Huwa unafanyaje kurudisha uhusiano mzuri na baba yako, kipindi nguvu ya chuki inapokuwa kubwa zaidi?

Aisee nimeshindwa kusoma, ila natumai kuna kitu tu kilichotokea kikasababisha mkafarakana, kwa kifupi unatakiwa kujifanya mjinga tu na kurudi chini na kumuomba msamaha kama mzazi, wanasema mzazi hakosei hata kama ndio mwenye makosa.

Rudi chini muendee mtake radhi na ukiri kuwa kweli uliyofanya yalikuwa ni makosa ila bado nafahamu kuwa wee ni mzazi wangu nahitaji kukuomba msamaha baada ya kugundua kuwa nilichokifanya ni makosa. Hata kama hataonyesha kukusamehe kwa muda ule lakini tayari kuna kitu deep inside his heart kitakuwa kimemuingia. Tafuta wazee wenye busara ikiwa ni marafiki zake au ndugu ikiwezekana uwaeleze wakusaidie kumueleza mzee wako kwa kuwa umemuomba msamaha lakini hajaupokea.

Mwsho ni kwamba, mzazi ni binadamu kuna leo kuna kesho, akitangulia mbele za haki kabla hujamuomba radhi mapema YOU WILL BE A LOSER usikubali kuwa hivyo aisee. Ila pia kumbuka NAZI HAISHINDANI NA JIWE.

Nakutakia kila la heri aisee.

Shkamoo Mzaramo na asante kwa kunifurahisha. Walau umeonyesha kujali.😄😄
 
Baba alimaliza kazi yake pale mimba yako ilipotungwa, yaliyofuatia ni majaliwa. Yanayotokea kwa familia yenu sasa huyapendi na kama mzaliwa juna uwezo nayo. Pambana na maisha yako, hujui sababu ya mabadiriko ya tabia ya baba yako, na mara nyingi ni mfarakano wa ndoa. Kumbuka umaskini ukiigilia mlangoni upendo hutokea dirishani.
 
Ahsante sana mkuu, lakini nadhani siwezi kukoromeana Wala kubishana na mzee wangu sina ujasiri huo
Sijawahi kumskia diamond akimkoromea wala kumtukana baba ake lkn mapicha picha anayomuonesha dunia nzima inamuombea msamaha!! Kijana umeyafuga maradhi kiasi cha kutosha, inaonekana una mapenzi sana na baba kuliko mama yako maana naona km maisha yake yako hatarini kupitia wewe. Wazaramo wenzio wanaimba harusini kila siku "....hakuna mwana asie na mama..."! Fungamana na mama na wadogo zako, msahau huyo baba, au mpaka awachinje ndo mjielewe jamani!!!!!????
 
Shkamoo Mzaramo na asante kwa kunifurahisha. Walau umeonyesha kujali.😄😄

Marhabaaaaaa mkuu.

Unajua caring is everything then mengine yanafuata, sasa jamaa nashangaa wanawaka tu mkuu. Alaaaaa.

Thanks a lot mkuu wng.
 
Ushauri wangu kwako ni huu, andaa mchongo, m'bambikie kesi huyo mzee apigwe mvua ya kutosha not less than 3yrs, google sheria za makosa ya jinai uone itakayokupendeza ya miaka tajwa hapo juu, akiwa jela sasa, nenda shinyanga angalia km kuna masalia yoyote beba ila aliyompa kimada kisheria mwachie usimuulize then rudi A town, uza hiyo nyumba na mnunue nyumba nyingine muishi na mama na wadogo zako kwa amani na upendo. Akija kutoka jela nadhani mtakuwa mmesha move on kitaaambo! Perhaps na nyumba ndogo atamkuta kishaolewa na kidume kingine, atabaki yeye na pu*** zake tu zinamning'inia. Akija kwenu mtimueni na mumpige matukio mpaka awe kichaa akafie milembe!!!
 
Habari za jioni Wana forum, nimeleta kwenu changamoto yangu angalau nipate busara zenu za kiushauri, najua humu Kuna watu wazima, wenye busara, hekima na waliopitia changamoto mbalimbali za kimaisha nisingependa kuona vijana wenye mihemko ya matusi na wale wasio na busara kutumia Uzi huu kutoa matusi, masimango ama kejeli. Japo nimeandika kwa kirefu lakini ningeomba tusome ili muweze kunipa ushauri vizuri.

Mimi ndiye kijana pekee na wa kwanza ( 30aged kwa sasa) katika familia yetu ya watoto watano, wanne wote ni wa kike, binafsi naipenda Sana familia yangu, naipenda mno na kiukweli linapokuja suala la familia yangu huwa sina mjadala nipo tayari kufanya lolote ili tu iwe na furaha. Kwa miaka kadhaa familia inapitia changamoto kubwa Sana inayonifanya mda mwingine nimchukie Sana baba yangu, sikuwahi kuwaza kumchukia mzazi katika maisha yangu ila kiukweli baba yangu sijui ni nini kimemkuta.

Nimezaliwa na kukulia kijijini huko Shinyanga na wazazi wangu, huku maisha yetu yakitegemea zaidi kilimo Cha jembe, mwanzoni mwa miaka ya 2000 baba alisafiri kwenda Arusha kutafta maisha, akituacha Mimi, mama na wadogo zangu wanne kijijini mwaka uliofuata mama na wadogo zangu walimfuata baba huku Mimi nikibaki kwa bibi kijijini nikiendelea na masomo. Nilipomaliza elimu ya msingi niliungana na wazazi wangu Arusha, kiukweli maisha hayakuwa mazuri Sana japo baba alikuwa amenunua kiwanja na kuanza kujenga nyumba za kuunga unga ( chumba kimoja kimoja). Baba alikuwa mpiganaji Sana ambae hakupenda kuona watoto wake tukipitia magumu,..alipambana kwa kila namna ili tuweze kusurvive. Kwa kipindi hicho nilishuhudia baba yangu akijatahidi sana kuihudumia familia kwa kila alivoweza, alifanya kazi yoyote ilimradi apate pesa ya kuhudumia familia.

Baada ya kuhamia Arusha nilipelekwa kidato Cha kwanza shule ya kata, nikiwa kidato Cha pili maisha ya baba yalibadilika ( mifereji ya pesa ilianza kuonekana) akanihamisha nikapelekwa shule ya private ambako nilimalizia elimu yangu ya O'level, Nikafaulu kwenda Advance na baadae chuo nikisomea kozi ya uhandisi, kipindi hiki mzee wangu alikuwa ameshauaga umaskini alikuwa ashajenga nyumba nyingine nzuri tu pembeni mwa ile ya mwanzo ya kuunga unga iliyokuwa inajengwa kwa chumba kimoja kimoja ikiwa na vyumba 8 pamoja na gari 2 za kutembelea.

Baba yangu alibadilika Sana kwa kipindi kifupi baada ya pesa kuanza kumtembelea ilikuwa ni starehe na yeye, yeye na starehe na Wala hakutaka ushauri ilikuwa akipata pesa anachukua gari haonekani mpka ziishe akawa mzee wa totoz Sana, binafsi nilijaribu kumshauri awekeze miradi ya kumuingizia pesa zaidi but niliishia kutukanwa na kudhalilishwa, lakini mda mwingine nikawa nakumbuka mateso aliyopitia mzee kuzitafta pesa nikaona ni sawa tu acha ajilawaze kwa vile alikuwa anaipenda Sana familia yake, inakula vizuri watoto wote wanasoma private school kasoro wa kike anaenifuata mm ( yeye alikataa mwenyewe akisema hana akili ya kusoma).

Mwaka 2012 nilipata ajira serikalini, na kipindi hicho nilikuwa na mpenzi wangu aliyekuwa mjamzito akiwa anasoma ustawi wa jamii ngazi ya diploma mwaka wa mwisho, nilipopata kazi tu tulitambulishana na kuanza kukaa wote Kama mke na mme.

Nilipangiwa kazi mkoa tofauti na Arusha hivyo nilikuwa mbali na Wazazi kidogo lakini mda mwingi tulikuwa tunawasiliana, mipango mingi ya mzee kwa kipindi hiki akiwa ameanza kupata pesa alikuwa hanishirikishi hivyo nilikuwa nasikia tu baba yako kanunua hiki, kafanya kile mimi nilikuwa nikimpigia simu nampa moyo tu aendelee kupambana.

Nilimaliza mwaka sijarudi kuonana na Wazazi japo nilikuwa nawasiliana nao Sana, na mzee japo nilikuwa namshirikisha mipango yangu karibia yote nae akawa ananipa moyo nipambane nilipojaribu kumuuliza maendeleo yake hakuwa anaiweka wazi, japo kwa pembeni nikawa napigiwa simu na baba wadogo naelezwa baba kakutwa baa kanywa hajiwezi kaibiwa pesa, Mara anatembea na watoto wadogo rika za wadogo zangu bila kificho... Mzee ni mkali ilikuwa ni vigumu kwangu kumshauri masuala Kama haya, hivyo sikuwa na namna zaidi ya kutulia na kipindi hiki nyumbani ilikuwa ni vurugu kila siku mzee anaanzisha ugomvi tu, kiukweli nikaaanza kumuona baba akiwa amebadilika sana, nyumba ikaanza kuwaka Moto kukawa hamna amani tena hata marafiki zake, ndgu zake wakawa wanatukanwa maskini hawana hadhi ya kufuatana nae ikabidi nimpigie niongee nae Kama kijana wake mkubwa lakini niliishia kutukanwa Sana, sikuwa na namna zaidi ya kutulia.

Mzee akawa ni mtu wa matumizi bila mipango, hapa hata familia ( wadogo zangu) wakawa hawajaliwi tena siku moja mama akanipigia simu kunieleza hali na maisha aliyokuwa nayo baba kwa mda huo ( hii ilikuwa Mara ya kwanza mama kunipigia simu kunielezea masuala ya mzee), akaniambia mzee ana hali mbaya na pesa kwa mda huo sio Kama mwanzo hivyo maisha ya nyumbani kidogo sio mazuri, ilibidi nichukue likizo ya mwezi nirudi nyumbani kuongea na baba na kuona namna ya kuokoa jahazi.

Nilipofika nyumbani kwa kweli nilikuta hali ya uchumi sio nzuri kwa baba, mzee sio yule niliyemzoea akifika sehemu anachoma mbuzi mzima na kula na marafiki sio huyu tena, Tuliongea mengi na mzee na akawa anasema ni kipindi tu kimebadilika na pesa imekuwa ngumu tena kwa busara sana na akanipa wazo lake la biashara zuri sana nililipenda na nikaona Kama akilifanya kweli litazaa matunda na akadai ni kwa vile hana pesa kwa Sasa angelifanya, nikamwambia mzee usipate shida hizi gari kwanza tuziuze halafu mimi naenda kukopa bank nikupe pesa najua ukiwa na miradi wadogo zangu watasoma, hapa nyumbani watakula bila hivo Mimi mwenyewe sitoweza kuhudumia familia yote hii ikiwa na mimi nina mke na mtoto sasa, mzee akanipa uhakika kabisa na kuniahidi nikashampa pesa nitakazokuwa nimekopa kila mwezi atanitumia pesa itakayotokana na faida ya miradi atakayofungua ili na Mimi niweze kumudu gharama za maisha, nikamwambia haina shida baba, usiku huo nikaenda kukata tiketi na kesho asubuhi nikasafiri kurudi kwangu kuchukua baadhi ya document ili nianze taratibu za kuomba mkopo, nilifanikiwa kuomba mkopo wa 24m ambao ningekatwa kwa kipindi Cha miaka 5 nikarudi arusha nikawa nasubiri mkopo uingizwe kwenye account.

Ni siku mbili zilikuwa zimepita nilikuwa sijamshirikisha mama nini nimeongea na baba, na baba pia hakumwambia mama.. nilivomweleza mama akashtuka, akasema pesa mpe ila usimpe pesa zote hizo kwa tahadhari, mimi nikapingana sana na mama nikamuona kama hapendi nimpe baba pesa, baada ya mabishano mama hakuwa na lingine zaidi ya kuniambia "sawa endeleeni". Nilibaki pale nyumbani ili nihakikishe namkabidhi pesa baba mbele ya familia kabla sijaondoka kurudi kazini.

Baada ya wiki3 nilipigiwa simu na watu wa bank kuelezwa pesa yangu ishaingizwa kwenye account yangu , nikaenda kuchukua niliporudi nyumbani nikamkibidhi baba 19mill. Mbele ya familia na kipindi hicho alikuwa ameuza gari zake 2 kwa jumla ya Tsh 12mill. Hivyo akawa na 31mill. Watoto walikuwa wanadaiwa Ada akatoa palepale 4m akampa mama akawalipie shuleni mmoja alikuwa kidato Cha tatu mwingine mwingine Cha kwanza, hivyo akabaki na 27mil.

Kesho asubuhi, mzee aliondoka kwenda shinyanga tayari kuanza taratibu za kufungua miradi yake Kama tulivokubaliana na Mimi nikaondoka kurudi kazini na mke wangu nikiwa na 4.6mill nilizobaki nazo, nilipofika Wala sikutaka kumsumbua mzee nilikaa kimya ili nimpe mda aandae mipango yake vizuri, baada ya kuwa nimekaa na ile 4.6mill kwa MDA na nisijue niifanyie nini mke wangu akanishauri tutafte kiwanja na akanishauri kwa sababu mzee ni mzoefu nimtumie pesa atununulie, nikaongezea 1.4m ikawa 6m nikamtumia ili atununulie viwanja viwili vya 3m kila kimoja, nikampa mapendekezo yangu nataka kiwanja kimoja kiwe shinyanga kingine mwanza Basi baada ya mda akaniambia ashanunua nikamwambia basi naziomba hati nizikute nyumbani kwa mama... Hapa ndipo matatzo yalipoanza anza.

Hati zikapelekwa nyumbani kwa mama kupitiwa moja inaonesha shamba limenunuliwa heka laki nne mwanza, kiwanja kingine shinyanga 1.5m imelipwa 1m deni laki5 halafu vyote majina ni ya baba na si yangu kumuuliza baba imekaaje akasema mradi ulikula pesa nyingi hivyo aliongezea kule na kuhusu majina haina shida, sikuwa na wasiwasi kabisa kwa sababu yule ni baba tena mzazi... Kadri siku zinavyoenda mzee Yuko kimya haniambii maendeleo ya uwekezaji Wala mama hajui kinachoendelea, Kuna siku alinipigia simu akanieleza uwekezaji umekamilika asilimia kubwa ila amepungukiwa na 2m nikatafta na zilizopungua nikakopa kwa watu binafsi kwa riba nikamtumia.

Siku zikaenda, nyumbani mama wanalia hali ngumu wananiomba niwatumie pesa na Mimi linapokuja suala na nyumbani na familia sijiulizi Mara mbili mbili Kama nina pesa, nikawatumia. Lakini nikataka kufahamu ni kivipi mzee asitume matumizi wakati alichukua pesa kwenda kufanya uwekezaji, nikamuuliza mzee anasema uwekezaji ndio umeanza faida bado ndogo ikabidi niwe mpole na kwa changamoto za biashara zilivyo sikuweza kubishana nae ilibidi niwe mpole....huko shinyanga mzee alikuwa tayari amenunua kiwanja mjini hivyo Kama ni suala la uwekezaji wa biashara hakuhitaji eneo tena.

Kuna siku mama alinipigia simu, baada ya kusalimiana akaanza kunieleza "Baba yako alikuja kuchukua ile hati ya kiwanja Cha shinyanga akisema inahitajika manispaa, lakini Kuna watu wameniambia huko amejenga nyumba na sehemu za biashara halafu kuna hawala yake alikuwa bamedi huku kamhamishia hapo na kamumilikisha nyumba na kampa hiyo hati" haya maneno yalikuwa mazito Sana kwenye masikio yangu kwanza sikutaka kuyaamini nikamwambia "mama wewe acha wivu baba hawezi kufanya hivo anatupenda Sana yaani huthamini hata juhudi zake kipindi kile akiwa fukara anashindia juani kwa ajili yetu tupate kula, baba ana akili timamu hawezi kufanya hivo, huo ni wivu tu hebu kaa mama angalia familia inakutegemea Sana usiweze kuyumba kwa vitu visivyo na ukweli" mama akaendelea kunisisitizia huo ndio ukweli na nikiukataa siku Moja nitakuja kuujua, baada ya kuagana na mama nikapuuzia yale maneno yake na Wala sikutaka hata kuulizia hiyo habari na hata sikuweza kumuuliza mzee mwenyewe kwanza naanzia wapi.

Siku zilivokuwa zinaenda sioni mrejesho mwaka ukapita na mimi niko mbeya kikazi, wadogo zangu wakafunga shule mmoja ndo akawa anaingia kidato Cha nne mwingine Cha pili, nikampigia simu baba kuhusu ada za watoto wakifungua shule, hapa ndipo nilipogundua kuna hali ya utofauti alinijibu, " Sina pesa warudie madarasa" nikamuuliza ina maana hayo madarasa wanarudia bure, mzee akasema yeye hana pesa na hataki kusikia hiyo habari..nikahisi kichwa kuanza kuniuma Sasa na jasho kuanza kunitoka taratibu, sikutegemea majibu Kama haya kutoka kwa baba, baada ya mda nikakumbuka Kuna viwanja vyangu viko huko nilimuagiza aninunulie nikampigia tena kumuomba aniuzie hivyo viwanja ili anitumie pesa nikalipe ada za wadogo zangu, akajibu sawa lakini viwanja viliuzwa na sikuambulia kuiona hata Mia tano yake.

Ikabidi nianze kufuatilia kwa ukaribu zaidi, nikagundua kupitia kwa baba wadogo na mashangazi kweli mzee ana mke walikutana baa kipindi mke akiwa mhudumu wa baa na ni mwenyeji wa njombe na hadi wao huwa wanawasiliana nae, ( nikayakumbuka maneno ya mama) na huko shinyanga kajengewa nyumba tena kwa pesa zangu na miradi kafunguliwa kwa pesa zangu na hata viwanja vyangu vimeuzwa pesa kachukua yeye na wamefanya uwekezaji wa mashamba ya miti ya mbao njombe.., hapa niliishiwa nguvu kabisa ila sikuwa na Cha kufanya..Akili yangu ikawa inawaza ni namna gani nitapata ada za watoto shule, mungu ni mwema nilifanikiwa kuwalipia na Mimi kwa mda wote sikuwahi kumchukia mzee nilijua ni makosa ambayo kila mtu anayafanya.

