Huwa tunachukia bure tu, ila kosa ni sie wenyewe....

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
69,802
137,076
Boxing njema kwenu wote wenye mabox mie hata roll pop sijapewa.....

kuna siku tunakuaga na mood zaidi kuandaa chakula kizuri kwa ajali ya wenzi wetu, unapika kwa bashasha zote, mood nzuri, unapika unaandaa kuliko kawaida ukitegemea mtu ale, aenjoy yani mlaji nae awe na mood kama ya mpishi....bahati mbaya mambo yanakua tofauti mlaji badala ya kula anaonja tu vijiko vitatu ananawa kashiba aiseee mpishi lazma hasira zikushike, hata ukijichejesha usoni moyoni lazma kuna mnuno.....pamoja na maandalizi motomoto ushajiuliza mood ya mlaji? Yupo katikati mood ya kula hicho ulichokiandaa? Au unakasirika bure tu? Yeah tunakasirika bure tu....

Kuna siku niliandaa bana nilijikoki nilisweat nikapika chapati roast, chai ya maziwa ina iliki na juice mmh mlaji akala nusu chapati akasema kashiba nilikasirika na ni mara nyingi tu inatokeaga hivo

Jirani angu siku moja nkamcheki yupo bize anapika mtori anapika kwenye chungu (vilee vya udongo) yani mood ipo high imagine siku hiyo anapika kwenye chungu sio sufuria, mtori umeiva kampakulia jamaa, jamaa akajibu atakula baadae nkaona sura ya jirani ikakunjika baada ya miezi akaja kunisimulia siku hiyo alivochukia nkamwambia nilikuona tu.

Shost mwingine nae siku hiyo kachafua meza kaandaa makolokocho kibao yani meza ni imejaa msosi ukaekwa mezani wanamsubiri baba atoke job ale, saa mbili saa nne saa sita baba hajarudi ikabidi shost alale wala hakula kwa hasira ikafata ratiba ya ugali dagaa hiyo yote hasira nkagundua kumbe ni wengi inatokeaga.

Bila shaka hata wanaume wenyewe huwa hawajui kama wanatukera, kosa hata sio lao tupo katika mood ya kupika ila hawapo katika mood ya kula hivo basi tupike tu kwa ajili ya kuenjoy wenyewe sio kwa ajili ya mtu ila ikitokea na mlaji kaenjoy kwa kiwango kilichotarajiwa basi ni raha utamu....

Cheers
 
Kuna mzee aliniambia toka unakotoka hata kama umeshiba vipi, msosi wa home kula na umalize!

Hapo hata kama kulikuwa na soo linapungua uzito.

Heri ya X-Mass mama mchungaji!
 
Maisha wakat mwingine yanachanganya hadi mood inakata kabisa.

Ni vizur kuwa mnatuandaa kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kupika chakula pendwa sio unapika unachopenda ww
 
Tuko tofauti mimi napenda kula hiyo ni kama ibada kwangu, labda itokee nimeamka na hangover ndio ufanisi unaweza kupunguwa lakini kwenye menu sina mzaha.

By the way mimi mwenyewe ni mpishi mzuri kwahiyo naenjoy zaidi msosi wa kupikwa home kuliko kula vichochoroni kama jibwa.
 
Maisha wakat mwingine yanachanganya hadi mood inakata kabisa.

Ni vizur kuwa mnatuandaa kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kupika chakula pendwa sio unapika unachopenda ww
Wewe utakuwa unayachanganya maisha au mwanamke anakuchanganya siyo bure, maisha yakikuchanganya utakosa hamu ya sex tu na siyo kula otherwise wewe ni group la kina chapombee oyee kula si lazima bora kuyumba.
 
Haha,kweli kabisa hio inaleta hasira kwakweli,ni bora kumweleza mapochopocho ya leo ni nini na nini,atawahi kurudi mbona ilimradi tu ufurahi
Wanawake tunafurahishwa na kukwazika na vitu vidogovidogo ambavyo wanaume hawaelewi wakati mwingine....
 
Jifunzeni jinsi ya kujimarinate ..na muwe wawazi sio unakurupuka tu kuandaa menu yako ya ajabu tu halafu msosi huo huo kila siku bana!
 
Muwe mnatuandaa kisaikolojia mapema yaan ile jamaa yupo job unamtext kuna msos mtam unamtengenezea na mabusu busu kibao😊

Yaeh lazima umuandae mwenzako but yet kuna mda unataman kumfanyia surprise ya kupika kwa ustadi apendacho ila unaishia kukasirika
 
hii ilinikuta yaani nikajikoki mwenyewe na nnavyopenda kupika, kafika mwenyewe nikiangalia kitambi naona kipo juu juu nikajua tu huyu keshakula huko, kupakua akala tunyama tuwili kasema ameshiba,
na mie nikamsubiria akaandaa chakula chake cha usiku nikazungusha kiuno dakika moja nikashuka nikamwambia nimetosheka...
toka hapo kama hajisikii kula anatuma sms mapemaa
 
hii ilinikuta yaani nikajikoki mwenyewe na nnavyopenda kupika, kafika mwenyewe nikiangalia kitambi naona kipo juu juu nikajua tu huyu keshakula huko, kupakua akala tunyama tuwili kasema ameshiba,
na mie nikamsubiria akaandaa chakula chake cha usiku nikazungusha kiuno dakika moja nikashuka nikamwambia nimetosheka...
toka hapo kama hajisikii kula anatuma sms mapemaa
Kama unajuwa mume wako ni mtu wa mitungi usimuwekee miubwabwa usiku, kama ni special menu iwe ni weekend au umpe taarifa mapema unaandaa nini.
 
Yaeh lazima umuandae mwenzako but yet kuna mda unataman kumfanyia surprise ya kupika kwa ustadi apendacho ila unaishia kukasirika
Kweli suprise ina raha yake, na suprise ndo inachukiza zaidi make mambo yanakua tofauti
Aisee kuna siku nilifanya suprise ya pilau na Bata yani Bata nimemtoa mbali, kupata mtu wa kumchinja ikawa shida nimezunguka mtaa mzima nyumbu kwa nyumba utadhani naomba kura kumbe natafuta mchinjaji....nilivofanikiwa muda ulikua umeenda so nikaanza kupika fasta fasta nikaweka mezani nangoja muda wa kuvunja vunja mifupa ya Bata eeeh bebi anatoka safari kumcheki kafika wapi ananambia kushafika yupo kwenye kihotel anakula ndo aje nilikata simu yani nlikua kama nimepigwa shoti ya umeme nikaenda kulala hiyo ni saa saba mchana
 
Kama unajuwa mume wako ni mtu wa mitungi usimuwekee miubwabwa usiku, kama ni special menu iwe ni weekend au umpe taarifa mapema unaandaa nini.

hanywi pombe kabisa, na katika suprise huwa siweki wali mostly vitu vya kuchoma choma na vimchemsho.. ila Matola hivi ukiangalia tu meza na bashasha za mapokezi si unajua leo kuna jambo?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom