikuizi miti mingine sumu nisije jishaua na chukua mti nasugua meno yangu mwishowe yanaanza kuanguka kama embe zilizoiva mtini

Kuna miti special inayotumika kama miswaki, hiyo ni mizuri sana
 
Back
Top Bottom