Mdogo wangu wa kidato Cha nne alimaliza shule na akafaulu kwa daraja la kwanza akapangiwa kilakala, ilibidi nirudi mijini kufanya maandalizi ya yeye kwenda Advance nikamkuta baba yupo nikatoa laki6 na kwa vile baba alikuwepo na yeye alisema atampeleka shule Mimi nikawaacha nikarudi kazini, Cha kushangaza baada ya miezi kadhaa napigiwa simu na mdogo wangu akinieleza anadaiwa Ada maana hajalipa hata shilling moja wakati baba alinithibitishia ashalipa, ilibidi nimpigie baba kupata ukweli akaniambia kulikuwa Kuna michango mingi, hivyo alinunua vifaa tu, na nguo,ada pesa ilipungua...sikutaka kubishana kwa sababu najua yeye ni mzazi lakini niliona kabisa baba kapeleka ile pesa kwa mama mdogo,...nilichofanya ni kumwambia mdogo wangu anipe namba ya mwalimu anaemuamini ili mimi nimtumie na nikafanya hivo na Ada ikalipwa pamoja na michango.

Ikabidi nianze kufikiria namna ya kuweka kitega uchumi pale nyumbani ili familia iweze kujimudu kwa matumizi madogo madogo, kwa vile pale nyumbani Kuna mafrem nikamfungulia mdogo wangu anaenifuata ( aliyegoma kusoma) restaurant, huyu japo alikataa kwenda shule ila alikuwa na akili ya biashara na utafutaji..aliiendesha vizuri sana ile restaurant na akawa anapata pesa sana, baba akaanza kumdai Kodi na kweli akawa anamlipa baada ya mda akamfukuza akasema hataki kumuona hapo kwake akiendesha biashara anataka kupangisha frem zake hata nilipojaribu kumshauri hakunisikiliza ikawa ni fujo na vurugu kila siku akiwepo baba nyumba inakuwa ya Moto kwelikweli, hakuna wa kumshauri si ndugu zake, marafiki Wala majirani na Wala familia yake ilibidi mdogo wangu aondoke na mtaji ukafa wa zaidi ya 1m+ na frem hazina mtu mpka leo.

Hapa nikawa na mzigo mkubwa sana watoto wanasoma private mmoja ndio yuko advance serikalini na mimi ndio kwanza mshahara wangu una mkopo na nyumbani wananitegemea mimi kwa matumizi ya kawaida ya kila siku na kila nikiwawekea miradi baba inaivuruga inakufa.

Baada ya mda nilianza kupata pesa nyingi tu hivyo nikawa stable kiuchumi swala la Ada kwa watoto shule halikuwa tatzo tena, pale nyumbani ile nyumba mzee aliyojenga zamani kwa kuunga unga nikaaanza kuikarabati kulikuwa na wapangaji wanapangisha elfu15 kwa mwezi nikawalipa siku zilizobaki wakaondoka nikaanza kuifanyia matengenezo, ilinigharimu zaidi ya 28m mpaka ile nyumba inakuwa ya kisasa kabisa, Sasa Cha kushangaza baba anapangisha chumba Sasa kwa Tsh elfu60 kwa mwezi kwa vyumba vinane na mafrem yake manne lakini hatoi hata pesa ya kununulia chumvi pale nyumbani wala kuwatumia wadogo zangu wanaosoma pesa za matumizi, inanilazimu niwatumie mimi yet akishachukua kodi anaenda kuzipeleka kwa mke mdogo shinyanga na Mimi yule baba yangu siwezi kubishana nae inanibidi ninyamaze tu na pale nyumbani nilitenga chumba na sebule master nikakitengeneza vizuri Sana kuliko vyumba vyote kwa ajili ya kuwa nakaa ninapokuwa nyumbani na nikaweka kila kitu bado akawa ananiambia nikatoe vyombo apangishe.

Baba alipoona nimemaliza kukarabati ile nyumba akajua mama yangu anafaidi zaidi labda namtumia pesa nyingi akaanza kutoa maneno makali Sana, ambayo yalinishtua Sana maana baba sikuwahi kumuona Wala kumsikia hivi.., anafikia kuwaambia watu kwamba ni " Bora kijana wangu afe au agongwe na gari tukose wote na mama yake" maneno yaliniiumiza Sana ikizingatia nafanya kila niwezalo familia isimame na Iwe na amani pamoja na kwamba Mimi mwenyewe bado sijajenga nimebahatika kununua viwanja 6 tu na vyote vikiwa tupu ila familia nilitaka iishi sehemu salama akiwemo, Maana pamoja na makosa yake ila sikuwahi kumsemesha Wala kumwambia Jambo baya naogopa kwa sababu Mimi bado ni mtoto kwake vyovyote itakavyokuwa, ila kwa Sasa amekuwa akisema waziwazi hatambui familia yetu anatambua nyumba ndogo hiyo ya shinyanga, na Kuna maneno anaongea kwamba Kuna siku atamuua mama yangu na yeye ajiue ama auze nyumba ( hili nilimkatalia waziwazi)au aichukulie nyumba mkopo halafu asiulipe ije iuzwe na bank, nimejaribu kumuuliza Mara kadhaa kutokana na hizi kauli Kali kutoka kwake lakini anakuwa mkali anasema tunashirikiana na mama kutaka kumuua, namuuliza baba Mimi nawezaje kukuuwa wewe? Anasema Mimi nitazaa wengine nyie sio wanangu na anaongea waziwazi kwamba yeye anatambua familia ya huyo mama mdogo wa shinyanga, kwa Sasa wamefanikiwa kupata mtoto mdogo ana miezi 2 na pia huyo mwanamke alikuwa na mtoto mkubwa tu yuko kidato Cha pili Sasa kabadilishwa jina anatumia jina la baba yangu Kama baba yake mzazi na baba anadai ile ndio familia yake.

Hapa katikati Kuna duka nilimfungulia mama Kuna siku mteja aliagiza soda mama akawa anamchukulia kwenye friza ghafla tu alipofungua akiwa hata hajaingiza mkono kwenye friji chupa mbili zilizokuwa kwenye friza chini zikapasuka bila kuguswa na zikamchana mama vibaya Sana usoni nilipigiwa simu nikiwa mbeya walimpeleka hospital na baada ya miezi miwli alipona, haikukaa mda ikatokea radi usiku tena bila mvua ikapiga upande wa dirisha wa chumba anacholala mama kwa bahati kabla ya dirisha kulikuwa na mnazi nje hivyo ikapiga mnazi, mnazi ukaanguka na kuungua nilivopigiwa simu ilibidi niombe ruhusa niende nyumbani kufika nikakuta watu wako nyumbani wanadiscuss lile tukio baba hakuwepo alikuwa shinyanga, alikuja baada ya wiki maana ilibidi nimsubiri tuzungumze kwa vile halikuwa Jambo la kawaida, kufika akakuta tupo na baadhi ya ndgu akasema " atajua mwenyewe, hayo Mimi hayanihusu" ilibidi kila mtu ashangae hata mimi nilishtuka kidogo nilikaa wiki moja halafu tukafanya maombi nikarudi kuendelea na kazi.. hata wiki haikuisha mama akaanza kuumwa na kwa vile Wazazi wangu Wana bima ilibidi niagize apelekwe hospitali wakaanza kumpeleka dispensary kila wakipima hawaoni ugonjwa na wanampa dawa za maumivu tu ambazo haikuwa zinamsaidia, wakampeleka hospitali kubwa nako kila wakipima hawaoni ugonjwa, ya mkoa nayo hivo hivo lakini akawa analalamika maumivu makali Sana na mwili Kama unawaka Moto, nikawaamuru wamsafirishe wampeleke muhimbili nako baada ya vipimo majibu yalikuwa hana ugonjwa, lakini kila siku alikuwa halali kwa kuugulia maumivu hali ilinifanya kutokuwa sawa kiakili, nikaomba ruhusa ili nikajiridhishe mwenyewe nilipofika nikampeleka tena hospitali nikapewa majibu yaleyale,.. tukageukia makanisani bado hakupata unafuu ndio hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya.., ikabidi nianze kutafta mawazo mbadala kwa wazee ( kipindi hiki mzee yuko shinyanga, yeye anapiga simu tu kuulizia) nilifika point kila mtu anaeniambia flani anaponya Mimi nampeleka mama kuona Kama anaweza kupata unafuu, Kuna kijana mmoja alikuja kumuangalia mama akaniambia huyu Kuna mtu pale tanga mjini nakuelekeza nenda atakusaidia, sikuwa na Cha kuuliza tena nilichohitaji mama arudi katika Hali ya kawaida tu akanipa namba ya huyo mtaalamu wa jadi siku hiyo hiyo nikaenda ubungo kupanda tashriff kwenda tanga nikiwa na mama tulifika salama yule mtaalam alimwangalia mama, huku Mimi hata nikiwa simuamini amini kwanza alikuwa bado msichana ni Kama 35+aged na mm najua nikisikia mganga Basi awe mzee, akaniagiza vitu vya kununua Mimi sikuwa mwenyeji tanga na nilivyoagizwa sikuvijua ilibidi nitoe pesa Kama 40elfu vikanunuliwe....akaanza kumfanyia dawa usiku huo baade nikamchukua mama nikampeleka hotelini kulala ( jina nadhani mtendele) karibu na nyinda, kesho yake mama akasema anasikia nafuu, ikawa ni Safari ya kwenda kwa mganga na kurudi hotelini mama alikuwa hatembei akilalamika miguu inawaka Moto lakini baada ya siku 2 akaanza kutembea mwenyewe na baada ya wiki moja mama akawa amepona kabisa, na yule mganga akahitaji elfu30 tu. Nikawa nimerudi na mama akiwa mzima mpaka Leo hajawahi kuumwa.

Baada ya kurudi na mama kutoka tanga na Mimi kazini nikapata barua ya uhamisho kwenda Arusha kikazi ambako ndio nyumbani,Sasa hapa kiuchumi sikuwa vizuri, mdogo wangu aliyekuwa advance ashamaliza anatakiwa kwenda chuo, na aliyekuwa Olevel alimaliza na matokeo hayakuwa mazuri nikampeleka chuo SAUT akasome diploma ya uandishi wa habari aliyochagua hivyo pesa karibu yote ya uhamisho niliitumia kwa ajili ya mahitaji Yao ya shule na ada,na mwingine ndo yupo bado Olevel ( private) ikanibidi niongee na mzee nirudi nyumbani kwa mda nikiwa najipanga maana pale nilitenga vyumba vyangu vikiwa na kila kitu na huku mimi nikiwa Sasa tayari nina watoto wawili mmoja akiwa na miaka6 Sasa na mdogo miaka 4, nilipofika pale nyumbani kimakazi nikakuta kuna kesi serikali za mitaa ikijiandaa kwenda polisi ambayo mimi binafsi sikuwa naijua Wala sikuwahi kuambiwa na mtu yeyote wa familia yangu, kesi yenyewe ni hii.
Mita chache kutoka pale nyumbani Kuna kanisa pamoja na kwamba linatoa huduma lakini bado lipo kwenye ujenzi, siku moja mchungaji alinunua vifaa vya ujenzi Kama mabati, nondo na vingine vinavyohusiana na ujenzi akaona kwa usalama aviweke pale nyumbani ikabidi aongee na baba na KWELI alimhakikishia usalama kabisa wa vifaa vyake ikabidi mchungaji aviweke pale., Baada ya siku kadhaa mzee alikodi gari akapakia vile vifaa vyote tayari kwa kwenda kuviuza,na alivizia watu wakiwa hawapo na hakuna aliyefahamu kwa wanafamilia zaidi ya wapangaji ndio walio muona na akawaambia anaenda kuezeka nyumba yake mpya anayojenga na wale wapangaji walijua yale mabati ni yake, baada ya siku kadhaa mchungaji akataka vifaa vyake ili aendelee na ujenzi mama alipoenda kufungua stoo hakukuta hata kifaa kimoja hapa ikawa mshikemshike MPAKA pale wapangaji waliposema, alipoulizwa baba akawa mkali na kutoa matusi kwa mchungaji na mama na kesho yake akaondoka kwenda shinyanga ikabidi mchungaji achukue hatua za kisheria, na mama akawa anasumbuliwa na kuitwa kuelezea serikali za mitaa ilivyokuwa wakati mzee hayupo, nilipofika nyumbani na kuikuta Hali ile ilibidi nimuite mchungaji nimuombe anipigie gharama ili nione namna ya kumlipa ili kuachana na ile kesi ambayo ni Kama ilikuwa inaidhalilisha familia pale mtaani, akaniletea risit za vifaa ambazo kwa ujumla wake ilikuwa Kama 3+mill, ambayo mama alithibitisha ni KWELI tulikubaliana nimlipe kidogokidogo kwa mda wa miezi 4 kitu ambacho alikubali na nikalimaliza Deni na amani ikarejea na kesi pia ikaisha

Baada ya siku kadhaa tangu nihamie pale nyumbanimzee kila siku akaanza Kuwa ananifukuza nitoke kwake apangishe chumba, tena kwa fujo Sana, na hata akiwa hayupo akirudi tu kutoka shinyanga anadai niondoke, wakati Mimi ndio nahudumia mahitaji muhimu yote ya nyumbani, yaani yeye alishasema hanunui hata chumvi. Ananiambia nitoke japo hata nyumba Mimi ndio nimeirekebisha..na Mimi sishindwi kutoka uwezo ninao wa kupanga na kuishi vizuri kabisa na familia yangu tatzo nilihitaji kupunguza gharama ili niwagharamie wadogo zangu wamalize chuo au pale nitakapoona nina uwezo wa kuwahudumia nyumbani, Ada za wadogo zangu na mimi kulipia nyumba kwa wakati mmoja ndio niondoke ili isifike sehemu wadogo zangu wakakwama. Imekuwa ni kelele mtindo mmoja mpka Kuna mda nahisi baba kalogwa, kwa mambo ninayofanya ilitakiwa anisapoti, lakini kwa nini anifukuza na kunichukia kiasi hiki wakati mimi ni mwanae, na sio mimi tu familia nzima hata ndgu zake wakati hakuwa hivi..? Na ikiwa pesa za wapangaji anachukua zote anapeleka shinyanga kwa nyumba ndogo na hakuna anaemuuliza na Mimi nilimwambia mama Wala asimuzuie.

Ndgu wanahisi mzee amepewa ndumba( limbwata) Kuna siku walikuwa wanagombana na ndgu yake mmoja na sisi watoto tukiwepo, yule ndgu yake akamwambia wewe hiyo sio akili yako ushapewa midawa tayari...mzee akajibu, hakuna wa kunipa dawa, Kama kuna mtu kanilisha limbwata ni mama flani ( anamtaja mama yangu)

Ungekuwa wewe ungefanyaje kwa Hali Kama hii, nishauri yawezekana nikajua Cha kufanya akili yangu imekuwa na msongo wa mawazo Sana japo nimepata mwanamke kiukweli ananisapoti Sana na namshukuru mungu kwa kunipa mke Kama huyu amekuwa faraja kwangu, kwa mama yangu, wadogo zangu na hata kwa ndugu zangu.. Baba pamoja na fujo zake zote za kutufukuza, matusi na kila Aina ya maudhi lakini bado haoneshi utofauti tena ndio amekuwa mstari wa mbele kunisisitizia niisaidie familia nilimfungulia biashara lakini asilimia kubwa anapigana kuwasaidia wifi zake wafikie mlaengo, ukifika nyumbani bila kuambiwa ni mke wangu utajua ni mdogo wangu.., maana mawifi zake wanavyoishi ni Kama dada zake, hata mama yangu wanachukuliana Kama mtu na mwanae wa kumzaa..

Ungekuwa wewe ndio Mimi kwenye familia ya baba Kama huyu, ungefanyaje
Duh pole sana kaka huyo mzee wako sio akili yake kabisa atakua kalogwa
 
Ahsante Sana mkuu Lucas, ushauri wako ni mzuri Sana lakini kwa ufupi vikao vishakalika vingi Sana vya ukoo, kwa Sasa asilimia kubwa ya ndugu hawaelewani na baba yangu na hana rafiki sasa wa kumfuata akamshauri wote wanatukanwa, kwa lugha mzee hashauriki kwa lolote lile

Sasa wewe kuwa kama mzazi au Mungu. Majuzi mtoto wangu alikuwa ananing'inia kwenye dirisha anaigiza ukonda wa daladala. Niliona hatari nikamuonya mara nyingi. Nikimtimua anarudi. Nikaamua kumuacha ili ajifunze kutokana na madhara. Alianguka. Kishindo kilinishtua na katumbo kakakata lakini lakini nikajidai sijali. Kakajikaza kasilie, kakagugumia maumivu halafu kakaja kuomba msamaha. Sasa wewe umeshajitahidi vya kutosha kumrudisha huyo mtu kwenye mstari tena kwa unyenyekevu mkubwa. Kwa sasa hakuna kitakachomrudisha baba yako zaidi ya ulimwengu aliouchagua. Muache huko ulimwenguni. Ulimwengu utashughulika naye, kisha atajirudi au atashupaza shingo (siombi afikie mwisho bila kubadilika). Tatizo lako ni moja tu. Unajiunganisha na matatizo ya baba yako. Huyo ni mtu mzima ameamua kufanya uchaguzi wake. Hutakiwi kujiona mnyonge kwa uchaguzi wake. Ulifanya zamu yako kwa uaminifu. Achana na baba yako. Kama una imani mwambie Mungu nimekuachia na uwe na amani ili uweze kuzingatia maisha yako. Huyo mzee maisha yake ameshayaishi kaona mpaka wajukuu. Muache. Ukiona anapigika vumilia usijidai mwokozi. Wewe chukua somo lako kwenye maisha yake na yote uliyopitia usonge mbele. "Ajionaye amesimama aangalie asianguke". Kumbuka hili usije kuwa kama baba yako kwa mkeo.
 
duh! sijui hata niseme nini, huyo mzee amelogwa tena sio na wachawi, kalogwa na shetani mwenyewe. pole sana ndugu yangu. Jenga nyumba sehemu nyingine uhamishe familia nzima muachieni huyo mzee na hiyo nyumba anayoona yake. Dunia itamfunza
 
Ushauri wangu kwako ni huu, andaa mchongo, m'bambikie kesi huyo mzee apigwe mvua ya kutosha not less than 3yrs, google sheria za makosa ya jinai uone itakayokupendeza ya miaka tajwa hapo juu, akiwa jela sasa, nenda shinyanga angalia km kuna masalia yoyote beba ila aliyompa kimada kisheria mwachie usimuulize then rudi A town, uza hiyo nyumba na mnunue nyumba nyingine muishi na mama na wadogo zako kwa amani na upendo. Akija kutoka jela nadhani mtakuwa mmesha move on kitaaambo! Perhaps na nyumba ndogo atamkuta kishaolewa na kidume kingine, atabaki yeye na pu*** zake tu zinamning'inia. Akija kwenu mtimueni na mumpige matukio mpaka awe kichaa akafie milembe!!!
Haahahah
 
Siku yingine fupisha kidogo story. Kifupi wasomaji wa JF si wenye nia ya kusoma gazeti refu, hivyo unaweza kuwa na hadithi nzuri lakini usipoifupisha hutawafikia wasomaji wako. Binafsi nilipofika nusu nguvu ikaniishia. Asante.
 
Hata hii comment usingetakiwa uandike, unataka kumpangia mleta Uzi maneno ya kuandika kwa uvivu wako mwenyewe.......
 
Habari za jioni Wana forum, nimeleta kwenu changamoto yangu angalau nipate busara zenu za kiushauri, najua humu Kuna watu wazima, wenye busara, hekima na waliopitia changamoto mbalimbali za kimaisha nisingependa kuona vijana wenye mihemko ya matusi na wale wasio na busara kutumia Uzi huu kutoa matusi, masimango ama kejeli. Japo nimeandika kwa kirefu lakini ningeomba tusome ili muweze kunipa ushauri vizuri.

Mimi ndiye kijana pekee na wa kwanza ( 30aged kwa sasa) katika familia yetu ya watoto watano, wanne wote ni wa kike, binafsi naipenda Sana familia yangu, naipenda mno na kiukweli linapokuja suala la familia yangu huwa sina mjadala nipo tayari kufanya lolote ili tu iwe na furaha. Kwa miaka kadhaa familia inapitia changamoto kubwa Sana inayonifanya mda mwingine nimchukie Sana baba yangu, sikuwahi kuwaza kumchukia mzazi katika maisha yangu ila kiukweli baba yangu sijui ni nini kimemkuta.

Nimezaliwa na kukulia kijijini huko Shinyanga na wazazi wangu, huku maisha yetu yakitegemea zaidi kilimo Cha jembe, mwanzoni mwa miaka ya 2000 baba alisafiri kwenda Arusha kutafta maisha, akituacha Mimi, mama na wadogo zangu wanne kijijini mwaka uliofuata mama na wadogo zangu walimfuata baba huku Mimi nikibaki kwa bibi kijijini nikiendelea na masomo. Nilipomaliza elimu ya msingi niliungana na wazazi wangu Arusha, kiukweli maisha hayakuwa mazuri Sana japo baba alikuwa amenunua kiwanja na kuanza kujenga nyumba za kuunga unga ( chumba kimoja kimoja). Baba alikuwa mpiganaji Sana ambae hakupenda kuona watoto wake tukipitia magumu,..alipambana kwa kila namna ili tuweze kusurvive. Kwa kipindi hicho nilishuhudia baba yangu akijatahidi sana kuihudumia familia kwa kila alivoweza, alifanya kazi yoyote ilimradi apate pesa ya kuhudumia familia.

Baada ya kuhamia Arusha nilipelekwa kidato Cha kwanza shule ya kata, nikiwa kidato Cha pili maisha ya baba yalibadilika ( mifereji ya pesa ilianza kuonekana) akanihamisha nikapelekwa shule ya private ambako nilimalizia elimu yangu ya O'level, Nikafaulu kwenda Advance na baadae chuo nikisomea kozi ya uhandisi, kipindi hiki mzee wangu alikuwa ameshauaga umaskini alikuwa ashajenga nyumba nyingine nzuri tu pembeni mwa ile ya mwanzo ya kuunga unga iliyokuwa inajengwa kwa chumba kimoja kimoja ikiwa na vyumba 8 pamoja na gari 2 za kutembelea.

Baba yangu alibadilika Sana kwa kipindi kifupi baada ya pesa kuanza kumtembelea ilikuwa ni starehe na yeye, yeye na starehe na Wala hakutaka ushauri ilikuwa akipata pesa anachukua gari haonekani mpka ziishe akawa mzee wa totoz Sana, binafsi nilijaribu kumshauri awekeze miradi ya kumuingizia pesa zaidi but niliishia kutukanwa na kudhalilishwa, lakini mda mwingine nikawa nakumbuka mateso aliyopitia mzee kuzitafta pesa nikaona ni sawa tu acha ajilawaze kwa vile alikuwa anaipenda Sana familia yake, inakula vizuri watoto wote wanasoma private school kasoro wa kike anaenifuata mm ( yeye alikataa mwenyewe akisema hana akili ya kusoma).

Mwaka 2012 nilipata ajira serikalini, na kipindi hicho nilikuwa na mpenzi wangu aliyekuwa mjamzito akiwa anasoma ustawi wa jamii ngazi ya diploma mwaka wa mwisho, nilipopata kazi tu tulitambulishana na kuanza kukaa wote Kama mke na mme.

Nilipangiwa kazi mkoa tofauti na Arusha hivyo nilikuwa mbali na Wazazi kidogo lakini mda mwingi tulikuwa tunawasiliana, mipango mingi ya mzee kwa kipindi hiki akiwa ameanza kupata pesa alikuwa hanishirikishi hivyo nilikuwa nasikia tu baba yako kanunua hiki, kafanya kile mimi nilikuwa nikimpigia simu nampa moyo tu aendelee kupambana.

Nilimaliza mwaka sijarudi kuonana na Wazazi japo nilikuwa nawasiliana nao Sana, na mzee japo nilikuwa namshirikisha mipango yangu karibia yote nae akawa ananipa moyo nipambane nilipojaribu kumuuliza maendeleo yake hakuwa anaiweka wazi, japo kwa pembeni nikawa napigiwa simu na baba wadogo naelezwa baba kakutwa baa kanywa hajiwezi kaibiwa pesa, Mara anatembea na watoto wadogo rika za wadogo zangu bila kificho... Mzee ni mkali ilikuwa ni vigumu kwangu kumshauri masuala Kama haya, hivyo sikuwa na namna zaidi ya kutulia na kipindi hiki nyumbani ilikuwa ni vurugu kila siku mzee anaanzisha ugomvi tu, kiukweli nikaaanza kumuona baba akiwa amebadilika sana, nyumba ikaanza kuwaka Moto kukawa hamna amani tena hata marafiki zake, ndgu zake wakawa wanatukanwa maskini hawana hadhi ya kufuatana nae ikabidi nimpigie niongee nae Kama kijana wake mkubwa lakini niliishia kutukanwa Sana, sikuwa na namna zaidi ya kutulia.

Mzee akawa ni mtu wa matumizi bila mipango, hapa hata familia ( wadogo zangu) wakawa hawajaliwi tena siku moja mama akanipigia simu kunieleza hali na maisha aliyokuwa nayo baba kwa mda huo ( hii ilikuwa Mara ya kwanza mama kunipigia simu kunielezea masuala ya mzee), akaniambia mzee ana hali mbaya na pesa kwa mda huo sio Kama mwanzo hivyo maisha ya nyumbani kidogo sio mazuri, ilibidi nichukue likizo ya mwezi nirudi nyumbani kuongea na baba na kuona namna ya kuokoa jahazi.

Nilipofika nyumbani kwa kweli nilikuta hali ya uchumi sio nzuri kwa baba, mzee sio yule niliyemzoea akifika sehemu anachoma mbuzi mzima na kula na marafiki sio huyu tena, Tuliongea mengi na mzee na akawa anasema ni kipindi tu kimebadilika na pesa imekuwa ngumu tena kwa busara sana na akanipa wazo lake la biashara zuri sana nililipenda na nikaona Kama akilifanya kweli litazaa matunda na akadai ni kwa vile hana pesa kwa Sasa angelifanya, nikamwambia mzee usipate shida hizi gari kwanza tuziuze halafu mimi naenda kukopa bank nikupe pesa najua ukiwa na miradi wadogo zangu watasoma, hapa nyumbani watakula bila hivo Mimi mwenyewe sitoweza kuhudumia familia yote hii ikiwa na mimi nina mke na mtoto sasa, mzee akanipa uhakika kabisa na kuniahidi nikashampa pesa nitakazokuwa nimekopa kila mwezi atanitumia pesa itakayotokana na faida ya miradi atakayofungua ili na Mimi niweze kumudu gharama za maisha, nikamwambia haina shida baba, usiku huo nikaenda kukata tiketi na kesho asubuhi nikasafiri kurudi kwangu kuchukua baadhi ya document ili nianze taratibu za kuomba mkopo, nilifanikiwa kuomba mkopo wa 24m ambao ningekatwa kwa kipindi Cha miaka 5 nikarudi arusha nikawa nasubiri mkopo uingizwe kwenye account.

Ni siku mbili zilikuwa zimepita nilikuwa sijamshirikisha mama nini nimeongea na baba, na baba pia hakumwambia mama.. nilivomweleza mama akashtuka, akasema pesa mpe ila usimpe pesa zote hizo kwa tahadhari, mimi nikapingana sana na mama nikamuona kama hapendi nimpe baba pesa, baada ya mabishano mama hakuwa na lingine zaidi ya kuniambia "sawa endeleeni". Nilibaki pale nyumbani ili nihakikishe namkabidhi pesa baba mbele ya familia kabla sijaondoka kurudi kazini.

Baada ya wiki3 nilipigiwa simu na watu wa bank kuelezwa pesa yangu ishaingizwa kwenye account yangu , nikaenda kuchukua niliporudi nyumbani nikamkibidhi baba 19mill. Mbele ya familia na kipindi hicho alikuwa ameuza gari zake 2 kwa jumla ya Tsh 12mill. Hivyo akawa na 31mill. Watoto walikuwa wanadaiwa Ada akatoa palepale 4m akampa mama akawalipie shuleni mmoja alikuwa kidato Cha tatu mwingine mwingine Cha kwanza, hivyo akabaki na 27mil.

