Huwa unapotezeaje kumpa shikamoo mtu usiye kuwa na uhakika anastahili shikamoo?

bush crazy

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
757
1,020
Poleni na kazi wakuu,

Katika maofisi mbalimbali kunawatu mwonekano wao huwa na utata either mwili mdogo au umri wake hautabiliki kiasi cha kukufanya uwe njia panda kumpa shikamoo au la.

Ila kuna watu wanapenda kuonekana wakubwa hata kama ni wadogo mfano watu wengi kutokea mkoa wa Mbeya.

Je, huwa unaipotezeaje shikamoo?

Mtu anastahili shikamoo akikuzidi miaka mingapi?

Mimi huwa nawasalimia pole na kazi kiongozi au mkuu!
 
Wanawake ndo huwa nawapotezea Sana maana mwanamke mwenye miaka 25 utasema ana 30+ na mwenye 30 utasema ana 40+ , hivyo huwa nawakwepa nisije kusalimia kitoto cha 2005 nikaonekana koro.

Ila wanaume huwa wanajulikana tu huyu kijana mwenzangu huyu mzee (Nampa heshima yake)
 
Wanawake ndo huwa nawapotezea Sana maana mwanamke mwenye miaka 25 utasema ana 30+ na mwenye 30 utasema ana 40+ , hivyo huwa nawakwepa nisije kusalimia kitoto cha 2005 nikaonekana koro.

ila wanaume huwa wanajulikana tu huyu kijana mwenzangu huyu mzee (Nampa heshima yake)
Wapo wanaume hawaeleweki pia we huoni Polepole mwenyewe anachanganya watu.
 
Wanawake ndo huwa nawapotezea Sana maana mwanamke mwenye miaka 25 utasema ana 30+ na mwenye 30 utasema ana 40+ , hivyo huwa nawakwepa nisije kusalimia kitoto cha 2005 nikaonekana koro.

ila wanaume huwa wanajulikana tu huyu kijana mwenzangu huyu mzee (Nampa heshima yake)
Kabisa mkuu kukadiria umri wa wanawake huwa inaleta utata kwa baadhi yao. Akishapata kazi na masiha fulani huwa wanabadilika sana miaka 25 kama 35 vile.

Vyuoni ndo balaa mwaka wa 1 katoto kanaonekana kabisa katoto kufika mwaka wa 3 ashakua mama mtu mzima wakati huo, mtoto wa kiume ndo unazidi kua katoto 😂😂
 
JK & Mzee Ruksa wangekataa zile hongo za shangingi na kasri walizopewa kwa hisani ya Bi Mkubwa, kweli hiyo shikamoo nisingeipokea. Lakini kwa mwendo huu, upepo ni kwamba ukipewa chukua, if possible, kwa mikono yote miwili na miguu pia. Tanzania bila ushamba inawezekana.
 
Back
Top Bottom