Huwa siwezi kumkatalia mtu akiniomba pesa, hata kama sina au nadhamiria kutompa

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
10,087
15,960
Wakuu mimi huwa nashindwa kumwambia mtu anaeniomba pesa kama, "hapana, sina pesa", yaani huwa inakua vigumu sana.

Yani ntajizungusha weeeee. Siwez mwambia kuwa "Aisee, sina hela hiyo"

Yani kabisa najua siwezi kumpa hiyo hela, ninaweza hadi kudanganya kuwa ntaangalia ila siwez kumwambia kuwa "Sina pesa, siwezi kukupa pesa"

Nyie wenzangu mnafanyaje inapotokea mtu anakuomba pesa halaf unajua huwezi kumpa? Yani huwezi kumpa kabisa, iwe unayo ama huna. Unapambana vipi na huyo mtu?

Au na nyie mnazunguka zunguka?

Uzi tayari
 
Sinaga maelezo mengi.

Ninayo nitakupa kama Sina nakujibu direct sina bila kupepesa macho.

Kama ninayo na unanikopa nakupa kile ambacho najua sitokudai ukileta umeleta profit kwangu naenda kulia bata.
 
Si bora wewe huwezi unajizungusha zungusha!

Sie wengine kama tunaona mhusika ni kweli ana shida na pesa hatuna, tunaweza hata kukopa mahali kwa ajili yake hata kama sio ndugu yako!!

Nina case ya mtu ambae aliniomba pesa zaidi ya miaka 5 iliyopita na nikashindwa kumpa! Huwezi amini, hadi kesho huwa inafika siku nakumbuka lile tukio la kushindwa kumsaidia!
 
Kibaya ukute umekopa kumpa
Kumbe mwenzio ni pesa ya weekend Tu ya bata anataka..
Na ukijaribu kumkumbusha
usha deni utasikia..
Aahh unanidai pesa ndogo hivyo..nikipata ntakupa...
Ndo ujue kweli mjini kuishi na watu kazi
 
Kiukweli hakuna hisia mbaya kama kumuona mtu anashida halafu huwezi kumsaidia kwa wakati huo, nafikiri hiki kitu kipo kwa watu wengi mimi mmojawapo. Lakini huwa nina majibu mawili tu either namsaidia hapohapo ama namwambia “nasikitika sina uwezo wa kukusaidia kwa sasa” halafu nabaki nikijisikia vibaya.

BTW, nakuona ona tu! 😀
 
BTW, nakuona ona tu!
Ni muda sijakuona
 
Kuna mwenzio aliishia kutopokea simu za watu, sababu yakukumbushiwa alichoombwa, wema usizidi uwezo huna sema sina sasa unavyoitika na kukubali wakati huna si kujitesa huko!
 
Kibaya ukute umekopa kumpa
Kumbe mwenzio ni pesa ya weekend Tu ya bata anataka..
Na ukijaribu kumkumbusha
usha deni utasikia..
Aahh unanidai pesa ndogo hivyo..nikipata ntakupa...
Ndo ujue kweli mjini kuishi na watu kazi
Mi mtu akitaka kuniona jeuri basi aniletee dharau kwenye pesa ninayomdai hata kama ni shilingi mia!
 
Kiukweli hakuna hisia mbaya kama kumuona mtu anashida halafu huwezi kumsaidia kwa wakati huo, nafikiri hiki kitu kipo kwa watu wengi mimi mmojawapo. Lakini huwa nina majibu mawili tu either namsaidia hapohapo ama namwambia “nasikitika sina uwezo wa kukusaidia kwa sasa” halafu nabaki nikijisikia vibaya.

BTW, nakuona ona tu! 😀
Halafu kuna ile siku cjui kwenye mada gani vile! Nikahoji mbona umepotea wewe...! Nikaona wacha nibishe hodi nisikie mawili matatu! Hadi sasa sikumbuki kilitokea nini hadi nikaishia mlangoni!
 
Hahah ntakucheki ndugu.
 
Back
Top Bottom