Kesho asubuhi, mzee aliondoka kwenda shinyanga tayari kuanza taratibu za kufungua miradi yake Kama tulivokubaliana na Mimi nikaondoka kurudi kazini na mke wangu nikiwa na 4.6mill nilizobaki nazo, nilipofika Wala sikutaka kumsumbua mzee nilikaa kimya ili nimpe mda aandae mipango yake vizuri, baada ya kuwa nimekaa na ile 4.6mill kwa MDA na nisijue niifanyie nini mke wangu akanishauri tutafte kiwanja na akanishauri kwa sababu mzee ni mzoefu nimtumie pesa atununulie, nikaongezea 1.4m ikawa 6m nikamtumia ili atununulie viwanja viwili vya 3m kila kimoja, nikampa mapendekezo yangu nataka kiwanja kimoja kiwe shinyanga kingine mwanza Basi baada ya mda akaniambia ashanunua nikamwambia basi naziomba hati nizikute nyumbani kwa mama... Hapa ndipo matatzo yalipoanza anza.

Hati zikapelekwa nyumbani kwa mama kupitiwa moja inaonesha shamba limenunuliwa heka laki nne mwanza, kiwanja kingine shinyanga 1.5m imelipwa 1m deni laki5 halafu vyote majina ni ya baba na si yangu kumuuliza baba imekaaje akasema mradi ulikula pesa nyingi hivyo aliongezea kule na kuhusu majina haina shida, sikuwa na wasiwasi kabisa kwa sababu yule ni baba tena mzazi... Kadri siku zinavyoenda mzee Yuko kimya haniambii maendeleo ya uwekezaji Wala mama hajui kinachoendelea, Kuna siku alinipigia simu akanieleza uwekezaji umekamilika asilimia kubwa ila amepungukiwa na 2m nikatafta na zilizopungua nikakopa kwa watu binafsi kwa riba nikamtumia.

Siku zikaenda, nyumbani mama wanalia hali ngumu wananiomba niwatumie pesa na Mimi linapokuja suala na nyumbani na familia sijiulizi Mara mbili mbili Kama nina pesa, nikawatumia. Lakini nikataka kufahamu ni kivipi mzee asitume matumizi wakati alichukua pesa kwenda kufanya uwekezaji, nikamuuliza mzee anasema uwekezaji ndio umeanza faida bado ndogo ikabidi niwe mpole na kwa changamoto za biashara zilivyo sikuweza kubishana nae ilibidi niwe mpole....huko shinyanga mzee alikuwa tayari amenunua kiwanja mjini hivyo Kama ni suala la uwekezaji wa biashara hakuhitaji eneo tena.

Kuna siku mama alinipigia simu, baada ya kusalimiana akaanza kunieleza "Baba yako alikuja kuchukua ile hati ya kiwanja Cha shinyanga akisema inahitajika manispaa, lakini Kuna watu wameniambia huko amejenga nyumba na sehemu za biashara halafu kuna hawala yake alikuwa bamedi huku kamhamishia hapo na kamumilikisha nyumba na kampa hiyo hati" haya maneno yalikuwa mazito Sana kwenye masikio yangu kwanza sikutaka kuyaamini nikamwambia "mama wewe acha wivu baba hawezi kufanya hivo anatupenda Sana yaani huthamini hata juhudi zake kipindi kile akiwa fukara anashindia juani kwa ajili yetu tupate kula, baba ana akili timamu hawezi kufanya hivo, huo ni wivu tu hebu kaa mama angalia familia inakutegemea Sana usiweze kuyumba kwa vitu visivyo na ukweli" mama akaendelea kunisisitizia huo ndio ukweli na nikiukataa siku Moja nitakuja kuujua, baada ya kuagana na mama nikapuuzia yale maneno yake na Wala sikutaka hata kuulizia hiyo habari na hata sikuweza kumuuliza mzee mwenyewe kwanza naanzia wapi.

Siku zilivokuwa zinaenda sioni mrejesho mwaka ukapita na mimi niko mbeya kikazi, wadogo zangu wakafunga shule mmoja ndo akawa anaingia kidato Cha nne mwingine Cha pili, nikampigia simu baba kuhusu ada za watoto wakifungua shule, hapa ndipo nilipogundua kuna hali ya utofauti alinijibu, " Sina pesa warudie madarasa" nikamuuliza ina maana hayo madarasa wanarudia bure, mzee akasema yeye hana pesa na hataki kusikia hiyo habari..nikahisi kichwa kuanza kuniuma Sasa na jasho kuanza kunitoka taratibu, sikutegemea majibu Kama haya kutoka kwa baba, baada ya mda nikakumbuka Kuna viwanja vyangu viko huko nilimuagiza aninunulie nikampigia tena kumuomba aniuzie hivyo viwanja ili anitumie pesa nikalipe ada za wadogo zangu, akajibu sawa lakini viwanja viliuzwa na sikuambulia kuiona hata Mia tano yake.

Ikabidi nianze kufuatilia kwa ukaribu zaidi, nikagundua kupitia kwa baba wadogo na mashangazi kweli mzee ana mke walikutana baa kipindi mke akiwa mhudumu wa baa na ni mwenyeji wa njombe na hadi wao huwa wanawasiliana nae, ( nikayakumbuka maneno ya mama) na huko shinyanga kajengewa nyumba tena kwa pesa zangu na miradi kafunguliwa kwa pesa zangu na hata viwanja vyangu vimeuzwa pesa kachukua yeye na wamefanya uwekezaji wa mashamba ya miti ya mbao njombe.., hapa niliishiwa nguvu kabisa ila sikuwa na Cha kufanya..Akili yangu ikawa inawaza ni namna gani nitapata ada za watoto shule, mungu ni mwema nilifanikiwa kuwalipia na Mimi kwa mda wote sikuwahi kumchukia mzee nilijua ni makosa ambayo kila mtu anayafanya.

Mdogo wangu wa kidato Cha nne alimaliza shule na akafaulu kwa daraja la kwanza akapangiwa kilakala, ilibidi nirudi mijini kufanya maandalizi ya yeye kwenda Advance nikamkuta baba yupo nikatoa laki6 na kwa vile baba alikuwepo na yeye alisema atampeleka shule Mimi nikawaacha nikarudi kazini, Cha kushangaza baada ya miezi kadhaa napigiwa simu na mdogo wangu akinieleza anadaiwa Ada maana hajalipa hata shilling moja wakati baba alinithibitishia ashalipa, ilibidi nimpigie baba kupata ukweli akaniambia kulikuwa Kuna michango mingi, hivyo alinunua vifaa tu, na nguo,ada pesa ilipungua...sikutaka kubishana kwa sababu najua yeye ni mzazi lakini niliona kabisa baba kapeleka ile pesa kwa mama mdogo,...nilichofanya ni kumwambia mdogo wangu anipe namba ya mwalimu anaemuamini ili mimi nimtumie na nikafanya hivo na Ada ikalipwa pamoja na michango.

Ikabidi nianze kufikiria namna ya kuweka kitega uchumi pale nyumbani ili familia iweze kujimudu kwa matumizi madogo madogo, kwa vile pale nyumbani Kuna mafrem nikamfungulia mdogo wangu anaenifuata ( aliyegoma kusoma) restaurant, huyu japo alikataa kwenda shule ila alikuwa na akili ya biashara na utafutaji..aliiendesha vizuri sana ile restaurant na akawa anapata pesa sana, baba akaanza kumdai Kodi na kweli akawa anamlipa baada ya mda akamfukuza akasema hataki kumuona hapo kwake akiendesha biashara anataka kupangisha frem zake hata nilipojaribu kumshauri hakunisikiliza ikawa ni fujo na vurugu kila siku akiwepo baba nyumba inakuwa ya Moto kwelikweli, hakuna wa kumshauri si ndugu zake, marafiki Wala majirani na Wala familia yake ilibidi mdogo wangu aondoke na mtaji ukafa wa zaidi ya 1m+ na frem hazina mtu mpka leo.

Hapa nikawa na mzigo mkubwa sana watoto wanasoma private mmoja ndio yuko advance serikalini na mimi ndio kwanza mshahara wangu una mkopo na nyumbani wananitegemea mimi kwa matumizi ya kawaida ya kila siku na kila nikiwawekea miradi baba inaivuruga inakufa.

Baada ya mda nilianza kupata pesa nyingi tu hivyo nikawa stable kiuchumi swala la Ada kwa watoto shule halikuwa tatzo tena, pale nyumbani ile nyumba mzee aliyojenga zamani kwa kuunga unga nikaaanza kuikarabati kulikuwa na wapangaji wanapangisha elfu15 kwa mwezi nikawalipa siku zilizobaki wakaondoka nikaanza kuifanyia matengenezo, ilinigharimu zaidi ya 28m mpaka ile nyumba inakuwa ya kisasa kabisa, Sasa Cha kushangaza baba anapangisha chumba Sasa kwa Tsh elfu60 kwa mwezi kwa vyumba vinane na mafrem yake manne lakini hatoi hata pesa ya kununulia chumvi pale nyumbani wala kuwatumia wadogo zangu wanaosoma pesa za matumizi, inanilazimu niwatumie mimi yet akishachukua kodi anaenda kuzipeleka kwa mke mdogo shinyanga na Mimi yule baba yangu siwezi kubishana nae inanibidi ninyamaze tu na pale nyumbani nilitenga chumba na sebule master nikakitengeneza vizuri Sana kuliko vyumba vyote kwa ajili ya kuwa nakaa ninapokuwa nyumbani na nikaweka kila kitu bado akawa ananiambia nikatoe vyombo apangishe.

Baba alipoona nimemaliza kukarabati ile nyumba akajua mama yangu anafaidi zaidi labda namtumia pesa nyingi akaanza kutoa maneno makali Sana, ambayo yalinishtua Sana maana baba sikuwahi kumuona Wala kumsikia hivi.., anafikia kuwaambia watu kwamba ni " Bora kijana wangu afe au agongwe na gari tukose wote na mama yake" maneno yaliniiumiza Sana ikizingatia nafanya kila niwezalo familia isimame na Iwe na amani pamoja na kwamba Mimi mwenyewe bado sijajenga nimebahatika kununua viwanja 6 tu na vyote vikiwa tupu ila familia nilitaka iishi sehemu salama akiwemo, Maana pamoja na makosa yake ila sikuwahi kumsemesha Wala kumwambia Jambo baya naogopa kwa sababu Mimi bado ni mtoto kwake vyovyote itakavyokuwa, ila kwa Sasa amekuwa akisema waziwazi hatambui familia yetu anatambua nyumba ndogo hiyo ya shinyanga, na Kuna maneno anaongea kwamba Kuna siku atamuua mama yangu na yeye ajiue ama auze nyumba ( hili nilimkatalia waziwazi)au aichukulie nyumba mkopo halafu asiulipe ije iuzwe na bank, nimejaribu kumuuliza Mara kadhaa kutokana na hizi kauli Kali kutoka kwake lakini anakuwa mkali anasema tunashirikiana na mama kutaka kumuua, namuuliza baba Mimi nawezaje kukuuwa wewe? Anasema Mimi nitazaa wengine nyie sio wanangu na anaongea waziwazi kwamba yeye anatambua familia ya huyo mama mdogo wa shinyanga, kwa Sasa wamefanikiwa kupata mtoto mdogo ana miezi 2 na pia huyo mwanamke alikuwa na mtoto mkubwa tu yuko kidato Cha pili Sasa kabadilishwa jina anatumia jina la baba yangu Kama baba yake mzazi na baba anadai ile ndio familia yake.

Hapa katikati Kuna duka nilimfungulia mama Kuna siku mteja aliagiza soda mama akawa anamchukulia kwenye friza ghafla tu alipofungua akiwa hata hajaingiza mkono kwenye friji chupa mbili zilizokuwa kwenye friza chini zikapasuka bila kuguswa na zikamchana mama vibaya Sana usoni nilipigiwa simu nikiwa mbeya walimpeleka hospital na baada ya miezi miwli alipona, haikukaa mda ikatokea radi usiku tena bila mvua ikapiga upande wa dirisha wa chumba anacholala mama kwa bahati kabla ya dirisha kulikuwa na mnazi nje hivyo ikapiga mnazi, mnazi ukaanguka na kuungua nilivopigiwa simu ilibidi niombe ruhusa niende nyumbani kufika nikakuta watu wako nyumbani wanadiscuss lile tukio baba hakuwepo alikuwa shinyanga, alikuja baada ya wiki maana ilibidi nimsubiri tuzungumze kwa vile halikuwa Jambo la kawaida, kufika akakuta tupo na baadhi ya ndgu akasema " atajua mwenyewe, hayo Mimi hayanihusu" ilibidi kila mtu ashangae hata mimi nilishtuka kidogo nilikaa wiki moja halafu tukafanya maombi nikarudi kuendelea na kazi.. hata wiki haikuisha mama akaanza kuumwa na kwa vile Wazazi wangu Wana bima ilibidi niagize apelekwe hospitali wakaanza kumpeleka dispensary kila wakipima hawaoni ugonjwa na wanampa dawa za maumivu tu ambazo haikuwa zinamsaidia, wakampeleka hospitali kubwa nako kila wakipima hawaoni ugonjwa, ya mkoa nayo hivo hivo lakini akawa analalamika maumivu makali Sana na mwili Kama unawaka Moto, nikawaamuru wamsafirishe wampeleke muhimbili nako baada ya vipimo majibu yalikuwa hana ugonjwa, lakini kila siku alikuwa halali kwa kuugulia maumivu hali ilinifanya kutokuwa sawa kiakili, nikaomba ruhusa ili nikajiridhishe mwenyewe nilipofika nikampeleka tena hospitali nikapewa majibu yaleyale,.. tukageukia makanisani bado hakupata unafuu ndio hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya.., ikabidi nianze kutafta mawazo mbadala kwa wazee ( kipindi hiki mzee yuko shinyanga, yeye anapiga simu tu kuulizia) nilifika point kila mtu anaeniambia flani anaponya Mimi nampeleka mama kuona Kama anaweza kupata unafuu, Kuna kijana mmoja alikuja kumuangalia mama akaniambia huyu Kuna mtu pale tanga mjini nakuelekeza nenda atakusaidia, sikuwa na Cha kuuliza tena nilichohitaji mama arudi katika Hali ya kawaida tu akanipa namba ya huyo mtaalamu wa jadi siku hiyo hiyo nikaenda ubungo kupanda tashriff kwenda tanga nikiwa na mama tulifika salama yule mtaalam alimwangalia mama, huku Mimi hata nikiwa simuamini amini kwanza alikuwa bado msichana ni Kama 35+aged na mm najua nikisikia mganga Basi awe mzee, akaniagiza vitu vya kununua Mimi sikuwa mwenyeji tanga na nilivyoagizwa sikuvijua ilibidi nitoe pesa Kama 40elfu vikanunuliwe....akaanza kumfanyia dawa usiku huo baade nikamchukua mama nikampeleka hotelini kulala ( jina nadhani mtendele) karibu na nyinda, kesho yake mama akasema anasikia nafuu, ikawa ni Safari ya kwenda kwa mganga na kurudi hotelini mama alikuwa hatembei akilalamika miguu inawaka Moto lakini baada ya siku 2 akaanza kutembea mwenyewe na baada ya wiki moja mama akawa amepona kabisa, na yule mganga akahitaji elfu30 tu. Nikawa nimerudi na mama akiwa mzima mpaka Leo hajawahi kuumwa.

Baada ya kurudi na mama kutoka tanga na Mimi kazini nikapata barua ya uhamisho kwenda Arusha kikazi ambako ndio nyumbani,Sasa hapa kiuchumi sikuwa vizuri, mdogo wangu aliyekuwa advance ashamaliza anatakiwa kwenda chuo, na aliyekuwa Olevel alimaliza na matokeo hayakuwa mazuri nikampeleka chuo SAUT akasome diploma ya uandishi wa habari aliyochagua hivyo pesa karibu yote ya uhamisho niliitumia kwa ajili ya mahitaji Yao ya shule na ada,na mwingine ndo yupo bado Olevel ( private) ikanibidi niongee na mzee nirudi nyumbani kwa mda nikiwa najipanga maana pale nilitenga vyumba vyangu vikiwa na kila kitu na huku mimi nikiwa Sasa tayari nina watoto wawili mmoja akiwa na miaka6 Sasa na mdogo miaka 4, nilipofika pale nyumbani kimakazi nikakuta kuna kesi serikali za mitaa ikijiandaa kwenda polisi ambayo mimi binafsi sikuwa naijua Wala sikuwahi kuambiwa na mtu yeyote wa familia yangu, kesi yenyewe ni hii.
Mita chache kutoka pale nyumbani Kuna kanisa pamoja na kwamba linatoa huduma lakini bado lipo kwenye ujenzi, siku moja mchungaji alinunua vifaa vya ujenzi Kama mabati, nondo na vingine vinavyohusiana na ujenzi akaona kwa usalama aviweke pale nyumbani ikabidi aongee na baba na KWELI alimhakikishia usalama kabisa wa vifaa vyake ikabidi mchungaji aviweke pale., Baada ya siku kadhaa mzee alikodi gari akapakia vile vifaa vyote tayari kwa kwenda kuviuza,na alivizia watu wakiwa hawapo na hakuna aliyefahamu kwa wanafamilia zaidi ya wapangaji ndio walio muona na akawaambia anaenda kuezeka nyumba yake mpya anayojenga na wale wapangaji walijua yale mabati ni yake, baada ya siku kadhaa mchungaji akataka vifaa vyake ili aendelee na ujenzi mama alipoenda kufungua stoo hakukuta hata kifaa kimoja hapa ikawa mshikemshike MPAKA pale wapangaji waliposema, alipoulizwa baba akawa mkali na kutoa matusi kwa mchungaji na mama na kesho yake akaondoka kwenda shinyanga ikabidi mchungaji achukue hatua za kisheria, na mama akawa anasumbuliwa na kuitwa kuelezea serikali za mitaa ilivyokuwa wakati mzee hayupo, nilipofika nyumbani na kuikuta Hali ile ilibidi nimuite mchungaji nimuombe anipigie gharama ili nione namna ya kumlipa ili kuachana na ile kesi ambayo ni Kama ilikuwa inaidhalilisha familia pale mtaani, akaniletea risit za vifaa ambazo kwa ujumla wake ilikuwa Kama 3+mill, ambayo mama alithibitisha ni KWELI tulikubaliana nimlipe kidogokidogo kwa mda wa miezi 4 kitu ambacho alikubali na nikalimaliza Deni na amani ikarejea na kesi pia ikaisha

Baada ya siku kadhaa tangu nihamie pale nyumbanimzee kila siku akaanza Kuwa ananifukuza nitoke kwake apangishe chumba, tena kwa fujo Sana, na hata akiwa hayupo akirudi tu kutoka shinyanga anadai niondoke, wakati Mimi ndio nahudumia mahitaji muhimu yote ya nyumbani, yaani yeye alishasema hanunui hata chumvi. Ananiambia nitoke japo hata nyumba Mimi ndio nimeirekebisha..na Mimi sishindwi kutoka uwezo ninao wa kupanga na kuishi vizuri kabisa na familia yangu tatzo nilihitaji kupunguza gharama ili niwagharamie wadogo zangu wamalize chuo au pale nitakapoona nina uwezo wa kuwahudumia nyumbani, Ada za wadogo zangu na mimi kulipia nyumba kwa wakati mmoja ndio niondoke ili isifike sehemu wadogo zangu wakakwama. Imekuwa ni kelele mtindo mmoja mpka Kuna mda nahisi baba kalogwa, kwa mambo ninayofanya ilitakiwa anisapoti, lakini kwa nini anifukuza na kunichukia kiasi hiki wakati mimi ni mwanae, na sio mimi tu familia nzima hata ndgu zake wakati hakuwa hivi..? Na ikiwa pesa za wapangaji anachukua zote anapeleka shinyanga kwa nyumba ndogo na hakuna anaemuuliza na Mimi nilimwambia mama Wala asimuzuie.

Ndgu wanahisi mzee amepewa ndumba( limbwata) Kuna siku walikuwa wanagombana na ndgu yake mmoja na sisi watoto tukiwepo, yule ndgu yake akamwambia wewe hiyo sio akili yako ushapewa midawa tayari...mzee akajibu, hakuna wa kunipa dawa, Kama kuna mtu kanilisha limbwata ni mama flani ( anamtaja mama yangu)

Ungekuwa wewe ungefanyaje kwa Hali Kama hii, nishauri yawezekana nikajua Cha kufanya akili yangu imekuwa na msongo wa mawazo Sana japo nimepata mwanamke kiukweli ananisapoti Sana na namshukuru mungu kwa kunipa mke Kama huyu amekuwa faraja kwangu, kwa mama yangu, wadogo zangu na hata kwa ndugu zangu.. Baba pamoja na fujo zake zote za kutufukuza, matusi na kila Aina ya maudhi lakini bado haoneshi utofauti tena ndio amekuwa mstari wa mbele kunisisitizia niisaidie familia nilimfungulia biashara lakini asilimia kubwa anapigana kuwasaidia wifi zake wafikie mlaengo, ukifika nyumbani bila kuambiwa ni mke wangu utajua ni mdogo wangu.., maana mawifi zake wanavyoishi ni Kama dada zake, hata mama yangu wanachukuliana Kama mtu na mwanae wa kumzaa..

Ungekuwa wewe ndio Mimi kwenye familia ya baba Kama huyu, ungefanyaje

Pesa huwa inabadilisha tabia zetu binadamu, binadamu akipata pesa majivuno na kiburi na kuona kwamba amekamilika na haifanyi kutoka kwa yeyote

Hapo la kufanya ni kuendelea kumnasihi mzee siku zote, pia usimpe pesa mpe pesa Mama maana kama hao wazee waliotoka nae tumbo moja familia moja wanachofanya ni kulalamika tu sidhani kama kuna Suluhu kutoka kwa watu
 
Pole sana mkuu haya mambo afadhali yako umetema nyongo ila yanazikumba familia nyingi sana hasa pale Baba anapoongeza mke changamoto huwa ni nyingi sana sababu idadi kubwa ya hayo unayoyapitia nimeyaishi kwa kitambo kirefu sana! Kiukweli kwa hapo alipofikia Mzazi wako kumbadilisha ni ngumu sana bila neema ya Mwenyezi Mungu! Ushauri wangu naona ni afadhali upige moyo konde kwa yote uliyoyafanya kwa manufaa ya familia yako upande wa Wazazi uhame tu kwanza hapo nyumbani bila kujali gharama Mungu atafungua milango! Mama usimshauri chochote pamoja na magumu anayoyapitia afanye kwa matakwa yake binafsi. Jitenge kwa muda na baba yako huku ukifuatilia yanayojiri chinichini kwani kwasasa hawezi kufanya lolote kuuza mali kama nyumba bila kumshirikisha mama hata kama atalazimisha mama akienda mbele ya sheria inarudi tuu! Hizi changamoto mkuu zinaleta shida sana hasa ukiwa na moyo mwepesi mkazie tuu mshua akili itamkaa sawa! Pole sana kwa yote unayoyapitia mtangulize Mungu pia akupe hekima na busara zaidi katika kulichukulia jambo hili
 
Aisee una moyo mgumu sana, umepoteza pesa nyingi sana kwa baba yako aisee. Angalau ungezitumia kuwaendeleza wadogo zako na familia yako ungekua mbali sana.
Kaa mbali na huyo mzee, muache avune kile anachokipanda, keshaingiliwa na roho mbaya na mwisho atawaua ninyi.
Unaweza ukiwa vzr mtumia mama za matumizi asihangaike pale nyumbani.
Yy kuwa mzazi tunashukuru, wapo wangapi hawajawahi ona wazazi wao na wana Amani ya maisha tu km watu wengine.
Mwisho tafuta kanisa la wokovu sali hapo ili nguvu za giza zishindwe. Kumbuka shetani anaisambaratisha familia.
Na kila mtu atavuna alichopanda.
 
Mwisho wa story nzima bado familia ina mgogoro,tena kiini cha mgogoro ni Mzee,da! Pole Sana.
Umeponzwa na yafuatayo;
*Mahaba na familia
*Huruma iliyopitiliza
*Kutokuwa na misimamo binafsi
*Heshima ya kike dhidi ya Mzazi ingali we ni mwanamme.
*Kuzarau mambo na kuchukulia mambo simple simple.
Well done my legendary for taking care your blessed family,God bless you Brother.
Du! Mzee anapasua kichwa balaa,nimejivisha kiatu chako,da! Kinabana Sana aiseeeeee,,,,,,.
Ushauri wangu:Vaa uanaume,Mzee ni kama wewe,ulichonacho ndicho anacho,alichojaaliwa ni nafasi aliyopewa ya kukuzaa tu,
Nenda kisheria hasa Kwa kushirikiana na mama,Mali zigawiwe baina ya pande mbili,afu kama kutokuwa na nyumba iuzwe kukaa mbali na mzee afu ununue sehemu ujenge huku ukiwa umepanga.
Najua ipo day atakuja,najua-najua believe me,ila mpaka abaki mweupe,Bola arudi akiwa anahitaji fadhira bila kitu atakuwa na nidhamu.
Pole Sana,jitahidi kuwa mwanamme.
Kumbuka:Kugombana na Baba ni suna ili kuwekana sawa,ila Kugombana na mama ni laana.Kwa mama ndo inapaswa ukae kimya ila sio Baba,Never ever.
 
Bro nakushaur kama mtu mzima niliyevuka 40
Kama unaweza kuanzisha makazi mapya anzisha kisha itoe familia yako kwenye mikono ya huyo mzee
Baada ya wewe kuondoka na kujiimarisha na mama yako na ndg sehemu mpya mzee atauza hizo nyumba hela atanpelekea mke mdogo
Baada ya hapo nakupa mwaka mmoja mzee atakuja anatembelea magoti kuomba msamaha maana kule atakuwa kafukuzwa
Ila mkiendelea kukaa hapo mnawwza kufanyiwa kubwa zaid ya kilichomkuta mama yako
Usigombane nae au kumjibisha we tafuta namna ya kujitegemea na kuanzisha maisha mapya na mamako ja wadogo zako
USHAURI BORAA KABISA HUU MLETA MADA UUSOME NA NINAKUSHAURI UUFUATE Mkuu
 
Pesa huwa inabadilisha tabia zetu binadamu, binadamu akipata pesa majivuno na kiburi na kuona kwamba amekamilika na haifanyi kutoka kwa yeyote

Hapo la kufanya ni kuendelea kumnasihi mzee siku zote, pia usimpe pesa mpe pesa Mama maana kama hao wazee waliotoka nae tumbo moja familia moja wanachofanya ni kulalamika tu sidhani kama kuna Suluhu kutoka kwa watu
Sio kweli Pesa inabadili tabia ya mtu.
Haijawahi hata sikumoja.

Ingekuwa ni hivyo basi huyu kijana angefanana na baba take au angemzidi baba yake.
(like father like son)

Iko hivi..
Pesa inachimbua tabia halisi ya mtu,
Haimbadilishi hata kidgo ila inazamaga chini na kuziibua juu tabia za mtu.

Mtu akiwa hana kitu hawezi akawa na ujasiri wakusema kitu mbele za watu,lkn akipata kitu(pesa)
Ndo utaona akisema,akitenda,
1: KATIKA USEMI wake ndo utagundua,ndani yake kunadharau,jeuri,kiburi,Chuki na majigambo mengi tofauti na wakati ambao hakuwa na pesa,
Lkn kuna wengine wana pesa chafu na hawana kabisa tbia km hizi..
2:KATIKA VITENDO.
Mtu akipata pesa utashuhudia kwa kiwango kikubwa,vitendo ambavyo hakuwahi kufanya kipindi kile ambacho hakuwa na pesa.Kama ni mtu wa bata,utamuona tu,
Uhuni,Kuongeza mke/ma dame,kunyanyasa wengine,kulala nje,na vitendo vingine vingi vinavyofanana na hivi.

Kwaio huyu mzee ni tabia yake kabisa,ila watoto hawakuwahi kuijua kipindi hana pesa ndio maana anasema kabadilika.

Kwaio tusiisingizie pesa kusema ina badili tba za watu No.
Haibadili ila inachimbua tabia halisi ya mtu.

Pole sana kwa mleta thread.
 
Umeponzwa na yafuatayo;
*Mahaba na familia
*Huruma iliyopitiliza
*Kutokuwa na misimamo binafsi
*Heshima ya kike dhidi ya Mzazi ingali we ni mwanamme.

Yeah, no wonder. Easy sana kutathmini matokeo ya ndondi. Si upo nje ya uzio?

Nukta zako 4 mkuu, zimejawa na kebehi, I beg to differ on that. Lakini nimehisi sana unavo mjali mleta uzi. Take some credit on it.
 
Back
Top Bottom